Mtaalam
JF-Expert Member
- Oct 1, 2007
- 1,371
- 251
MSANII maarufu wa Uganda, Jose Chameleon amejirusha kutoka ghorofa ya tatu ya Hoteli ya Impala mjini Arusha na kusababisha kuumia vibaya ikiwa ni pamoja na kuvunjika miguu yote.
Chameleon ambaye amekuwa akitamba na nyimbo za Jamila, Mama Mia na nyingine alijirusha kutoka chumbani kwake katika ghorofa ya tatu ya hoteli hiyo alfajiri ya saa 11 kuamkia juzi.
Imeelezwa msanii huyo alishituka akiwa chini amevunjika miguu hiyo na walinzi walikimbilia eneo aliloangukia baada ya kusikia kishindo na kumkuta akiwa hawezi kuinuka.
Hata hivyo haikueleweka kilichomfanya msanii huyo ajirushe, baadaye wenyeji wake ambao ni Clouds FM waliokuwa wamemualika kwa ajili ya shughuli ya Fiesta ya Tanga juzi walibidi kufanya utaratibu wa kumpeleka hospitali.
Lakini baadaye walitakiwa kutomtibu na baba yake aliagiza ndege ambayo ilitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA na kumbeba na kumpeleka Uganda ambako amelazwa katika hospitali moja ya nchini humo akipata matibabu.
Kuumia kwa msanii huyo kulisababisha ashindwe kufanya shoo katika tamasha la Fiesta ambako kulikuwa na wasanii wengi wa Tanzania na yeye ndiye alikuwa mgeni aliyetakiwa kuongoza shoo hiyo.
Henry Mdimu, Tanga