Msanii Gachi aliyeimba wimbo wa “Samia Tunamkubali, Alalamikia Kuvunjwa kwa Biashara Yake Singida

Kumtaja taja Rais haina msaada wowote kama hufuati utaratibu.
Naipongeza sana Serikali kwa zoezi hili ...
Tabia ya kufanya biashara barabarani na maeneo yasiyo rasmi ni ya kipumbavu sana...
 
2030 napaona mbali sana
 
Mleta mada ni jamii ile ya minyumbu iliyojazana JF ikinung'unulanung'unula bila mpango. Hiyo picha uliyomuonyesha akiwa jukwaani mwenzio hapo alikuwa anapiga kazi iliyompatia hiyo biashara. Sasa ukitaka asifanye kazi mwishowe awe km nyie manyumbu?!!!!

Kwani ukiwa msanii uliyewahi kumpamba Raisi B's ndo unakuwa juu ya Sheria?!!! Nyambaaaf
 
Kumuimbia Samia haina maana uvunje sheria.
Wewe ni machinga na machinga wengi wameondolewa vibanda vyao walivyojenga kihasara hasara.
Fuata sheria na uimbe vizuri.
 
Kwani wamemvunja kiuno, aendelee kukata viuno aone kama kuna mtu atathubutu kuivunja hiyo biashara yake mradi tu visiwe vigodoro hadharani.
 
Sasa ukimuimba kiongozi ndiyo ruksa kutofuata utaratibu?..
Huyo kiongozi anafuata utaratibu upi? Ule wa kuua watu hapo October 29? Au wa kuiba kura na kujitangaza mshindi? Chauma walipata kura ngapi za jumla hata wapate viti maalum bungeni?
Utaratibu manake nini??
 
Serikali ipi sasa unayotaka ikusaidie wakati ndio hiyo hiyo inayoondoa mabanda...

😀
Ndio uone huyu dada mjinga sana....ukimuangalia kajipodooooa utadhani ni mtu kumbe kichwa cheupeee...
 
Hivi wakuu ingetokea kibanda chake pekeyake kimeachwa mngesema nini?
 
Ila hii nchi 😂😂😂
Kwamba akiwaimbia ccm ndo avunje sheria!? Hapo na bado wategemee mengi
 
Kwani ukimwimbia nyimbo Rais ndio sababu ya kuvunja Sheria?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…