Msanii Madee unatuumiza na kututia hasira mno sisi Hustlers

Msanii Madee unatuumiza na kututia hasira mno sisi Hustlers

Hivi Inaingia Akilini Kwenu Mtu Ambaye Anajua Fika Kuwa 90% Ya Watanzania Ni MASIKINI Wa KUTUKUKA Ambao Kila Siku Tunahangaika Kuutafuta Mkate Na Sometimes Tunalala Tu " Kavu Kavu " Na Kupiga " Miayo " Huku Tukikodolea Mikenchi Tu Majumbani Kwetu Halafu Msanii Mmoja Wa Bongo Fleva Madee Anakuambia Kuwa Endapo Timu Yake Ya Arsenal FC Leo Itafungwa Na Chelsea FC Ktk LONDON DERBY Basi Atachoma Moto Moja Ya Gari Lake La Kifahari. Na Ikumbukwe Kuwa Madee Hana " CHOMBO CHA USAFIRI " Nikimaanisha Zile Gari Zenye Thamani Ya Kati Ya Tsh Milioni 3 Hadi Tsha Milioni 15 Ambazo WATANZANIA Wengi MNAZO Bali Madee Ana " MAGARI " Nikimaanisha Kuwa Magari Yake Mengi Yanaanzia Tsh Milioni 50 Hadi Tsh Milioni 120.


Naomba Kuuliza Je Hii " Nadhiri " Aliyoiweka Madee Ya Kuchoma Moto Moja Ya GARI Zake Siyo Ni TUSI LILILOTUKUKA Kwa Sisi " MANGUMBARU? " a.k.a Masikini? Kweli Kuna Watu Wana NYODO, KASHFA Na MATUSI Ya Reja Reja Hapa Duniani. Kwanini Tu Asingeliweka Kama BAHATI Nasibu Hilo Gari Lake Ili Akina Siye TUPAMBANE Kuligombania Na Tulipate Kwani Kusema Ukweli TUMESHACHOKA SASA KUOTA VIGIMBI VYA KUKIMBILIA MADALADALA, KUPIGWA NDOLE NA KUIBIWA Huku TUKIJAMBIWA KILA MARA NDANI YA VYOMBO VYA USAFIRI Kiasi Kwamba Ikifika Iwe Kazini au Nyumbani Unanuka SHOMBO Tu.


Tafadhali Kwa Aliye Karibu Na Msanii MADEE Naomba Amwambie Asilichome Moto Hilo GARI Lake Na Kama Vipi Alitafutie Tu UTARATIBU Sisi MANGUMBARU Tulipate Na Tutamshukuru Mno.
Ndugu una haki ya kulalamika sana maana hizo zinazochomwa moto ni pesa walizopiga katika kampeni za uchaguzi 2015 ndani ya CCM. Jamaa walipiga mpunga mrefu sana wacha ziwachanganye akili
 

Attachments

  • 1453694678828.jpg
    1453694678828.jpg
    8.4 KB · Views: 40
hizi ndiyo zile hela alizo mdhulumu dogo janja
 
Ndugu una haki ya kulalamika sana maana hizo zinazochomwa moto ni pesa walizopiga katika kampeni za uchaguzi 2015 ndani ya CCM. Jamaa walipiga mpunga mrefu sana wacha ziwachanganye akili
Wakati wao wameambulia ubwabwa tshirt na kapelo. kweli hapo lazima roho imuume
 
Angeahidi kutoa mtandao pendwa ningemuona wa maana
 
Back
Top Bottom