Hua nashangaa sana ni kwamba Tanzania kwenye upande wa burudani watu ni wapenzi sana wa mziki wa magharibi kuliko wa kiafrika...muda sana sijasikia wasanii haswa wa kongo wakija kupiga show za nguvu hapa kwetu, tangu Fally Ipupa N'simba a.k.a Dicap la merveille, a.k.a El pibe de oro, a.k.a El Maravilloso, a.k.a 3x Hustler, a.k.a El Rey Mago, a.k.a Champions love, kuja bongo sijaona msanii mwingine wa kongo ... sitaki kabisa kumzungmzia Koffi Olomide maana alikuja kimashauzi sana na kupiga ngoma moja tu ya Selfie ..
Nmeona live concerts za Hervé NGola Bataringe a.k.a Ferre Gola na akina Cindy yani unainjoi...basi bajitokeze batu bazamini baletee sisi bapenzi ba muziki ba kongo.
View attachment 609511
View attachment 609512
View attachment 609514
View attachment 609515
Brother nakukubal katika music la kongoWasikupotezee muda Mkuu ukitaka kweli ujaze ' Nyomi ' la Kufa Mtu halafu urudishe Pesa yake na upate ya ziada kabisa na uwafurahishe Watanzania wengi wanaojua ' ladha ' halisi ya Muziki wa Kikongo na Mafundi wa huo mziki basi mlete huyu Mtu Jean Bedele Tshituka Mpiana ( JB Mpiana )a.k.a Mukulu ya Bamukulu a.k.a Souverain a.k.a De La Patria a.k.a Moto Pamba a.k.a Bin Adam a.k.a Lonkia Milo Dan Koko a.k.a Leadere Charismatique a.k.a Mokonzi Ya Fikin na Bendi yake nzima ya Wenge Musica BCBG ( Le quipe Nationale / Timu ya Taifa ) utaona ' balaa ' lake kwa Tanzania nzima ' itatikisika ' na ndipo utajua kuwa siku zote GENTAMYCINE Mimi huwa sipendi vitu ' vibovi vibovu ' na ninachokipenda Mimi basi jua hata Mwenyezi Mungu nae pamoja na Malaika wake wote Wakuu Mikaela na Gabrieli nao wanapenda hivyo hivyo.
Sijaona kama JB Mpiana DRC nzima na hakuna Bendi mahiri na inayopiga vizuri muziki wa ' Live ' kama Wenge Musica BCBG na hakuna Bendi DRC nzima ambayo ina ' Rapa ' fundi na balaa kama Wenge Musica BCBG aitwa Pitshou Lisimo a.k.a GENTAMYCINE kwani hata hii jina la hii ID yangu pendwa nimelitoa Kwake huyo ' Rapa ' wenyewe Kongo wanaita ' Atalaku ' na Wafaransa wanaita ' Animateur ' na kwa Kiswahili chetu tunaita ' Mghani '.
Mkuu ukimleta JB Mpiana na Wenge Musica BCBG nchini Tanzania ' hakyanani ' utakuwa umenifurahisha hakuna mfano.
...JB wa miaka ileeee, sio huyu wa leo...Brother nakukubal katika music la kongo
Hao jamaa nawakukubali sana pia
Ila angalia wasanii wa ajabu ajabu wanakuja kufanya show huku kwetu...vitu vya ajabu ajabu tu
Werrason ana album mpya now....aje kuitambulisha bongo..
Monica seka
Duuh jamaa yuko vizuri aise...JB wa miaka ileeee, sio huyu wa leo...
...JB wa miaka ileeee, sio huyu wa leo...
Wanapiga vizuri sana ...kama huamini angalia live concerts zaoHivi Kongo bado wanapiga mziki???
Kabisa mkuu...kuna show moja matata sana alipiga pale UKferre golla--muzee ya 3eme de toit..100 kilos....vita imana........HAPO KWA SLOW RHUMBA NI MWISHO
Mshono unakusumbua!, nilisema ni JB wa enzi zileeee, siyo huyu wa leo!, kipindi hicho alizungungwa na watu wakali...Mpera, Aimelia...baada hao kusepa kipi umekisikia kutoka kwake?....kuna mafaninio yeyote kutoka kwake album alizotoa?...mambo magumu kwake...ni miaka mingapi hajatoa album?...anajua itabuma..kila kila siku anasogeza mbele uzinduzi anadai kulogwa....Humjui JB Mpiana Mkuu hivyo tuliza tu huo ' mshono ' tafadhali. Kama mpaka leo hakuna Mwanamuziki yoyote yule wa Congo DR kuanzia wale ' Manguli ' akina Koffi na Werrason achilia mbali hawa akina Fally na Ferre ambao wameweza kuvunja rekodi ya JB Mpiana kwa ' Kutapisha ' Kumbi Kubwa za ' Miziki ' ya Kikongo duniani kama za Zenith, Bercy, Olympia zote za Ulaya huko Ufaransa na Ubelgiji na huu wa Bandal jijini Luanda nchini Angola leo hii utasemaje JB Mpiana wa miaka ile siyo wa leo? Shika adabu yako tafadhali. Hakuna kama JB Mpiana na Wenge Musica BCBG Congo DR na ukitaka ' ladha ' na ' burudani ' tosha ya muziki wa ' live ' Wenge Musica BCBG ya JB Mpiana haina mfano na hili halina ubishi labda uwe tu na Hila / Ngendembwe zako tu.
Naona m
Mshono unakusumbua!, nilisema ni JB wa enzi zileeee, siyo huyu wa leo!, kipindi hicho alizungungwa na watu wakali...Mpera, Aimelia...baada hao kusepa kipi umekisikia kutoka kwake?....kuna mafaninio yeyote kutoka kwake album alizotoa?...mambo magumu kwake...ni miaka mingapi hajatoa album?...anajua itabuma..kila kila siku anasogeza mbele uzinduzi anadai kulogwa....
Hebu ngoja niitafute hiyo album! Maana hiyo masifa unayo toa kweli hii bendi yako. Lakini upo vizuri! kweli wewe ni mtaalam.JB Mpiana hajawahi kuwa na Mwimbaji aitwae ' Mpera ' bali alikuwa na mwimbaji wake ' Kipenzi ' aitwae Alain Mpela ' Afande '. Kuhusu JB Mpiana kutoa Nyimbo mpya na ndiyo maana nilikuambia mapema tu kwamba ' tuliza mshono ' kwani huna unachokijua kuhusu Mwanamuziki Kipenzi changu JB Mpiana na Bendi yangu Pendwa ya Wenge Musica BCBG. Album mpya kabisa ya JB Mpiana na Kundi lake zima la Wenge Musica BCBG inaitwa ' Balle De Match ' ambapo humo kamtambulisha ' Rapa ' mpya kabisa na anayekuja kwa Kasi aitwae Fusee De Geirre ambaye amekuja kuziba nafasi ya yule Rapa Marehemu Faustin Nzinga Yankobo a.k.a CELLULAIRE Mokili Mobimba. Itafute hiyo Album halafu usikie ' Chemistry ' nzima ya ' Marapa ' akina GENTAMYCINE na Fusee De Geirre uone balaa lake huku katika Solo Gitaa akisimama mwenyewe safari hii Mitre Ficarre Mwamba na katika Rythm Gitaa akiwemo Kijana mpya kabisa aitwae Zygal na kama kawaida katika drums / chips yupo mwenyewe ' Mtaalam ' Seguen Mignon Maniata Ikuzu huku kule katika Vinanda kama kawaida wakiwepo ' Mafundi ' wale wale akina Geremi Kitubu na Cedric Gezeula na katika Ngoma za Tumba akiwemo Kijana mpya aitwae Zullu Mbonda na katika Bass Gitaa akiwepo yule yule Sunda Bass Le Pro.
Mkuu achana kabisa na Wenge Musica BCBG ya mwenyewe JB Mpiana kwani ni moto wa kuotea mbali tena sana au mno tu.
Hebu ngoja niitafute hiyo album! Maana hiyo masifa unayo toa kweli hii bendi yako. Lakini upo vizuri! kweli wewe ni mtaalam.