Msanii mkali unatoa nyimbo kali na mtaa unakuelewa, tuzo ya nini?

Msanii mkali unatoa nyimbo kali na mtaa unakuelewa, tuzo ya nini?

blackstone

Senior Member
Joined
Aug 11, 2015
Posts
147
Reaction score
128
Wakuu

Msanii mkali unapiga show pesa inaingia, album unauza na zinauzika pote duniani, tuzo za nini? Sasa ifike wakati serikali iweke mfumo wa album vizuri.
Wasanii washindane kimauzo ya album, ndio mziki utarudi thamani yake.
Shows peke yake haitoshi kujua kama msanii anapendwa sana au hapendwi na watu.

Mtaani hadi huko Mabwepande wakikuelewa hapo umefanikiwa, uswazi ngoma zako zikigongwa na kupendwa na waswazi na ushuani. Ukijiamini na kuipa thamani kazi yako tuzo ya nini sasa. Tuzo za hapa bongo hazina thamani tena na si lazima upate tuzo ndo tujue we mkali.

Piga kazi zitakazobaki kwenye mioyo ya watu. Big up kwa wote wasiopata tuzo ila mtaa unawaelewa.

Over
 
Ktk muziki kipimo kimojawapo kuwa unapendwa na unakubalika kwa kiasi gani basi ni TUZO, labda upinge jinsi ya hao wanaopewa tuzo wanastahili au hawastahili. Na ndio maana kwenye wasifu (CV) za wasanii wengi uwekwa tuzo ngapi na za aina gani anazimiliki.
 
Back
Top Bottom