Msanii Fareed Kubanda 'Fid Q' afunga ndoa katika Msikiti wa Qiblatain Boko, Dar es salaam

floow

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Posts
411
Reaction score
855
Fareed Kubanda aka Fid Q ameikacha rasmi kambi ya makapera aliyodumu kwa muda mrefu, baada ya kufunga ndoa mwanzoni mwa mwaka 2019 na mchumba wake aliyemtambulisha mwaka jana.

Rapa huyo kutoka Mwanza hakutoa taarifa za awali kabla ya kufunga ndoa hivyo kwa wengi limekuwa tukio la kushtukiza. Wasanii wenzake waliohudhuria tukio hilo walimpongeza kwa hatua nzuri aliyofikia baada ya kuwa single kwa muda mrefu.

Siku chache zilizopita rapa huyo maarufu kwa jina la Ngosha, aliposti picha akiwa na mrembo ambaye jana alikamilisha usemi kwa kumpa heshima ya kuwa mkewe wa ndoa.

Wasanii wengi waliompongeza Fid Q na kuposti katika mitandao yao ya kijamii akiwemo Ambwene Yesaya maarufu AY aliyehudhuria ndoa hiyo.

“Hongera sana ndugu yangu @therealfidq kwa kufunga ndoa Inshaalah Mwenyezi Mungu Aibariki Ndoa Yenu ,” aliandika AY.
Babu Tale meneja wa Diamond amempongeza rapa huyo kwa kuandika katika ukurasa wake wa Instagram, “Hongera Mtani @therealfidq na karibu kundini Mungu awasimamie kuilinda ndoa yenu maana kwenye imani ya dini yetu hapa umepanda daraja. Kama nakuona utakavyo pasuka maana mama kwa kutoa kitu hatari nakumbuka ule msosi mpaka watu wakafungwa karata kwa utamu wa chakula.”

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msanii wa muziki wa Hip Hop Bongo, Fareed Kubanda maarufu kama Fid Q, leo Januari 1, 2019 amefunga ndoa kwenye msikiti wa Qiblatain ulipo Boko jijini Dar es salaam.

Fareed, amekata kiu ya mashabiki wake ambao walikuwa wanatamani kumuona anafunga ndoa, ambapo leo amelitimiza hilo.

Hongera sana Fareed Kubanda kwa kuvuta jiko, Mungu awabariki na kuwasimamia katika maisha yenu mapya ya ndoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…