Msanii Ben Pol anusurika kufa baharini, Boti yao yazama

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Ni jana wakitokea kisiwa cha Mbudya kurudi Jangwani Sea Breeze kwa mujibu wa maelezo yake kufika katikati boti ikazima na ikaanza kuingiza maji na taratibu ikaanza kwenda chini bahati nzuri walikuwa wamevaa life jackets ndio boti ilivyowaacha na kuzama wakabaki majini wakielea bila kujua la kufanya kwa muda wa saa mpaka walipopita wavuvi na kuwaokoa.

Anasema anashukuru Mungu kwa kuwaweka hai kwani lilikuwa ni jambo la hatari mno isipokuwa kuna mtu mmoja hajulikani alipo na hata ilipofanyika juhudi kurudi Mbudya kumtafuta hakuwepo huko.

Hayo ndiyo maelezo yake mzee wa Sofia Sofia.

Binafsi natia shaka usalama wa vyombo vile kwenda Mbudya pia suala zima la uokoaji pindi ikitokea janga mfano wa hili,wadau tusipende safari za huko pasipo umuhimu.
 
Hii taarifa ungeileta baada ya tuzo za mama kuisha! watu wote wameelekeza macho yao wote kule
 
Kwani mbudya kuna nini kule ?
Kila msanii anaenda kule kuna nini wanachokifuata
 
Likija swala la maji tena bahari inabidi mi huwa sina hamu nalo...
Waanzishe ndege za kwenda mbudya...

Dah, huogopi kama mimi.Sipati picha ningekuwepo kwenye hiyo boat ingekuwaje!
 
naskia mwenzao mmoja hawajui alipo
ila wamejkaza sana mi wangekuta mwili unaelea network zmekata
 
Hahaaaa ungepata presha y kupanda na kushuka ......pia hata zote zinakuja kwa pamoja kifo kisikie 2

Ndugu yangu naogopa usafiri wa majini balaa.
Mimi hizo bata zinipite tu kwakweli, sitaki hata kusikia.Hasa nikiwaza meli zinavyopataga ajali watu wanavyoteseka....unakufa huku unajiona? Mungu anipitishie mbali.
 
Dah, huogopi kama mimi.Sipati ningekuwepo kwenye hiyo boat ingekuwaje!

Kuna wakati niliwapeleka wadogo zangu huko beach, nimekaa nikajisahau nikakuta wanaogelea...
Nilishtuka hadi nikatamani niwapige makonzi...
Kuogelea najua sana tu, ila sijawahi pata courage ya kuogelea kwenye maji ya bahari au mto...
Kila nikiwaza kwenda mbudya nahairisha safari...
Najiuliza siku nikienda zanzibar sijui itakuwaje.?...
 
Mhhh vile viboti vile nilijua ipo day,mi roho huwa ipo juu lazma nivae buoyer mapemaa,
Yani sitarudia kwenda tena huko
 
Ndugu yangu naogopa usafiri wa majini balaa.
Mimi hizo bata zinipite tu kwakweli, sitaki hata kusikia.Hasa nikiwaza meli vinavyopataga ajali watu wanavyoteseka....unakufa huku unajiona? Mungu anipitishie mbali.

Ni sawa bt kifo kiko kila mahali iwe angani,ardhi ila kifo cha maji unakufa huku unajiona
 
Ndugu yangu naogopa usafiri wa majini balaa.
Mimi hizo bata zinipite tu kwakweli, sitaki hata kusikia.Hasa nikiwaza meli vinavyopataga ajali watu wanavyoteseka....unakufa huku unajiona? Mungu anipitishie mbali.
maji mazuri kwa kuyanywa tu na uzingatie yasije kukupalia .
 
Mi jirani na hapo ila siwezi enda, naogopa maji sana. Yaani sitaki hata yaona
 
Wapinzani wake kwenye muziki walitaka wamtoe kafara ajiangali hasa yule aliyezoa tuzo za kubebwa,ni mtu wa ndumba sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…