Msanii gani kufunika fiesta 2018?

Fiesta imeanza2001 wasafi wameanza lini...!!
Na wanafanya vzr tuuu!!!!!
 
Hawapo ila Tanzania hii kuna wasanii wengi kushinda hao WCB naamini itafanya vzr...japo Mimi sitahudhuria kulingana na umri wangu kwa sasa!!!ila wapo!!!
Kiuhalisia sa hivi wasanii hawapo wengi kama zamani, ukitoa WCB na baadhi wanaojitambua waliobaki ni kina Gigy Money na Amber Lulu
 
Kiuhalisia sa hivi wasanii hawapo wengi kama zamani, ukitoa WCB na baadhi wanaojitambua waliobaki ni kina Gigy Money na Amber Lulu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] amber Lulu nae msaniii au gigy money!!!
 
CMG bado wana nguvu hasa upande wa wasanii. Wasanii wengi bado hatima yao imeshikwa na CMG. Hapa tz ni wasanii wachache sana ambao wapo independent pasipo kuhitaji mbeleko ya CMG. Hivi leo hii zikitangazwa show mbili siku moja huku CMG huku WCB halafu kote Maua Sama anahitajika, unadhani ataenda wapi? WCB walichofanikiwa ni kutengeneza himaya yao ila ni wao peke yao wanaoweza kulindwa na himaya hiyo, wasanii wote Walio nje ya WCB hatima yao haiwezi kulindwa na WCB.
Halafu CMG wanaujua huu mchezo, tokea 2011 wanafanya hizi mambo, ramani zote wanazo kiganjani, WCB wasijaribu kupimana msuli na CMG itawacost. Msanii yeyote atakaye ungana na WCB katika hii vita ajue tu kuna maisha baada ya huu upepo kutulia!

Huo ndio mtazamo wangu
 
CMG ilikuwa inawajenga wasanii na kuwabomoa wao wenyewe.
Ila kinyago walichokichonga (diamond), kinawatisha sana kama walikinunua vile.
Wasanii wengi sana sasa hivi wanatamani kuwa sehemu ya WCB angalau wapate kubaki kwenye ramani. Ni wasanii wangapi wamekuwa chini ya CMG kwa muda mrefu sasa hivi wameishia kupata hela ya kupanga Kinondoni na Sinza tu? Wananyonywa na wanajua kama wananyonywa ila hawajazikomaza akili zao.
 
Fiesta imeanza2001 wasafi wameanza lini...!!
Na wanafanya vzr tuuu!!!!!
Eti namimi ndio Nashangaa me bado naamini Fiesta ze best burudani. Kama dogo Janja mbona anahit song, uje Nandi uje fidq, uje linah, uje mauwa Sama, billnass, uje richmavoko, uje rubby, uje kuna kundi hivi lavijana watatu Jina Lao nimelisahau kidogo mbona wasanii tunao kibao jamani ukiachana na WCB
 
Clouds siku hizi ni wa kawaida sana maana hata wasanii wanawachukulia kawaida sana tofauti na zamani
Zamani kulikuwa na iman et usipoenda kutambulisha wimbo wako clouds (xxl) basi hiyo nyimbo haitakuwa hiti lakin sahiv wasanii hawaendi kutambulisha na ngoma zinakuwa hit mfano kwangwaru haijatambulishwa clouds lakin ndio ngoma kubwa mwaka huu mfano mwingine dogojanja wimbo wake wa #banana hakwenda kutambulisha clouds lakin ni wimbo unaofanya vizuri ikumbukwe tu banana wimbo wa dogojanja ulitambulishwa kwa mala ya kwanza wasafi TV
 
Zilipendwa hizo enzi, hivi sasa social networking ndio kila kitu zina nguvu kuliko redio na TV. Ili upepo utulie basi nguvu ya radio na TV iipite ya social networking jambo ambalo haliwezakani na halitowezekana kwa dunia ya sasa hivi, kwani radio na TV source yao kubwa ni social networking, ila social networking inajitegemea na ndio maana siku hizi nyimbo inaachiwa YouTube, instagram, Facebook etc, bila kufanya media tour na bado ina hit. Ndio maana kila radio ina acc ya fb, YouTube, instagram etc na mwisho kaangalie tafiti, wasikilizaji wa radio na TV wamepungua sana sababu ya hizi social networking na WCB wanajua kuitumia nguvu yao ya followers huku social networking na ndio maana Lava lava na Mbosso hawaja pewa promo na CMG na EATV na radio, lkn kila nyimbo wanayoitoa ina viewers zaidi ya 1m, ndani ya mda mchache, ukienda iTunes Kenya wanakimbiza, ukija boom play nyimbo zote ni zao. Ile miaka ya kusema bila wao husongi mbele inazidi kuyoyoma, social networking hivi sasa imekuwa kama kilevyi na Kuna watu wapo tayari wakose hela ya kula na si bando.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…