Msanii maarufu kwa jina la Gachi, ambaye aliwahi kuimba wimbo wa “Samia Tunamkubali, Mama Asemewe”, amelalamikia kuvunjwa kwa sehemu yake ya biashara mkoani Singida.
Kupitia malalamiko yake, Gachi amesema kuwa pamoja na wafanyabiashara kulipa kodi, bado wanakabiliwa na vitendo anavyodai kuwa ni vya manyanyaso na kuvunjwa kwa maeneo yao ya biashara.
Ameomba waandishi wa habari waliopo Singida kufika katika eneo hilo na kushuhudia hali ilivyo, huku akitoa wito kwa wananchi kuungana katika kudai haki na kusimamia maslahi ya wafanyabiashara wanaodai kuathiriwa na zoezi hilo.
Your browser is not able to display this video.
Video hii akiwa anakata viuno jukwaani kwenye kampeni za CCM 2025
Itakuwa banda lake kalijenga juu ya mtaro/mfereji wa maji ya mvua. Hawa mbona wako wengi tu miji mbalimbali nchini wameambiwa wajihadhari na el nino kwa kuzibua mifereji na mitaro iliyozibwa na matakataka pamoja na kujaa udongo. Vibanda vingi vimeondolewa mitaroni
Unakuta mmachinga kajenga kibanda chake juu mfereji/mtaro wa maji ya mvua na umeziba. Mvua kidogo tu maji yanajaa barabarani hayana njia ya kwenda mbaki na watu. Miji mingi mingi imetangaziwa kuzibua mitaro na mifereji yao kujiandaa na el nino. Ni safishasafisha ya njjia za maji ya mvua