Msanii Belle 9 amewakosea nini Watanzania? Kwanini anapuuzwa? Ni wapi anakosea?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wana jamvi wasalaam...

Wana jamvi katika adhabu ambayo anaweza kupewa mtu na ikamuumiza sana na akashindwa kujua la kufanya au suluhu ni adhabu ya kupuuzwa.

Adhabu ya kupuuzwa ndio aliyo pewa msanii Bell 9 na watanzania walio wadau wa muziki! Bell 9 ni mmoja wa wasanii wenye sauti nzuri, mtunzi mzuri na mwimbaji mzuri lakini hakuwai kufurahia matunda ya kipaji chake kama wengine!

Bell 9 pamoja nakujua hayo yote na baadhi ya watanzania kusifu nyimbo zake lakini zimekuwa zikikosa muda wa hewani wa kutosha kama nyimbo nyingine na ni vigumu nyimbo kupata muda wa hewani kwenye radio station na Tv kama walaji hawauchagui wimbo husika!

Watanzania, Bell 9 amewakosea nini? Kwanini mna mpuuza kiasi hiki? Pamoja na msanii huyu kutoa wimbo mpya hivi karibuni lakini kwa utafiti nilio ufanya mapokeo yake ni madogo na ya kukatisha tamaa pamoja na wimbo husika kuwa mzuri sana.

Msanii Bell 9 anakosea wapi?

Aina ya studio anayo record?
Aina ya management aliyo nayo?
Aina ya utunzi anao utumia au nyimbo anazo imba?
Amejiweka mbali na mashabiki?
Kwakuwa hana kick au scandal?

Nimejiuliza maswali mengi lakini nimekosa majibu kabisa juu ya msanii huyu Bell 9 na huwa namuonea huruma pamoja na kuonesha juhudi lakini ana puuzwa sana ....hakika kwa jinsi anavyopuuzwa huyu msanii ningekuwa ndugu yake ninge mshauri atafute shughuli nyingine ya kufanya.

Kuna nyimbo zinapata air time ya kutosha hadi unashangaa, huyu Bell 9 ana shida gani?

Msanii Bell 9 amewakosea nini watanzania? ni wapi anakosea?

Karibuni wana jamvi.
 
Kuna masharti ya mganga kakosea...

Kwa hiyo unajaribu kusema wanamuziki wote wanao fanya vyema kwa sasa wana kwenda kwa Waganga? Unamshauri aende kwa waganga?
 
Mi mwenyewe naunga mkono hoja ila sometime its fortune that rules mans life!

Duu aisee kwa hiyo pengine hana bahati..sasa ni kweli kuwika kwa msanii kuna tegemea bahati pekee? Unaiongelea vipi management yake?
 
Mimi hajanikosea chochote na namkubali sana tu.Nyimbo zake alizowahi kuzitoa hakuna niliowahi kutokuupenda hata mmoja! Hata mimi hua nashangaa kwanini hatoki? Laiti ningekua na uwezo ningempa hata tuzo moja tu ya kumfariji.
 
Msanii Bell 9 anakosea wapi?
Aina ya studio anayo record?
Aina ya management aliyo nayo?
Aina ya utunzi anao utumia au nyimbo anazo imba?
Amejiweka mbali na mashabiki?
Kwakuwa hana kick au scandal?
Binafsi huyu dogo nimemkubali from the very first song! Hayo uliyotaja ni chanzo hususani hapo kwenye RED lakini in addition, ambalo nalo pia linachangiwa hapo kwenye RED, hivi sasa ukitaka uendelee kusikika basi na wewe mwenyewe hutakiwi kujipoteza bila sababu za msingi! Radio station huwa zinapokea nyimbo nyingi sana kwa siku hususani zile radio pendwa! Sasa msanii hata kama utatoa pini kali namna gani, ukipotea itafika wakati pini lako nalo litapotezewa coz' kila siku new hits zinaingia sokoni! Hivi sasa si kama zamani... mashabiki wana access na kusikiliza wimbo husika kupitia various sources; kwa sasa zaidi kupitia kwenye simu na kidogo kwenye radio na kwenye mitandao! Nyimbo ikiwa hit, kama usafiri wako ni daladala kila siku, basi kuna uwezekano kwenye kila route wimbo husika utasikika! Kutokana na hilo, it's obvious baada ya muda wimbo utapotezewa tu coz' mtu utakuwa umesikia mara kadhaa... angalu mara kumi kwa wiki!

So, ikiwa msanii utakuwa unakaa sana bila kutia nyimbo mpya, then prepare yourself to be left behind! Hata wewe Mkuu wangu Ruttashobolwa ingawaje unamkubali Diamond, nikikuuliza Nitampata Wapi umeisikiliza lini mara ya mwisho si ajabu huwezi kukumbuka! Now assume Chibu anakaa miezi sita bila kuachia track... si ajabu ndani ya hiyo miezi sita huyo Diamond utakuwa umesikiliza mara chache tu na zingine ni zile za kugongana na nyimbo husika just by chance!

So, pamoja na mchango wa mashabiki, msanii mwenyewe anatakiwa kuji-boost! Huyu Kiba ambae kila leo siku hizi Kiba, Kiba! tayari alishapotea coz' mwenyewe ali-opt kujipoteza!
 
Last edited by a moderator:
Mimi hajanikosea chochote na namkubali sana tu.Nyimbo zake alizowahi kuzitoa hakuna niliowahi kutokuupenda hata mmoja! Hata mimi hua nashangaa kwanini hatoki? Laiti ningekua na uwezo ningempa hata tuzo moja tu ya kumfariji.

Pamoja nakumkubali umewai kujiuliza ni wangapi wanao mkubali kama wewe huchagua nyimbo zake kwenye radio stations zichezwe? Kila mtanzani ukimuuliza utasikia ana msifu na kusema nyimbo zake ni nzuri na anazipenda lakini ukichukua wasaha wakusikiliza radio hata nusu saa huwezi kusikia nyimbo yake ikiombwa..hivi kuna nini
 
Binafsi namkubali Bele 9 kuliko hata Chibu, na bado naamini hapa alipo Chibu palitakiwa pawe mahali pa Bele 9 kama sio clouds kuleta fitina kipindi kile hawa wasanii wawili ndio "wanatoka".
 

Mkuu chige pamoja na hayo uliyo yaeleza pengine kuna kitu nimenotice kuhusu maelezo yako na ambacho nime kisahau kukiuliza ni kuhusu juhudi zake binafsi kupush mziki wake ikiwa na kujiweka karibu na mashabiki wake...na katika hilo nashindwa ni muhukumu vipi maana muziki wa sasa nabado napata shaka kuhusu ukaribu wake na media pamoja na wadau wa muziki!
Na kuhusu management yake bado napata mashaka na ufanisi wake na pengine ninge mshauri atazame upya..
 
Last edited by a moderator:
Mbona wapo wengi tu ambao muziki wao haupigwi?
Ruttashobolwa uweke huo muziki wake hapa ili tuusikie;

Mtie moyo tu, hata ubuyu ulianza kama mchicha.
 
Nina uhakika kila anayependa mziki ukimuuliza atakwambia jamaa anajua, yani kwa hili sidhani kama kuna team yoyote haimkubari.
Lakini hata mimi nashangaa inakuaje havumi kama wengine maana kuna watu wa kawaida wanavuma zaidi yake yeye.
Sometimes inawezekana ni bahati
 
Binafsi namkubali Bele 9 kuliko hata Chibu, na bado naamini hapa alipo Chibu palitakiwa pawe mahali pa Bele 9 kama sio clouds kuleta fitina kipindi kile hawa wasanii wawili ndio "wanatoka".

Mkuu katika hili ntakupinga kidogo..mimi sifikiri kama clouds wanapaswa kupewa lawama au media yeyote kwa kuwa wao wanawapa walaji wanacho kitaka!

Kwa hiyo unataka kusema Clouds hawapigi nyimbo yake? Clouds wataipaje nyimbo air time ambayo haichaguliwi na walaji? Mbona kuna radio nyingi bongo na hata huko air time hazipewi vyakutosha?
 
Mimi hajanikosea chochote na namkubali sana tu.Nyimbo zake alizowahi kuzitoa hakuna niliowahi kutokuupenda hata mmoja! Hata mimi hua nashangaa kwanini hatoki? Laiti ningekua na uwezo ningempa hata tuzo moja tu ya kumfariji.

Labda kwasababu hachukui wadada wakali macelebrities wa bongo.Huoni Nuhu Mziwanda pamoja na utahira wa ubongoni ana jina sasa kisa anamchukua shishi baby?

Hii ndiyo bongo.
 
Belle 9 kama matonya tu wanaimba vizuri ila ndo hivo...hadi nimehisi kuwaonea huruma

Mpaka wapate viskendo vya kijingajinga ndio utawasikia...hebu mshauri Belle 9 amchukue Wema au jokate. U ll prove that.
 
Management ni kitu muhimu sana.. pia awe karibu na fans wake kwenye social networks so that they can request his songs.....

Take my words Belle
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…