Msanii G - solo

Msanii G - solo

ukwaju_wa_ kitambo

Senior Member
Joined
Sep 15, 2024
Posts
150
Reaction score
173
MSANII G - SOLO

"Msanii wa Tanzania Gerald Mwanjoka ‘G-Solo’ aliyewahi kurekodi wimbo mmoja na msanii maarufu wa hip hop wa Marekani LL Cool J uliojulikana kwa jina la Hip Hop Is Everywhere..

Pamoja na ule wimbo uliomtambulisha vyema Hapa Tanzania akiwa amemshirikisha msanii Inspector Haroun nime bahatika kuzungumza nae vitu kadhaa kuhusu muziki na haya ni machache kati ya Mengi nilizungumza nae G solo ambaye ni mwanaharakati & msanii wa Muziki Aina ya Rap " since 1994. Na harakati zake kwenye moment za Ant - Virus / Vinega zilizotokea miaka ya hapa katikati

Ukwaju wa kitambo: jambo la kwanza nilikuwa napenda kufahamu G - solo ni nani angalau kwa kifupi.

Msanii G - solo : jambo la kwanza napenda mfahamu herufi G katika nick name yangu " G - solo" imesimama kama hivi..

Herufi G - Gerald ambalo ndio jina langu harisi , lakini kwenye neno " solo" tafsiri / kirefu chake ni.. herufi " S" imesimama kama " saying , herufi "O" imesimama kama " On" na herufi " L" imesima kama " lycris " na mwisho kabisa herufi " O" imesimama kama " only ..

G - Gerald ( jina langu halisi)
S - saying
O - on
L - lycris
O - only.

Ukijumulisha herufi ama maneno yote hayo ndio inapatikana G - solo

Kiukweli kwenye upande wa shughuli zangu za Muziki mimi nimeanza mwaka 1993, na harakati zangu za Muziki nilianzia mkoani Dodoma, huu mwaka 1993 ndio nilikuwa nimemaliza / nimehitimu Elimu yangu ya Msingi " Darasa la Saba" uamuzi uliofuata nikaona ni bora nifanye Muziki ndio huo mwaka nikiwa mkoani Dodoma ndio nikaaza kujihusisha na mambo ya Muziki.

Mwaka 1995 ndio nikaondoka zangu Dodoma ili nielekee Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kufika katika jiji lile na nia yangu ilikuwa ni kutafuta fursa nyingine kubwa ki muziki, .

Ukwaju wa kitambo : je? Unaweza kunieleza ni wasanii Gani mlianza nao harakati za Muziki Enzi hizo.

Msanii G - solo : unajua Enzi hizo kila Eneo Au mkoa kulikuwa na wafalume wake kwenye upande wa Muziki ambao wanawakirisha lile Eneo kwenye upande wa Muziki ,

Hiyo ndio Siri ambayo watu wengi walikuwa hawajui ama hawaitambui,kama umesoma Historia ya Taifa letu la Tanzania , Enzi hizo ikiwa bado inaitwa " Tanganyika" ule Utawala wa kichief kwenye maeneo mbalimbali Tanganyika, ndivyo hivyo hivyo wasanii Enzi hizo walikuwa na Utawala wao kwenye mikoa ama maeneo wanayotoka ama kuzaliwa.

Naweza kukutajia baadhi ya wafalume ama ma chief ( wasanii ambao walikuwa wanataburika ama kuwakirisha mikoa yao Enzi hizo)

Jijini Mwanza.

1. Wepesi wa Akili
2. King cliff nigga

Mkoa wa Iringa

1. Crazy Doggy
2. Mangi
3. Mike tee

Mkoa wa Morogoro

Enzi hizo Afande sele akuwepo kwenye Ramani ya Muziki

1. Boy - G ( ndio alikuwa king wa Morogoro)
2. Master Bros ( aliyeimba mwimbo unaitwa " Nini maana ya Maisha")
3. G - Y
4. Kulikuwepo na Crew inaitwa ( Sky magic) katika hii Crew ndio unakutana na wasanii kama Vile Geoffrey Tumaini " Dudu Baya"
5. Mwingine alikuwa ni msanii Squezer pale morogoro ingawa Asili yake ni mtu wa Iringa.
6. Salama S.k ambaye kwa sasa ni meneja wa msanii Nasibu Abbudul " Diamond"

Mkoni Arusha.

1. Crew ya Explastaz
Na makundi mengine mengi

Mkoa wa Mbeya

1. Joseph mbilinyi ( mr 2)
2. Doctor Y
3. Adili chapakazi

Mapambano na hawa wasanii pamoja na makundi yalikuwa yanafanyika mikoani ila final ilikuwa inapelekwa Dar Es Salaam ili kwenda kumpata mshindi kwa Tz nzima kwenye upande wa sanaa ya Muziki hapa Tanzania.

Kwa upande wa jijini Dar Es Salaam kulikuwa na makundi kama:

1. Kwanza Unit ( K.U)
2. Hard blasters Crew ( H.B.C)
3. Gangster with matatizo ( G.W.M)
4. Ugly Faces ( kina mack dizzo na mwenzie Dazz)
Lakini Crew ya Gangwe Mob imekuja Baadae.

Ukwaju wa kitambo: je ni makundi ama wasanii Gani ambao walikuwa wanakuumiza kichwa Enzi hizo kutokana na ubora wa uandishi ama kazi/ project zao ..

Lakini ni wasanii Gani waliku inspire kufanya Muziki..

Msanii G - solo : cha kwanza walioniumiza sana kichwa kwenye mambo ya ushairi wa mashairi ni Crew ya kwanza unit, kundi la pili ni G.w.m, but me I was not inspired na makundi/ Crew za muziki kutoka hapa Tanzania.

Nilikuwa inspired na msanii saleh jabir ndio alikuja kuniboost mimi , mimi nilikuwa na Desturi ya kungeuza nyimbo za kimarekani to kiswahili ila kwa style ya kiutofauti ( sio tafsiri ama maana ya kile wanachokiimba katika nyimbo za kimarekani Hapana!.. ) ,

Kwa mfano msanii / Rapper snoop doggy anavyosema one, two, three to the four.

Mimi nilikuwa nabadili na kusema hivi.

" mi nakuonya sikia tu Mtoto"

Nilikuwa nachange maneno hiyo ndio ilikuwa style yangu ya kurap Enzi hizo,

Ukwaju wa kitambo: je? Ukiachana na hi hit song inaitwa " heka heka za Teacher " ambayo watu ama wadau wengi wanaifahamu uliyomshirikisha msanii kutoka Crew ya Gangwe mobb " inspector haroun je? Zipo zingine.

Msanii G - solo : OK nilifanya kazi moja inaitwa " Weekend " wimbo wa weekend ulifanya vizuri sana sokoni ila kabla ya kutoa wimbo huo wa weekend, wimbo wangu wa kwanza ulikuwa unaitwa " leo ni leo " nilirekodi mwaka 1995, kazi hii nilirekodi katika Studio za " Mawingu Studio" na hii ndio ngoma ambayo iliwatambulisha kundi/ Crew ya wale kina Dada wanaitwa " Unique Sisters" kwenye muziki kwa Sababu mimi ndio niliongea na kaka yao ambae kwangu alikuwa ni Rafiki yangu wa Karibu.. na Support ya kaka yao ndio iliyonifanya kufanya kusafiri kutoka Dodoma to Dar es Salaam Enz hizo.

Itaendeleea..

Ukwaju wa kitambo
0767 542 202

IMGP2586.JPG
 
HUU UZI UPO CELEBRITIES SASA UMEOANA HAITOSHI UMELETA HUKU TENA. HATUTAKI UCHAFU. JUMLA NI TATU SASA.
 
Back
Top Bottom