Msanii Madee Ali,azuia nyimbo zake alizoshoot South Africa zisipigwe kwenye TV na Radio station,azifuta kwenye channel yake youtube

Madimba jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2017
Posts
1,577
Reaction score
3,146
Mambo vipi naitwa MadeeAlly leo Sept 06 2019 kwa hiari yangu nimeamua kuzuia kuchezwa kwa nyimbo zangu ambazo nimezifanya kwenye ardhi ya South Africa especially #VUVULA na zingine zisipigwe kwenye kituo chochote cha habari na zaidi ikiwa ni ni TV, Kwa sababu TV ndio kitu kinachoonyesha mandhari ya nchi tajwa ambayo ni SA, Binafsi nimechukua hatua kwanza kwa kuufuta hata kwenye channel yangu ya Youtube ambako ulikua unapatikana.
.
.
.
Binafsi wakati natoka Manzese kwenda kushoot SA plan ilikua nikutangaza vivutio vya Africa kwa ujumla, Kwa kuwa imani inaniambia sisi Waafrika ni Wamoja.
.
.
Nimefikia hatua hii kwa sababu kuu mbili.. (1)kile kinachoendelea kwasasa kila mtu anajua namna Wasouth Africa wanachowafanyia Waafrika wenzetu, 2) Ni kumuenzi Mzee wetu MUGABE ambae wengi wetu humu tunajua historia yake ya kupambania mtu mweusi (Mwafrika)na miongoni mwa watu waliokua wakipinga utawala wa watu weupe alikua anapambana kuhakikisha Waafrika tunajikomboa.
.
.
Sitakua sawa kuendelea kuitangaza SA kupitia muziki wangu, ZIMA KWAITO 🎤❎ R.I.P ROBY
 
Huku nikutafuta Kiki sasa wewe hata ukufuta hizo ngoma zako huna impact yoyote uko south Africa kwenyewe hufahamiki
We jamaa unaongea ujinga, fikiria wasanii wote wa Afrika wangekuja na mawazo kama ya Madee na wanamichezo unadhani isingekuwa na Impact? Sisi wa Afrika wkt tunakuwa na mawazo ya kipuuzi, ingekuwa Ulaya na USA ndio huo ujinga unafanyika unadhani ingekuwa kimya kwa watu maarufu kama ilivyo huku kwetu
 
Huku nikutafuta Kiki sasa wewe hata ukifuta hizo ngoma zako huna impact yoyote uko south Africa kwenyewe hufahamiki
hujui anachofanya madee, emu watanzania tuache hayo mawazo eti kila kitu ni kiki, anafanya hivo kama harakati ili na wasanii wenzie wafanye wa africa nzima na waitenge south,ukiona video za jamaa wanavouliwa huko south ndo utaelewa
 
hujui anachofanya madee, emu watanzania tuache hayo mawazo eti kila kitu ni kiki, anafanya hivo kama harakati ili na wasanii wenzie wafanye wa africa nzima na waitenge south,ukiona video za jamaa wanavouliwa huko south ndo utaelewa
Kuna watu wajinga sana yaan hawajua alichokifanya madee inatakiwa kifanywa na wanamziki wt Afrika? Au mnaona watu kuuliwa namna ile ni sawa wkt watu wao wapo kila Nchi? Wanataka mpk bwana wao diamond afanye kama madee ndio wasapoti
 
Kuna watu wajinga sana yaan hawajua alichokifanya madee inatakiwa kifanywa na wanamziki wt Afrika? Au mnaona watu kuuliwa namna ile ni sawa wkt watu wao wapo kila Nchi? Wanataka mpk bwana wao diamond afanye kama madee ndio wasapoti
mkuu, nimemshangaa sana jamaa,bongo ukifanya la maana unasemwa, ukifanya upuuzi unapongezwa
 
Tatizo hafahamiki hata hizo harakati zake hazita msaidia angefanya diamond ndo ingeleta attention huko south Africa cos ni msanii mkubwa lakini pia anapendwa na watu lakini madee Nani anamfahamu uko south? Kama sio Kiki ni nini?Hii ndio hoja yangu sio kwamba alichokifanya ni kibaya hapana tatizo lake Hana influence yoyote
 

Madee?

And who the fvck is he?

He aint no musician!

He’s a jumping old man in some Tiptop music videos!

Pretty much!
 
Angalau angefanya diamond ingemake sense huyu madee hata south Africa kwenyewe hafahamiki kiufupi Hana impact yoyote naona lengo lake ni kutafuta Kiki Hana lolote.
Wew jamaa kuna time nahis ushabiki wako mpaka umepelekea kuwa na kiwango kidogo cha akili,Yan kila afanyacho Diamond na crew yake ndo unaona ni bora,Madee kufanya hiv siyo kwamba ni msanii mkubwa ila kafanya hv ili awe kama daraja la wasanii wako hao wakubwa wenye impact huko SA waweze kuiga ili angalau kupunguza machafuko hayo,Pata picha endapo Mond,kiba,vanessa n,k wakiiga alicho fanya Madee itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…