TANZIA Msanii Golden Jacob Mbunda(Godzilla) afariki dunia

MSTAAFU RAISI JAKAYA KIKWETE : >>>Nimestushwa na taarifa za kifo cha msanii wa kizazi kipya GodZila. Alikuwa kijana mdogo mwenye ndoto kubwa na ameondoka wakati ambapo bado mchango wake ulihitajika. Nawapa pole familia ya Marehemu na wasanii wote kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema.
 
Daaaaaah RIP Zilla... Ule wimbo wa Salasala... Utanikumbusha wewe Daima


-All Star Zimeanikwa juu ya nyaya za Umeme (Wauza Ngada)

-Njoo kwa Hekima na nakupa tahadhari kuna wakabaji wanapiga ngumi kama mabondia.

-Kwa ajili ya shortcut masela wanapata mkwanja ukiona na mabegi ujue ndani yamejaa ganja.

WESTSIDE SALASALA.
 
Mwili wa mwanamuziki, Golden Jacob ‘Godzilla’ uenda ukaagwa sehemu tatu kabla ya kuzikwa kwenye makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Baba mlezi wa Godzilla, Antoni Kato amesema hapo awali walipanga bajeti ya mazishi milioni sita na nusu, lakini imeongezeka kuwa milioni nane kutokana na jana usiku saa nne baadhi ya wasanii kuomba aagwe Leaders msanii huyo.

Kato alisema familia ilipanga Godzilla aagiwe nyumbani kwao Salasala na baadae kanisani, lakini limejitokeza suala la wasanii wenzake kuomba aagiwe Leaders.

Hata hivyo Kato alisema leo jioni watakaa kikao kuamua kama itawezekana Godzilla mwili wake ukaagwa sehemu tatu ambazo ni nyumbani, kanisani na Leaders sababu watu wote wanaumuhimu kwake.

"Habari iko hivi, sababu Godzilla alikuwa mtoto wa Salasala, watu wa Salasala wameomba wamuagie Salasala, sasa kuna uwezekano tukafanyia Salasala tu, na suala la Leaders wasanii wenzake jana usiku walikuja kuomba, hili ombi tunalifanyia kazi, lakini kama ndugu wa karibu wakisema aagiwe Salasala tu tutamuaga Salasala, kwa sababu Salasala ndio ibada itafanyika hapo nyumbani.

"Si unaona huo mkanganyiko, ndio maana tunajaribu kuona kama ratiba itawezekana, tujipange tufanyie Salasala, halafu twende kwenye ibada na baadae twende Leaders tukimaliza hapo tunaenda Makaburi ya Kinondoni kuzika, sababu ni maeneo ya hapo hapo, ndio maana nasema bado tunalifanyia kazi na yote yawezekana tu na hatuwezi kumuuzi huyu tukamfurahisha huyu," alisema Kato.

Kato alisema yeye amemlea Godzilla tangu alivyokuwa na umri wa miaka miwili pindi alipofiwa na baba yake, hivyo kwa upande mwingine ni jirani yake.

Godzilla amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumatano ya Februari 13, 2019 majira ya saa 10 alfajiri nyumbani kwao salasala jijini Dar Es Salaam, baada ya kusumbuliwa na Malaria pamoja na presha.
 
"Nafanya mishe mishe zangu town,ghafla mood yangu ina go down najiisi niko kwenye saifa niko kwa Mungu ghfla navutwa na Lucifer i need one minutes"-Godzilla
Mkuu sorry unaweza nisaidia audio au video ya ngoma ya hiyo mistari

Au Kama inashindikana hata jina la wimbo nijaribu kuitafuta online

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hhhhh kama umeelewa sawa mkuu,sikuuliza kwa nia mbaya ni mshangao tu ambao ni aghlabu kutokea katika maisha yetu.

Mkuu unanisakama sana na panya kwa nini?

Mkuu hata sili panya mimi japo natoksea huko kusini,sili na sijawahi kula chamaki nchanga.


Kumbe hauli samaki nchanga a.k.a. wale wale, Yondo Sister, Wasenegali, wamikorogo....samahani sana kwa kukushutumu.
 
Ni mbele yake nyuma yetu tujiandae
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zilla baada ya kupigwa chini hakuwa yule yule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu manzi sijui alimpa nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwili wa aliyekuwa rapa maarufu Bongo, Golden Mbunda "Godzilla" umewasili nyumbani kwao Salasala na kupelekwa kanisani kwa ajili ya ibada ambapo baadaye utaagwa na kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni, Dar.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…