Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mnatazama kwenye TV wanamiliki magari ya kifahari, Nyumba za kifahari, nguo za bei Kali. Mkuu hayo sio maisha yao wanaigiza, ukija kwenye maisha halisi utawashangaa hamna kitu.Mpe pole aise duu!!!!. Huku mkoani tunawaona wakubwa kweli kweli mjini huko
Mkuu sijui habari yako inaukweli kiasi gani,lakini kwenye hilo la sembe usingelisema hapa,kama kweli ulitaka jamii ifahamu basi tungefahamu tu kwa yeye kuwa chini ya ulinzi wa polisi. Lakini hivo ulivyofanya ni kama umemuambia aanze kukimbia jambo litakalofanya kumpata kuwa kugumu.Mnatazama kwenye TV wanamiliki magari ya kifahari, Nyumba za kifahari, nguo za bei Kali. Mkuu hayo sio maisha yao wanaigiza, ukija kwenye maisha halisi utawashangaa hamna kitu.
Mkuu kwa jinsi jamaa anavyotoka povu atakuwa ndio muhusika..au bongo movie memberHuyu mbona kaenda mbali sana kaguswa? Kazi ipo.
Ohiii unabwia eeehHivi kibongo bongo ngada bei ya rejareja ikoje. Mfano gram 1 ni sawa na shilingi ngapi? Au vile vipinchi vya kwenye nailoni zamani sana ilikuwa kimoja buku, siku hizi ni bei gani?
Kova amepata wapi pesa za kuwa na kiwanda cha matofari Dar es salaam?si Kabla hujafika kiwanda cha Kova cha matofali? basi ntamuulizia leo nipige nae picha niwatumie au ntamuonesha huu ujumbe hapa ha ha ha.
Duh we jamaa mmbea aisee
Hahahaha atakuwa mwandishi wa Global kwenye timu ya Fichua maovu, ndio wanaweza kazi hiziDuh we jamaa mmbea aisee
fanya maisha yako bro mmekutana ukubwani kila mtu na malezi aliyokuwa nayoNdugu zangu nayasema haya si kwa chuki au unafki , ila wakati mwingine inabidi tuseme kama funzo kwa jamii yetu inayotuzunguka. Na si vyema kujadili maisha ya mtu lakini huyu ninayemjadili ni msanii tena ana jina kubwa tu, hawa ndio tunawaita kioo cha jamii hivyo wanapokwenda tofauti lazima tuseme.
Wapo wengi tu wenye tabia hii ambao huishi maisha yasiyo yao. Kwa sababu tu wanaitwa wasanii na wanajulikana kwenye jamii. Huyu msanii ni wa Bongo movie anaitwa Jumanne Mshindo. Ni msanii wa muda mrefu wengi mmnafaham wale wapenzi wa filamu za bongo. Ukimuona ni mtanashati kweli na Mungu kamjalia umbo lenye Pesa.
View attachment 388623
Katika tembea tembea yangu siku ya wikiendi, nikafika sehemu moja inaitwa Chamazi kwa rafiki yangu, kanunua huko kakibanda kake safi anakaa na familia yake. Wakati tunaendelea kupiga stori hapo nje maana nyumba yake haina fensi. Gafla nikamuona jamaa mnene anatokea kwenye nyumba ya pili yake nayo haina fensi ila ni ya zamani. Nikawa kama nimemfananisha, ikabidi niulize mwenyeji wangu, vipi huyo jamaa aliyepita hapo anafanana na msanii mmoja maarufu wa filamu. Jamaa akacheka, kisha akasema ni kweli wala ujamfananisha, Anaitwa Jumanne Mshindo na hapo ni kwao.
Nikamtania kumbe unaishi na wazazi wa msanii mkubwa hapa kwako, kilichonishangaza akaniambia sio naishi na wazazi wake pekee ata mwenyewe anaishi hapo, na nilipoaamia hapa toka mwezi 10 mwaka Jana nilimkuta hapa, anaishi maisha ya shida sana. Na hii Nyumba ninayoishi kaka yake ndiye aliyemuuzia aliyeniuzia Mimi baada ya kuikarabati. Baada ya kaka yake kuuza hii nyumba alivutia unga yote nae anaishi hapo kwao. Na ili eneo lote lenye majengo lilikuwa lao waliuza viwanja vyote wamebaki na nyumba hiyo moja ambayo haina hata nafasi ya watoto kucheza.
Sikuridhiki na maneno ya jamaa ikabidi mwenyewe niende Chamazi kwa wakati wangu kufanya utafiti. Kilichonishangaza zaidi baada ya utafiti kumbe ndiye muuza unga, kwa wale mateja wa Chamazi. Anashinda kwenye jumba bovu hapo jirani na mateja humzunguka kwa ajili ya huduma. Na anaishi hapo kwao kwa kipindi kirefu yeye na mke wake chumba kimoja, vyombo vyote kauza kabakiza kitanda tu. Nikaingia ndani kabisa kuhusu historia ya hapo nyuma ya familia yao. Baba yao alikuwa na uwezo mkubwa tu, baada ya kufariki, wakauza Nyumba pale mtoni, mashamba, viwanja n.k ikabaki Nyumba 1 iliyoko Chamazi ambayo mama yao anaishi sasa. Pesa nyingi wakagawana vijana wakala maisha.
Kilichosababisha niandike haya ni baada ya kubaini mama yao anateseka sana licha ya mtoto wake ana jina kubwa kwenye jamii na kwenye mitandao wanatupia vitu na maisha ya maigizo, ukiingia kwenye ukurasa wake Facebook unakuta kapiga picha suti kali, gari na funguo mkononi . Kumbe maigizo matupu. Walipouza Nyumba na viwanja vya uridhi yeye alikimbia kuwekeza kwenye movie, alinunua gari Kali, alipanga Nyumba nzima na furniture za kila aina, nguo za bei Kali, akawa anakesha bar kwamba aonekane ni staa mwenye Pesa. Bila kukumbuka kujenga, Pesa zilipoisha karudi kwao kumuangaisha mama yao na soko la movie halilipi kabisa. Hapo kwao ni familia kubwa sana, Nyumba ya vyumba 4, yeye anaishi chumba kimoja na mke, kaka yake nae mvuta unga chumba kimoja, kuna mdogo wake wa kike, bado wajukuu wa kike na wakiume na mama yao humohumo. Jamani hata Pesa ya kupanga chumba kimoja inakosekana unabaki kupishana na mama yako kwenye bafu moja? Kweli haya ndio maisha ya mtu mzima.
View attachment 388649
Wasanii badilikeni jaribuni kuishi maisha yenu halisi, kama huna sema sina, sio kudanganya watu kwenye mitandao mna maisha bora kumbe hakuna chochote, mnashindia mihogo. Fanyeni kazi zingine kama bongo movie haiwalipi, kuna mashamba kibao mkalime.
Poa mkuu, maana ili ni jiwe la gizani limewapata wengi, badilikeni maisha ya maigizo acheni.fanya maisha yako bro mmekutana ukubwani kila mtu na malezi aliyokuwa nayo
Rafiki kama na wewe unaishi maisha ya kuigiza acha, fanya kazi usaidie wazazi wako. Nimeitoa kama fundisho kwa nyinyi wasanii, hamjielewi umaharufu unawachanganya sana.Jamaa mmbea kuliko Shigongo, eti kamfuatilia mpaka Chamazi kujionea mwenyewe hali halisi. Halafu hizi tabia za usinitch hizi.
Hahahaha mkuu na wewe ni walewale bado unabanana na mama yako kwenye chumba kimoja. Pole sanaDuh we jamaa mmbea aisee
Polisi wetu hawa mkuu si wote baadhi, wanashiriki na hawa wauzaji, wakati nikiwa katika uchunguzi nikabaini kuna polisi wanapita wanapewa 5000 wanasepa, biashara inaendelea. Nilienda kwa mjumbe kuuliza kama anafaham biashara ya sembe kwenye mtaa wake, majibu yake tu nikabaini ni mshiriki. Nilikosa ushirikiano na viongozi wa serikali za mitaa, ningemchukua mzogamzoga. Ila bado naendelea kuweka mitego mtasikia tu.Mkuu sijui habari yako inaukweli kiasi gani,lakini kwenye hilo la sembe usingelisema hapa,kama kweli ulitaka jamii ifahamu basi tungefahamu tu kwa yeye kuwa chini ya ulinzi wa polisi. Lakini hivo ulivyofanya ni kama umemuambia aanze kukimbia jambo litakalofanya kumpata kuwa kugumu.
unataka awe nacho nangurukuru?Kova amepata wapi pesa za kuwa na kiwanda cha matofari Dar es salaam?
Huu sio ubuyu ni habari tena serious ikihusu maisha ya vijana kuteketea na madawa.hahahah we jamaa kwa kupenda ubuyu. so ukaamua kwenda na chamazi kabisa aisee
Hiyo picha hapo ndo wewe? Mwanaume wa kweli...Polisi wetu hawa mkuu si wote baadhi, wanashiriki na hawa wauzaji, wakati nikiwa katika uchunguzi nikabaini kuna polisi wanapita wanapewa 5000 wanasepa, biashara inaendelea. Nilienda kwa mjumbe kuuliza kama anafaham biashara ya sembe kwenye mtaa wake, majibu yake tu nikabaini ni mshiriki. Nilikosa ushirikiano na viongozi wa serikali za mitaa, ningemchukua mzogamzoga. Ila bado naendelea kuweka mitego mtasikia tu.
Hizi kazi zetu, kwenye sembe sina huruma na mtu, pale Mwenge na Mwananyamala masela wananijua mziki wangu wakiniona wanasepa kwenye vijiwe vyao.