Msanii Matonya na utajiri wa kutisha

Msanii Matonya na utajiri wa kutisha

Jamani mi naona a modest house na Toyota brevis....sasa huo UTAJIRI was kutisha uko wapi?

Ndio maana mwanzo nikatoa angalizo la bei ya viwanja vya bahari beach,viwanja vya kule vingi ni eka moja na bei ya kiwanja tupu ni 800m,kuna kingine kinauzwa sqm 2400 ni 350m,kwa nusu eka tena kina nyumba ni zaidi ya 500m? Pili ana yard ya magari nao si utajiri kaka?
 
Aaah ok basi kumbe na yeye ni bilionea...manake nyumba mil 500 ukijumlisha na yard hio balaa!
 
Huyu huyu matonya?

Halafu anajitahidi kujifanyia promo baada ya watu kumbaini kachoka hata hela ya kula hana. Huyo jamaa kachoka mbaya ana kijumba uchwara pale tanga. Akija mjini anahifadhiwa na jamaa yake pale faya. Sijui kwanini anadanganya watu
 
Mie nimebaki kinywa wazi na labda!
 
Nina mashaka sana na hii habari! Matonya nimekutana nae juzi, juzi kushinda jana calabash mwenge analazimisha kuomba kiroba, alinisumbua hadi nikampaka maana simjui hanijui kanivamia tu leo mseme anamiliki nyumba bahari beach! ! Kweli jamani? Anyway labda inawezekana
 
Dah nilidhani Matonya yule omba omba,,anyway big up
 
Halafu anajitahidi kujifanyia promo baada ya watu kumbaini kachoka hata hela ya kula hana. Huyo jamaa kachoka mbaya ana kijumba uchwara pale tanga. Akija mjini anahifadhiwa na jamaa yake pale faya. Sijui kwanini anadanganya watu

mkuu umenena vema,huyu jamaa n muong hatare juz kat hap dsm kaja maskani hata hela ya bajaj hana tukamuungia kisela
na dsm tonya hana nyumba anahifadhiwa na mchiz getto leo anakuja na mboyoyo nying kweny media et ana nyumba
shame on u
 
Hivi huyu si alidakwa na sembe china akiwa na mwana mfalme

Ikabidi mfalme apande pipa kwenda kuwaokoa

Bei yake ikawa ni mkataba wa gesi ya Mtwara na Bandari ya Bagamoyo

Mie mwenyewe niliskiaga alidakwa na sembe china akiwa na Rizmoja.mshua alienda kunegotiate yaishe kimya kimya ndio vile meli ya samaki wa magufuli ikaamuriwa wafungwa waachiwe huru na walipwe meli yao kwa thamani ya rizmoja na huyu jamaa sasa sijui lipi la ukweli.ila kuhusu ngada ni kweli alibebaga then ndio after kukamatwa ndio akachenj biashara.
Hivi mtoto wa Rais ana shida abebe dawa za kulevya wakati kuna wapambe kibao tu wangeweza kumbebea wakati mwenyewe akiendelea kunywa juice Ikulu? Yaani mnaamini hadithi za kutunga za Yerricko Nyerere na ID ya Jason Bourne ambayo zamani watu walikuwa wakiamuamini hadi alipokuja kuumbuliwa na moderator wa JF!!!
 
Bado hatuwezi kusema ni utajiri wa kutisha pls
 
Hivi mtoto wa Rais ana shida abebe dawa za kulevya wakati kuna wapambe kibao tu wangeweza kumbebea wakati mwenyewe akiendelea kunywa juice Ikulu? Yaani mnaamini hadithi za kutunga za Yerricko Nyerere na ID ya Jason Bourne ambayo zamani watu walikuwa wakiamuamini hadi alipokuja kuumbuliwa na moderator wa JF!!!

Shauri yako...nchi hii ni zaidi ya uijuavyo
 
Shauri yako...nchi hii ni zaidi ya uijuavyo
Hoja yangu sio kwamba mtoto wa Rais au hata Rais mwenyewe hawezi kuwa drug dealer, hoja yangu ni kwamba, mtoto wa wa Rais hana shida ya kubeba drugs mwenyewe wakati kuna wapambe kibao wanaoweza kumbebea huku mwenyewe akiwa mbali kabisa! Simulizi ya Yerricko Nyerere ilikuwa ni kwamba Rizmoko alibeba mzigo mwenyewe... ndo nakueleza hana shida hiyo (ya kubeba mwenyewe) coz' kuna watu kibao wanaoweza kumbebea!
 
Huo ni uzushi Wa mjini Wa walio feli wewe ni mmoja wao
 
Hoja yangu sio kwamba mtoto wa Rais au hata Rais mwenyewe hawezi kuwa drug dealer, hoja yangu ni kwamba, mtoto wa wa Rais hana shida ya kubeba drugs mwenyewe wakati kuna wapambe kibao wanaoweza kumbebea huku mwenyewe akiwa mbali kabisa! Simulizi ya Yerricko Nyerere ilikuwa ni kwamba Rizmoko alibeba mzigo mwenyewe... ndo nakueleza hana shida hiyo (ya kubeba mwenyewe) coz' kuna watu kibao wanaoweza kumbebea!

Hilo la shida wala usilisemee....kwa sababu drug dealers hawana shida kaa zako na zangu

Kuhusu Mwana mfalme kubeba au kutokubeba is non issue....The issue ni kwamba walikua pamoja na huyu Tonya.

Mkuu...Usiwe Tomaso sana...Unajua Mzigo wa masogange ulikuwa wa nani?
 
wakaenda lukuvi na nzoa kuhakikisha anapata haki zake wakati watanzania kibao wamekamatwa kenya brazil china n.k wala hawana time nao
 
Hilo la shida wala usilisemee....kwa sababu drug dealers hawana shida kaa zako na zangu

Kuhusu Mwana mfalme kubeba au kutokubeba is non issue....The issue ni kwamba walikua pamoja na huyu Tonya.

Mkuu...Usiwe Tomaso sana...Unajua Mzigo wa masogange ulikuwa wa nani?
Tatizo source yako ni Jason Bourne a.k.a Yericko Nyerere ambae ndie alileta hiyo simulizi ya JK na kumwokoa Rizmoko baada ya kubambwa huko China! Simulizi yenyewe inayotumika kama source, ina mapungufu!! Labda nikukumbushane machache, kwanza simulizi ile ilimtaja mtu aliyekamatwa pamoja na Rizmoko ni Abdalah Aman Mohamed... for what I know, Matonya anaitwa Seif!!! Sasa tuendelee na sehemu ya ile simulizi:
Mnamo tarehe 2/7/2012 majira ya saa nne (4:13) za usiku hapa Tanzania, rais Jakaya Kikwete alipokea simu kutoka kwa mtanzania mmoja aitwae Philip Malmo ambae ni balozi wa Tanzania nchini China, Taarifa muhimu baada ya salamu ilikuwa ni Ridhiwani amekamatwa uwanja wa ndege wa Hong Kong na madawa ya KULEVYA,
Gari ya kirai namba T 435 CDR aina ya Landcruiser nyeusi iliingia nakuwabeba watu watatu akiwemo rais Jakaya kuelekea airport, kama dakika 13 ikafika airport, tayari ndege ilishaandaliwa na palikuwa na maafisa watatu, wote tuliingia katika ndege ile isipokuwa yule dereva wa gari ambae aligeza mjini, hiyo ilikwa sasa ni saa 7:43 za usiku.
Haya tuitafakari hiyo habari! JK ameletewa taarifa ya kukamatwa Riz1 saa 4.13 usiku cku ya tarehe 02/07/2012! Baada ya maandaliziya hapa na pale, hadi saa 7:43 usiku (03/07/2012) tayari walikuwa kwenye ndege ready for take off! Bila shaka, kwa safari muhimu kama hiyo, hawakuwa na sababu ya kusubiri subiri tena, kwahiyo let's say waliruka saa 8 usiku (dakika 15 baadae... tarehe 03/07/)! Saa 8 Tanzania ni saa 1 asubuhi China 03/07/2012!

Simulizi inaendelea:
Tarehe 3, majira ya saa nane za usiku kwa china, tulifika China, hakukuwa na aina ya mapokezi yoyote ya kiserikali
Hapa ni kwamba, walitoka Tanzania tarehe 03/07/12 saa 1 kwa saa za China halafu tena anasema walifika China tarehe 3, saa nane usiku!!!! Je, tarehe 03/07/2012 saa 8 usiku kwa China, Tanzania inakuwa saa ngapi? Kumbuka, China wapo saa 5 mbele yetu... which means kwa Tanzania ilikuwa tarehe 02/07/2012 saa 3 usiku!!!! Sasa ikiwa JK alipigiwa simu tarehe 02/07/2012 saa 4:13 usiku na tayari wakafika China 02/07/2012 saa 3 usiku kwa saa za Tanzania, tuite nini hii??!! Enzi hizo saa zilikuwa zinaenda kinyume nyume, au? Anyway, nisikuze mambo, ngoja tuendelee! JK na Timu yake walitoka TZ mida ya saa 8 ucku (03/07/2012) ambayo ni saa 1 asubuhi kwa China (03/07/2012) na wakafika China saa 8 ucku (tunaambiwa tarehe 3... au ni tarehe 04?) Tu-assume ilikuwa 04/07/2012! Kwa huo muda, ina maana walitumia zaidi ya saa 15 angani!!!!!! Walipitia wapi wakati waliondoka na ndege ya Rais?!

Tuendelee na simulizi ile:
Tarehe 3, majira ya saa nane za usiku kwa china, tulifika China, hakukuwa na aina ya mapokezi yoyote ya kiserikali, na baada ya kushuka tulimkuta Malmo na msaidizi wake wakitusubiri, Malmo alikuwa tayari ameshaandaa hoteli lakini kulingana na tukio lilivyo tulikubaliana tusilale na tukammwambia mheshimiwa rais amwambie Hu Jintao kuwa ameshafika. Rais alitekeleza hilo na baada ya dakika 15 maafisa watatu wa china walifika nakujitambulisha kuwa wenyeji wetu, wakatuchukua hadi alipo Hu Jintao katika moja ya ikulu ya Hong Kong,
Kutokana na unyeti wa issue yenyewe, vijana wa kazi wakamwambia JK kwamba wasilale na waanze on the spot! Remember, JK na timu yake wamefika saa 8 usiku (let's assume saa 8 kamili) baada ya kupokelewa na issue ya hapa na pale, robo saa baadae wakaja vijana wa kazi wa Rais wa China ambao walitoka na akina JK hadi Ikulu ya President wa China iliyopo Hong Kong!!! Hata kama walikuwa fasta namna gani, basi bila shaka JK alikutana uso kwa uso na Hu Jintao saa 8:30 usiku, tarehe 04/07/2012 kwa saa za China wakati ni saa 3 usiku tarehe 03/07/2012 kwa Tanzania!

Msimulizi wetu anaendelea:
Kikao chao kilichukua masaa manne, na jambo kuu walilokuwa wanakubaliana ni mashariti ya kumuachia, Hu Jintao alihitaji jambo moja tu, kwamba nini serikali ya china itapata kwakumwachia huru Ridhiwani?
Kikao cha JK na Hu Jintao kilichukua saa 4! Remember, JK na timu yake waliingia China saa 8 ucku na ilichukua robo saa vijana wa Hu Jintao kutokea airport kabla hawajaenda kwa Hu Jintao na ndio maana nikasema kuna uwezekano walikutana na Rais wa China saa 8:30! Potelea mbali, let's assume Hu Jintao alikutana na JK alipofika tu airport, yaani saa 8 ingawaje the guy is good katika kurekodi muda, angalia hapa:
Mnamo tarehe 2/7/2012 majira ya saa nne (4:13) za usiku hapa Tanzania
tuliingia katika ndege ile isipokuwa yule dereva wa gari ambae aligeza mjini, hiyo ilikwa sasa ni saa 7:43 za usiku
Ingekuwa mwingine hapo angesema saa nne na robo, saa nane kasorobo! Anyway, maongezi yalichukua saa 4... which means yalienda hadi saa 12 asubuhi (but possibly beyond saa 12 unusu asubuhi)! Msimulizi wa ile hadithi huyu tena:
Majira ya saa 11 alfajiri kwa saa za china, Ridhiwani aliletwa akiwa katika gari dogo, nakupokelewa na jk huku wakikumbatiana wote WAKILIA.
Yaani mazungumzo yameisha saa 12 lakini Rizimoko aliletwa saa 11 !!!!!!! Ina maana aliletwa katikati ya mazungumzo tuliyoambiwa yalichukua saa 4?? Ina maana aliletwa kabla hawajafikia makubaliano? Jamaa huyu tena:
Majira ya saa 12 za asubuhi tukaondoka kurudi Tz.
Kwa mkali wa kurekodi muda kama huyu sitarajii iwe saa 12 na dakikaa kadhaa mbele.... sasa kwa kauli yake hii ya mwisho ni as if JK alipofika tu airport (saa 8 usiku) akaanza mazungumzo hapo hapo yaliyochukua saa 4 hadi saa 12 walipoanza kurudi TZ!!!! Hata hivyo, sio issue, issue ni kwamba, hiyo ilikuwa saa 12 asubuhi huko China siku ya tarehe 04/07/2012 kwa China wakati ni saa 08 usiku tarehe 04/07/2012 nchini Tanzania!!! Tuendelee-- Lakini kwanza jikumbushe
Mnamo tarehe 2/7/2012 majira ya saa nne (4:13) za usiku hapa Tanzania
Lakini kama ulikuwa mfuatiliaji mzuri wa Jason Bourne, nadhani unakumbuka ile series ya safari za JK... Jason Bourne huyu hapa tena:
SAFARI YA 329
Tarehe 2/7/2012

Rais Jakaya baada ya kutoka kuhudhuria sherehe za uhuru nchini Rwanda, ameunganisha kwenda nchini Burundi kuhudhurua sherehe za Uhuru wa nchi hiyo!
Haya tusaidiane, Ina maana baada ya kutoka Rwanda akaenda Burundi na Burundi hakulala, akarudi Tanzania na usiku huo huo akaunganisha China kwenda kumwokoa RizMoko, au? Mimi na wewe hatujui lakini ngoja tuone hii picha: JK.jpgJuu ya hiyo picha inaonsha tarehe 04/07/2012, maelezo ya hiyo picha yanasema: "Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili Uwanja wa ndege wa wa Julius Nyerere jijiniDar es salaam jana jioni wakitokea Burundi na Rwanda walihudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hizo." Sasa ikiwa picha ilikuwa posted 04/07/2012, ina maana jana yake ilikuwa 03/07/2012! Aidha, hiyo habari ilikuwepo hapa JF, hii hapa: https://www.jamiiforums.com/jamii-p...is-kikwete-arejea-toka-rwanda-na-burundi.html . Back to our story! Sasa je, hiyo tarehe 03/07/2012 alikuwa China or East Africa?. Simulizi ya JK kwenda kumuokoa Rizmoko aliziweka hapa: https://jasonbournetz.wordpress.com...nchi-rehani-kumuokoa-mwanae-asinyongwe-china/

Kwenye ile simulizi ya dawa za kulevya, Jason Bourne alidai kwamba:
Taarifa hii ni yakweli mimi nilikuwemo kwenye msafara huo,
Na Kama unakumbuka sawa sawa, majority JF walikuwa wanaamini kwamba Jason Bourne ni kijana wa kazi wa Ikulu!!! Na katika kujionesha yeye ni Kachero Muhimu la Ikulu, alishwahi kuleta habari ambayo moja ya paragraph zake ilikuwa inasema:
Kwamuda wa miaka miwili sasa tangu tulipoanza kazi nzito ya upelelezi wa wakubaini na kuzuia uingizaji na utoroshaji wa pesa nchini,
Juhudi zetu zimeanza kuzaa matunda baada ya kubaini majina halisi ya watanzania walioficha fedha nje ya nchi na wanaoingiza fedha haramu nchini.

Kwakushirikiana na mashirika ya kijasusi ya CIA-USA, M1-6-UK, RAW-India, DGSE-Ufaransa, FSB Urusi, ISI Pakistan, na MSS-China, ambayo yamekuwa yakifuatilia nyendo za fedha haramu hasa za kighaidi dunia, tumefanikiwa kutambua Watanzania, Wakenya, Waafrika kusini, Waganda na Wakongo wengi matajiri walioficha fedha uswisi.
More: https://jasonbournetz.wordpress.com/2012/09/15/hawa-ndio-watanzania-walioficha-fedha-uswisi/
Wadau JF waliendelea kumuamini kwamba ni kachero la Ikulu hadi siku mods walipomuumbua kwa kuunganisha ID zake!! Binafsi sikuwahi kumuamini hata siku moja kv ikiwa suala ni kutunga na kuchambua hadithi hata nami sijambo isipokuwa kwahiyo mtu hawezi kunidanganya kwa hadithi za kutunga!!!
 
Back
Top Bottom