ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
Tunaendelea pale tulipoishia kwenye kipande kilichopita , mahojiano yangu " Ukwaju wa kitambo na msanii " G solo"
Msanii G solo : Kaka yao na wale kina Dada Crew ya " Unique sistes" ilinipa support kubwa sana kwenye upande wa ghalama za usafiri kutoka Dodoma hadi Dar es Salaam, ukaribu wetu tuliishi zaidi ya urafiki ikafika time tukawa kama ndugu, ndio kitu ambacho hata mimi kilinifanya nione umuhimu wake katika maisha yangu nami sikuwa na hiyana kwake. Nikatoa shavu kwa Dada zake maana nao walikuwa bado wanajitafuta kwenye Game ya Bongo fleva In short walikuwa bado ni ma under Ground wanatafuta upenyo kimuziki..
Kuanzia hapo nadhani mimi msanii G - solo nikawa nimewafungulia mlango kwenye sanaa ya Muziki wa Bongo fleva nchini Tanzania Crew ya " Unique sisters" , juhudi zao pamoja na kipaji chao ndio nguzo muhimu iliyowapelekea wao kupata project nyingi kutoka kwa wasanii mbalimbali nje na ndani ya mipaka ya Tanzania , baada tu ya Collabo yangu kila msanii akawa amewatazama kwa jicho Tatu na kutamani kufanya nap collabo ama kazi na wasanii hao wa kike " Unique Sisters " ambao walikuwa ni Ndugu..
Kipindi hicho tukija kwenye suala nzima la kurekodi , Tulikuwa tunarekodi katika Mazingira Magumu Sana Tofauti na sasa, Tulikuwa hatufahamu kama kesho yake itakuwa nzuri kama ilivyo hivi hii leo. Wasanii wamepata wepesi katika suala nzima la kurekodi ( Audio & video production) kwa kifupi mimi msanii G - solo nilipitia mambo mengi katika Muziki Wangu nadhani hata haya ninayokuelezea hayatoshi kueleza mapito yangu yote katika safari yangu ya Muziki Since 1993.
Ukwaju wa kitambo: je? Ni Tukio Gani ambalo ulilipitia katika safari yako ya muziki, jambo ambalo kantu uwezi kulisahau katika Maisha yako..
Msanii G - solo : jambo la kwanza ambalo nalikumbuka na liliniumiza sana moyo wangu. Ni pale nilipo Record nyimbo zangu Tatu [3] katika Studio ya " Mawingu Studio " kwa producer Dj " bonnie luv" kisha baada ya siku kadhaa likatokea tukio pale studio za " Mawingu Studio" kuna baadhi ya vifaa vya Studio viliibiwa , zile kazi zangu Tatu [3] ambazo Tayari nilikuwa nimekwisha Record ziliibiwa na wale wezi / majambazi ile siku ya Tukio..
Iliniumiza Sana kwa Sababu mimi Enzi hizo / kipindi hicho nilikuwa natokea Dodoma , na nikitazama maisha Yangu yalikuwa ya kipato cha chini sana , sometime mimi G - solo nafanya uamuzi mgumu najinyima kufanya baadhi ya vitu ili niweke tu fedha za kulipia Studio maana nilikuwa nina Sprit ama passion ya kufanya Muziki, .
Baada ya lile Tukio ndio nikawa na Mawazo Mengi nitapata wapi? Tena fedha za kurekodi ngoma zangu Studio , kwa hiyo hilo Tukio lilinichanganya sana Akili Yangu kusema na ukweli..
Na kipindi hicho kurudia kurekodi nyimbo Studio ilikuwa Ngumu sana kwa sababu Tulikuwa tuna Record kwenye Tape moja (1) Maalumu , .Na Mic iliyokuwa inatumika kurekodia ngoma Enzi hizo Studio ilikuwa ni mic 🎤 ya hotuba ( hizi Mic zinazotumika na wanasiasa kwenye majukwaa). Ndio tulitumia kurekodia nyimbo tukiwa mule Studio Enzi hizo " Katika studio za " Mawingu Studio" Tofauti na sasa Wasanii wanatumia mic Aina ya " Condenser Microphone" ...
Zamani kulikuwa hamna kurudia maana ilikuwa ni "One Take" inawapasa wasanii wote mnao imba ama kurekodi ule wimbo muwe wote studio , sehemu inayo hitajika wasanii sisikike sauti mbili inapindi wote wasanii mnaopaswa kuweka ama kutia maneno katika hiyo sehemu muimbe kwa pamoja, Tofauti na sasa kila msanii anaingiza vocal studio kila msanii kwa nyakati tofauti tofauti , sehemu penye mistake unaweza kurudia ila kwa upande wetu sisi jambo / kitendo hicho cha kurudia ilikuwa hamna lakini pia sisi wasanii wa zamani tulikuwa makini sana wakati wa kurekodi , ndio maana Asilimia kubwa ya wasanii wa zamani , walikuwa na Desturi ya kufanya mazoezi ya Uimbaji wa ngoma zao kabla ya kwenda studio kurekodi mara kwa mara almost kama wiki 1 ama wiki 2 kabla ya kwenda kurekodi studio ili kuepusha hizo mistake na vitu vingine kama vile nyakati za kurekodi ngoma studio..
Pia kick & snare zilikuwa juu sana wakati wa kurekodi kwenye zile Beat pale "Mawingu Studio"
Kwa hiyo ilihitaji msanii awe na power ya kutosha ili aweze kutoa zile punch ryhems zake kwenye mic ili maneno yake yaweze kusikika Vizuri , cha Tatu uwe na pumzi ,pumzi itakayokuwezesha kuimba nyimbo yako hadi mwisho bila kukata pumzi,..
Na mwisho kabisa yale mazoezi yalitusaidia Sana sisi wasanii wa zamani kukalili zile Beat ama midundo na kutuwezesha kufahamu kuwa sehemu hii ya beat niweke mashairi haya na pale niweke mashairi yale kutokana na Aina ya midundo na mashairi niliyoandika mimi msanii kwa usaindizi wa producer, maana wao ndio walikuwa wanatoa muongozo namna ya uimbaji katika zile Beat.
Na nina kumbuka Collabo yangu ya kwanza kupewa ama kurekodi nilipewa shavu na Crew ya G.W.M inaitwa "Bwana kidevu" .
Itaendelea..
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202