Msanii huyu anaitia aibu tasnia ya filamu

Yote mengine ya kwake ila hili la unga letu sote ambao tuna ndugu na jamaa ambao wameathirika na janga hili nakupongeza kwa hilo mleta uzi.
 
Sio bure, interest ya kufamfanyia utafiti mtu ambaye hakuhusu wala so ndugu yako siku kadhaa hadi akawa anafunga safari kwenda kufuatilia. Wewe Jesca unaona in kawaida? Kuna kitu nyuma ya pazia

Hivi wee jamaa unajua maana ya celeb?! Yani mtu akisha amua kuishi kistaa unafuatiliwa maisha yako hadi unapo lala! Na mleta thread kamfichua jamaa ni muuzaji mzuri tu wa madawa kwa maelezo ya mleta thread! Sasa wew unataka ayafanye siri! huenda ukawa unajua maovu mengi huko kitaa kwako ila unayafumbia macho mwisho wa siku likitokea balaa unakuja kujutia ningejua!!
 
Halafu mleta thread hajasimuliwa kaenda mwenyewe kajikita huko kambi hii habari
ina ukweli 75% ni sawa na hisa anazo miliki Manji pale Yanga!

Hivi wee jamaa una ndugu yako alieathirika na madawa kweli?
 
Kuna ujumbe mkubwa sana kwenye hii habari:

Hivi watu wa pwani wana matatizo yanayo fanana!kuuza rasilimali zao na kufanyia starehe! Ni rahisi kukuta wanafamilia wanauza nyumba ya urithi, wanagawana pesa. Na wao kwenda kupanga kwenye nyumba za wengine!!!Angalia maisha ya wasanii wa pwani na wengine wa huko bara, ni tofauti kabisa.Ni hii hii akili ya starehe starehe ndio iliyowatia umaskini watu wengi.Ukweli ni kwamba uongozi hatutatoa kwa watu wa pwani tena.
 
Sasa wewe baada ya kugundua mchizi anauza crack kwanini hukumreport police au umeridhishwa na anavyowapoteza vijana wenzio
 
fuata maisha yako kaka, kwani asipokuwa na kijiko si maisha yake , wewe yanakuhusu nn??

Watanzania jitaidini kufata ya kwenu yasiyo wahusu yapotezeeni
Sasa kama wewe ni mfata yako umeingia jf kutafuta nini kwan kuna mstari hata mmoja wa coding uiouandika katika hii app.....na kwanini usome huu .....tuoneshe mfano kwanza kwa wewe kufataa yako
 
"mtu mbeya huwa anasema kweli ila tu husema sehemu zisizostahili" mwanaume kumsengenya mwanaume mwenzake ni dalili za uoga na UKAOGE
Na haswa pale anaposhindwa kumfuata mwenyewe na kumwambia ukweli na badala yake anamsema kwenye mitandao.

Sijui ni uoga au?
 
hii ni zaidi ya ubongo muvi wake,kuna kitu kati yako na yeye nyuma ya pazia hatukijui.....!!
 
Hapana huyu jamaa kasema wazi wazi bila kuficha, kuna ukweli hapa tena 90℅.
Sina shaka na habari yake, linalonipa shaka in muda wa kwenda kumfatilia huyo mtu maisha yake A-Z. Hajaniconvice kuwa hakuna kitu kati yake na mhusika. Ndio maana nasema wewe unamwamini? Kwasababu kama predictions zangu ziko sahihi katika moja ya habari alizoleta lazima chumvi iwepo, ukitaka kujua ni jamaa anavyokuwa mkali kwenye comment za wale wanaohoji,.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…