TANZIA Msanii maarufu Bi Hindu amefariki Dunia leo Julai 9, 2022

TANZIA Msanii maarufu Bi Hindu amefariki Dunia leo Julai 9, 2022

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2020
Posts
3,585
Reaction score
8,106
Taarifa za huzuni kubwa

Msanii mkongwe Nchini Tanzania, Chuma Suleiman almaarufu Bi Hindu ametutoka leo Jumamosi Julai 9, 2022 akiwa Magomeni nyumbani kwake.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mjukuu wake huku sababu ya kifo chake ikitajwa kuwa ni maradhi ya muda mrefu.

Bi Hindu ni mmoja wa waasisi wa Kaole Sanaa, kundi ambalo lilipata umaarufu mkubwa mwanzoni mwa miaka ya 2000, pia ni mdau mkubwa wa Klabu ya Simba, aliwahi kuonekana mara kadhaa katika matukio yaliyohusu klabu hiyo.

Aidha, amewahi kuwa mmoja wa watangazaji wa Kituo cha E-FM Radio cha Jijini Dar es Salaam.
70BCAE5D-E41B-4346-80CC-DC86C07B3C51.jpeg
FB_IMG_16573528903359602.jpg
 
Bi Hindu mmoja kati ya wasanii waliojizolea umaarufu katika michezo ya kuigiza miaka ile Kaole Sanaa Group inatamba.

Baadae akaibukia kwenye vipindi vya redio kama msemaji na mkosoaji wa tabia mbovi za wanawake wenzake (mchambaji)

Vilevile, alikuwa ni mwanachama shupavu wa Simba hasa tawi la Mpira Pesa na kutokana na ushupavu wake wa kuhoji hadi viongozi wa juu wa timu yake walikuwa wakimuogopa (Rejea enzi ya utawala wa Aden Rage Simba alikuwa akimzuia kuingia kwenye vikao)

Ameacha alama kubwa sana kila alikopita...pumzika kwa amani Iron Lady Bi Hindu. Ama kweli nyakati ngumu hazipiti ila watu wagumu hupita.
 
RIP kungwi, ulale salamaaa
[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Back
Top Bottom