Msanii Kali P hataki tena kusikia muziki

sady kimwana

Member
Joined
Feb 6, 2024
Posts
28
Reaction score
114

Msanii aliyetamba na ngoma ya Imekaa vibaya na Tumbo joto , Abdul Miraj maarufu kama Kali P amesema hataki tena kusikia masuala ya Muziki .

Kali P amesema ameamua Kumrudia Muumba wake na sasa hive ana takribani miaka 12 ameingia katika dini na ameachana na maswala ya Muziki.

"katika dini yetu ya Uislamu muziki ni haramu ndio maana mimi nikajitoa kwa sababu ya kumuogopa Mungu, Kama Ujumbe kuna njia watu kuwafikishia ila sio Mziki, siku ambayo niliacha mziki nafsi yangu ilisema sipendi tena Mziki. Kipindi nafanya Muziki nilikuwa na miaka 22, nyimbo zangu zikipigwa najisikia vibaya sana na sina habari nazo tena, atakayeimba atakuwa anajichochea moto mwenyewe" Alisema Kali P

kali P kwa sasa anafahamika kama Sheikh Abdul Miraj na anapatikana maeneo ya Kitunda.
 
Muziki wa zamani haukuwa na hela ndio maana wanauchukia.

Internet na Digital platforms ndio zimeleta utajiri kwenye muziki. Leo hii ray vanny anapewa ubalozi wa tembo card crdb na kukunja milioni 500. Anaanzia wapi kuuchukia mziki.

Huwezi msikia alikiba aseme anauchukia mziki.. huku ameimba toka enzi za kina Kali P wanaimba
 
Kale kasauti " Bora nirudi kijijini"
 
Kutoka kimziki ni swala la msimu.....kipindi cha Kina Kali P walipiga mziki mzuri sana lakini nyakati hazikuwapa fursa ya kukunja mamilioni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…