me naona vituko vyake ndo vinamfanya tumsikie lakini kwa mziki nafikiri ni funguo tu ya kufanyia mambo yao flani..Jamaa katoa boko aisee.
Tena sio msanii mkubwa tu...
Kaongeza na Hip Hop juu!
we una unasema amefungiw huk instagram anapost show aliyopigaHakuna mtanzania asiyejua ya kwamba msanii wa muziki wa bongofleva Emmanuel Elibariki a.k.a Ney wa mitego kafungiwa na BASATA kwamba asijihusishe na muziki kwa muda usiojulikana.
Kwanza niseme tu hongera kwa kufungiwa kwa sababu huyu jamaa alikuwa anakera watu sana kwa nyimbo zake zisizoeleweka mlengo wake ilikuwa ni nini hasa?
Nyimbo nzima kusemasema watu tu,sasa ndio muziki gani huo?.sasa unajua ni kwa nini nakwambia kaumbuka? Ni kwa sababu huu wimbo wake wa mwisho kuutoa unaoitwa pale kati patamu ,ukiusikiliza utaelewa wazi kwamba alikuwa anatafuta KIKI kama aliyopata Snura na wimbo wake wa chura.
Sasa Ney alidhani na yeye ataitwa na media zote kufanya interview lakini kinyume chake hakuna hata chombo cha habari chic hire kilichomwita wala nini,na hata habari yake ya kufungiwa wala haijawa gumzo kabisa kwenye vyombo vya habari kama alivotegemea yeye.
Na hii ni kwa sababu clouds media walipotezea so hata media zingine zikapotezea pia.
Pole sana Ney
We jamaa umedata si bure,wapi nilipofurahia kwamba atapigwa na rumba? Na wapi niliposema nyimbo zake hazina maadili?acha ushabiki wa kishamba mkuuThread umeleta wewe unafurahia Ney kakomolewa, sasa nini cha kusoma vizuri hapo? Eti unafurahia atapigwa na rumba, hizo ni akili za kichawi. Sasa ukimuona anaendelea kuburuza mikoko sijui utajinyonga? Acha majungu kama BASATA, kwa Tanzania hii sijawahi kukutana na mtu anayefuata maadili tangu nizaliwe. Kwere tu.
We jamaa umedata si bure,wapi nilipofurahia kwamba atapigwa na rumba? Na wapi niliposema nyimbo zake hazina maadili?acha ushabiki wa kishamba mkuu
Mkuu hongera kwakuwamwagia upupu hawa watoa mapovu wanaonuka shidaNo reaserch no right to speak!!!! Mkuu unauhakika na uliachoandika????
Mbali na hayo uliyoyasema kumbuka kuwa E FM 93.7 Dar waliwakutanisha Nay wa Mitego na Kiongozi wa Basata na Wakabishana sana kuhusu hizi mambo za kufunguia nyimbo na yule kiongozi wa Basata aliishia kujiuma uma tuuu na utaona kabisa ni chuki bianfsi!!! Alisema sababu kubwa ni cover zilizo tumika na Maudhui lakini Mtangazaji alisemwambia sio lazima wote waelewe kama wewe!!!
Pili NaY alihoji kwanini Media zilizo cheza nyimbo yake kwa Takribani Siku 7 kwanini hazikufungiwa na TCRA hadi basata ndo wamekuja kuona wimbo unamatatizo baada ya siku saba kupita!!! Kumbuka kila radio station kabla ya kucheza nyimbo lazima isikilizwe kabla ya kuipeleka hewani!!
Ukisema hakufanya interview wewe ni Muongo Media nyingi tuu zimemuhoji!!!
Angalia MRISHO MPOTO,AFANDE SELE,PRO J na wengine wamekuwa mstari wa mbele katika kumtetenea katika hilo hao wote ni wajinga? Na ninafikiri ishu imeisha subiri Video Next wiki!!!!!!,tumeshamuona kwenye show ya Mwendokasi Nay akiperform Pale kati Patamu!!!!!
Acheni Chuki binafsi imba wewe Pale kati patamu kama utauzaa Watu wanataka burudani na sio hayo mnayo yasema!! Pigeni burn Video za mbeleeee zote!!! Maana asilimia kubwa hata media zetu zinarusha sana video za mbeleee kwa mda mrefu!!! Huwezi kuleta maadili kwa njia hiyoooo!!!!
Hakujua kua ni kosa? Tatzo msanii mkubwa wa hip hop alaf anaishi kwa kiki..
Jamani muoneeni huruma anafamilia ya watoto wawili na mama yake mzazi anamtegemea