Mhaya gani mwenye roho mbaya kama za watu wa kaskazini?
Roho mbaya haina kabila, dini wala chama cha siasa. Na ubaya hauna kwao wala hauna Kabila! Wajua historia ya Wasamaria? Wengi wakisikia "Msamaria Mwema" hudhani Wasamaria ni watu wa huruma, matendo mema na ya haki. La hasha! Ni yule mmoja tu aliyemwonea huruma mtu aliyemkuta njiani akiwa ameshambuliwa na majambazi; wamemwibia kila kitu alichokuwa nacho, wamempiga wakamwacha karibu ya kufa. Yeye alipomkuta, alimwonea huruma, akamwendea akasafisha majeraha yake kwa divai na mafuta, akayafunga. Kisha akamweka kwenye punda wake akaenda naye mpaka nyumba ya wageni ambapo alimtunza. Kesho yake, yule Msamaria alipokuwa anaondoka, akampa mwenye nyumba ya wageni fedha akamwomba amtunze yule mgonjwa na akaahidi kulipa gharama yo yote ya ziada atakaporudi.
Ikumbukwe kwamba Kuhani mmoja naye alipita njia ile. Alipomwona huyo mtu, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo. Vivyo hivyo Mlawi mmoja naye alipopita, alimwona, akapita upande mwingine wa barabara akamwacha hapo hapo.
Ajabu ni kwamba Makuhani na Walawi ni miongoni mwa watu waliokuwa wanahesabiwa haki na jamii ilihali Wasamaria lilikuwa kabila lililohesabika la wakorofi, wadhurumaji, wanyanganyi, wauaji, na kila baya lilihesabika kuwa upande wao. Huyu mmoja tu aliyemfanyia huruma mateka ndiye aliye BRAND upya kabila hili. Leo hii ukisema fulani "Msamaria Mwema", linaloingia vichwani mwa watu moja kwa moja ni kuwa fulani ni "Mtu wa Huruma!"
Muonekano wa mtu yeyote akiwemo Ruge kwenye jamii, haupaswi kuhusishwa na asili yake ya kuzaliwa. Isitoshe Ruge anaweza kuwa anaujua na kuuishi vema utamaduni na mila za Marekani na za Dar zaidi kuliko za Wahaya!