Madimba jr
JF-Expert Member
- Aug 12, 2017
- 1,577
- 3,146
Hii ni habari njema kwa wasanii wa Tanzania kuona wanapewa heshima ya kutosha,tulishazoea kuona wanasiasa tu ndio wanapewa heshima kama hii,sasa ni zamu ya wasanii natamani siku nyingine kusikia Marijan rajabu primary school au King Majuto Road,au Ali Kiba Hospital,hapa tuweke team pembeni heshima ya Kitaifa ya wasanii wetu inahitajika sana mana wao ndio pekee wanaoitangaza nchi yetu kimataifa na sio team ya taifa wala Mh.Lusinde.