BilioneaPATIGOO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2012
- 12,320
- 11,327
- Thread starter
-
- #41
Hahaha hapa ndo napokukubali brotherJB Mpiana hajawahi kuwa na Mwimbaji aitwae ' Mpera ' bali alikuwa na mwimbaji wake ' Kipenzi ' aitwae Alain Mpela ' Afande '. Kuhusu JB Mpiana kutoa Nyimbo mpya na ndiyo maana nilikuambia mapema tu kwamba ' tuliza mshono ' kwani huna unachokijua kuhusu Mwanamuziki Kipenzi changu JB Mpiana na Bendi yangu Pendwa ya Wenge Musica BCBG. Album mpya kabisa ya JB Mpiana na Kundi lake zima la Wenge Musica BCBG inaitwa ' Balle De Match ' ambapo humo kamtambulisha ' Rapa ' mpya kabisa na anayekuja kwa Kasi aitwae Fusee De Geirre ambaye amekuja kuziba nafasi ya yule Rapa Marehemu Faustin Nzinga Yankobo a.k.a CELLULAIRE Mokili Mobimba. Itafute hiyo Album halafu usikie ' Chemistry ' nzima ya ' Marapa ' akina GENTAMYCINE na Fusee De Geirre uone balaa lake huku katika Solo Gitaa akisimama mwenyewe safari hii Mitre Ficarre Mwamba na katika Rythm Gitaa akiwemo Kijana mpya kabisa aitwae Zygal na kama kawaida katika drums / chips yupo mwenyewe ' Mtaalam ' Seguen Mignon Maniata Ikuzu huku kule katika Vinanda kama kawaida wakiwepo ' Mafundi ' wale wale akina Geremi Kitubu na Cedric Gezeula na katika Ngoma za Tumba akiwemo Kijana mpya aitwae Zullu Mbonda na katika Bass Gitaa akiwepo yule yule Sunda Bass Le Pro.
Mkuu achana kabisa na Wenge Musica BCBG ya mwenyewe JB Mpiana kwani ni moto wa kuotea mbali tena sana au mno tu.