ukwaju_wa_ kitambo
Senior Member
- Sep 15, 2024
- 150
- 173
wachache sana wanaomjua msanii huyu aliyefahamika kwa jina lake Richard Mangoustino .
Enzi hizo msanii huyu Richard mangoustino alikuwa ni Mwalimu wa muziki katika nyumba ya kukuzia vipaji hapa nchini nya THT .
Mangustino amekuwa mwanamuziki kwa takriban miaka mingi imepita sasa uwezo wake ni mkubwa sana kimuziki.
Mangoustino amewatoa wasanii kibao ambao wanafanya vizuri sana katika gemu akiwepo Hafsa Kazinja, Mwasiti, Bui bui, Vumi na wengineo kibao.
Lengo lake hasa Enzi alitapenda / kutaka kuhakikisha analeta mabadiliko makubwa sana kwa wasanii ambao aliwafundisha kwani alikuwa ana amini hao ndio watakaoshilika jahazi la muziki hapa nchini lakini yote tisa, kumi ali taka kuwa na pesa kwanza kwani raha ya muziki upate pesa.
Mangoustino ambaye ni msanii kutoka Congo DRc enzi hizo ikijiita zaire mwenye afadhali kwenye upande wa lafudhi.
Baadhi ya kazi alizowahi kutamba enzi hizo alizoshiriki msanii huyu kutoka Drc Congo ni.
1. O Ten ft. Mangoustino - Mimi
2. Waswahili asili ft. Mangoustino - pengo
3. Mwana Fa ft imam Abbas, jose mtambo & mangoustino - wakati umelala
4. Rich one ft. Juma nature & Mangoustino - hatuna kitu ( intro)
5. Mwana Fa ft. Shakii & mangoustino - tuliza ball ( back vocal)
Na nyingine nyingi..
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202
( katika picha ya kwanza ndio muonekano wa msanii Mangoustino wake wa sasa na picha ya pili ni muonekano wa msanii mangoustino katika video ya wimbo wa " waswahili asili" unaitwa pengo: )
Moja kati ya hit song zinazoishi milele kutokana na ushairi ama Tungo zilizopatikana katika wimbo huu..