Msanii Ben Pol anusurika kufa baharini, Boti yao yazama

Msanii Ben Pol anusurika kufa baharini, Boti yao yazama

Kuna wakati niliwapeleka wadogo zangu huko beach, nimekaa nikajisahau nikakuta wanaogelea...
Nilishtuka hadi nikatamani niwapige makonzi...
Kuogelea najua sana tu, ila sijawahi pata courage ya kuogelea kwenye maji ya bahari au mto...
Kila nikiwaza kwenda mbudya nahairisha safari...
Najiuliza siku nikienda zanzibar sijui itakuwaje.?...

Bora wewe, mimi nina ndugu huko Zanzibar lakini kila nikiwaza yale majanga ya baharini sitaki hata kupasikia!
 
Duuuuuh,tuzo 5 hazikutosha wanataka kumtoa kafara msanii mwenzao kama watoto hawana lengo ndo show zote afanye yeye ???? ( jus kidin)
 
Huko nilisikia safari watu wanataka tuende huwa nakumbuka hii story.
 
Ni jana wakitokea kisiwa cha Mbudya kurudi Jangwani Sea Breeze kwa mujibu wa maelezo yake kufika katikati boti ikazima na ikaanza kuingiza maji na taratibu ikaanza kwenda chini bahati nzuri walikuwa wamevaa life jackets ndio boti ilivyowaacha na kuzama wakabaki majini wakielea bila kujua la kufanya kwa muda wa saa mpaka walipopita wavuvi na kuwaokoa.

Anasema anashukuru Mungu kwa kuwaweka hai kwani lilikuwa ni jambo la hatari mno isipokuwa kuna mtu mmoja hajulikani alipo na hata ilipofanyika juhudi kurudi Mbudya kumtafuta hakuwepo huko.

Hayo ndiyo maelezo yake mzee wa Sofia Sofia.

Binafsi natia shaka usalama wa vyombo vile kwenda Mbudya pia suala zima la uokoaji pindi ikitokea janga mfano wa hili,wadau tusipende safari za huko pasipo umuhimu.
Huko Mbudya sio sehemu salama sana, r.i.p Pancho
 
Dah huku kulitaka kumuua Ben pol, kumemuua Pancho Latino who is next beware everybody!
 
Naona kila aliyeenda huko anaapa kutoenda tena .
Weekend hii na mimi nina safari ya huko nitaleta mrejesho.
 
Back
Top Bottom