Msanii Ray C azidiwa na Madawa ya Kulevya; asaidiwa na Polisi



Msanii wa muziki Rehema Chalamila aka Ray C usiku wa jana alikamatwa na jeshi la polisi maeneo ya Kinondoni Manyanya almaarufu ‘Kinondoni kwa Mpemba’ jijini Dar es salaam baada ya kupiga makelele barabarani akidai anataka kutekwa.

Muimbaji huyo mahiri ambaye ameathirika na Matumizi ya madawa ya kulevya, alidaiwa kufika katika eneo hilo na kuomba msaada lakini baadae aliomba kisu ili ajichome huku akiongea vitu visivyoeleweka.

Mmoja kati ya mashuhuda wa tukio hilo ambaye ni msanii wa filamu, Esha Buheti kupitia instagram yake aliandika ujumbe huu:

Nashindwa hata niongee nini jamani, rayc Leo kinondoni umenitoa machozi, jamani tufanye kitu tumsaidie rayc, I mean it jamani siku zote nlikua najua anaonewa ila nlichokishuhudia leoo nimeumiaa kutoka moyoni amedhalilika mwanamke mwenzetu, jamani tufanyeje? .

Nilikuwa na Kabula Kinondoni kwa wapemba tumefata chips mara tukaskia mtu anasema me Rayc nataka kuvua nguoo, nikajua utani kushuka ni Ray C anasema nishikeni kuna watu wanataka kuniteka, alikua na nguvu sana watu kamshika akaanza kuongea vitu havieleweki, akaanza kutafta kisu ajichome, watu walimzuia sana walishindwa akaaanza kugaragara kwenye matope akipiga KELELE kiukweli nilijikuta nalia mara ikaja gari YA polisi ikambeba ila kwa tabu sanaa alikua akipiga kelele jamani nisaidieni msiniache kiukweli mpk rayc anaondoka na ile gari yapolisi sikujua anapelekwa wapi alikua kama mtu alopata kichaa, YARRAB TUNAMSAIDIAJE RAYC?


Baada ya ujumbe huo, aliamua kupost video tena na kuandika:

Ray C hastahili haya jamani kweli Leo hii anafikia hatua hii? Najua hajitambui ila tumfikirie mwanamke mwenzetu ambae ni mamaake, anajiskiaje? Rayc nn kimekupata ? Hiii video inasambaa kila sehem kweli huyu ndo RAYC AMBAE NI NEMBO YA TAIFA?


Plz tumsaidie manake tusimhukumu? MBONA sisi kila siku mungu tunamkosea na hesabu makosa yetu? We need to do something jamani @tzshaderoom @mangekimambi_ @divathebawse @babutale @ @mwanafa @linexsundaymjeda @paulmakonda naomba tumstiri huyu mtu plz plz @lisa_fickenscher ( tunafanyaje kumsaidia jamani tusichoke me natamani aende rehab mwaka mzima) Leo rayc umedhalilika najua haikua akili yako mama DAAAAH hata sijui amepelekwa wapi maskini atakua amelala wapi?

Vipi kuhusu kesho Yake? Mamaake anajiskiaje? Inaumaa jamani tusikubali kumpoteza huyu dada nawaombaa tusaidiane @millardayo @rayc1982 my love kama hauko sawa jamani ongea na watz wapo tayari kujitolea kwa hali na mali my love.


 
Dah inatia huzun sana,
Hawaa wakina Ray c wapo weng sana hawana msaada.
We must du smthng
 
Alostoo.... sio unga wa sembe ule ni msala ukiuvaa umenasa, apelekwe sober house tu
 
Dah inatia huzun sana,
Hawaa wakina Ray c wapo weng sana hawana msaada.
We must du smthng
Nothing can be done to save all of them than abiding and stop the use of those harmful drugs. That is the only way.
 
Yeye mwenyewe anatakiwa kujitambua na kutambua njia za kushinda matatizo yake. Ni kweli mwenzetu ana matatizo na anahitaji huruma. Ingawa kama binaadamu twatakiwa kumuonea huruma mwenzetu, lakini kama yeye hataki kujionea huruma unafikiri wengine watawaza nini?
 
Sembe tamu sana huwezi kuacha kama hujapenda,mwenyewe
 
Nothing can be done to save all of them than abiding and stop the use of those harmful drugs. That is the only way.
Nakubalian nawe, ila sometng ifanyik kwa matokeo hasi yaliyopo
 
Nakubalian nawe, ila sometng ifanyik kwa matokeo hasi yaliyopo
Inasiitisha sana kwa huyu mdada. Mkuu wa Msoga alijitahidi Sana akampatia tiba. Baada ya kupona amerudia tena kulekule. Ni vigumu Sana kumnasua mtu ambaye yeye mwenyewe ameona mahala alipo panampendeza.
 
Ni huruma na huzuni kubwa sana Kwa kijana km huyu ambaye miaka michache nyuma aliitwa superstar leo hii ni teja chakaramu, duh kweli Dunia haina huruma. Ama kweli apandaye ubaya atavuna katika uharibifu!! #Rayc Teja!
 
Yataka moyo!? Kutoa msaada kwa mtu asiejitambua, yataka moyo. Hivi unafikiri kila siku ni lazima yeye na matatizo hayahaya yasiokwisha. JK kajitolea kumsaidia sana lakini wapi, mtu bado anabwia hayo makitu na wala hana dalili za kuacha. Anataka kuipima imani jamii? Mbona juzijuzi mwenzake kasaidiwa na anaendelea vizuri?
 
Tanzania kuna wengi wenye shida zaidi yke,,,jiulize kikwete wametumia sh ngapi kumtibia,zaidi ya mamilioni,mtu kama chidi benz watu wanahangaika,,wakati juzi nimeona baba mwenye mtoto wa miaka mitano ambaye hawezi kusimama wala kukaa anahitaji 350000 tu akafanyiwe ct scan...alaf tunahangaika na watu ambao walichagua maisha wanayoyaishi,,;Crap..
 
Video iliyosambaa mtandaoni ikimuonyesha Ray C amechanganyikiwa.
Tunaomba waliomsaidia Chid Benz wamsaidie na Ray C.

 
Ray C huyu?
Labda ni Mungu tu! [emoji134]
 
Huyu rayc afungwe gerezani muda mrefu kama miaka miwili ili aweze kutibiwa kwa usahihi tena asiwekwe magereza ya huko dar apelekwe mikoani atapona tu ,yy kashindwa kumaliza dozi hiyo ndio suruhu
 
Atakoma aliyepo magogoni kwa sasa si mkwere tena huyu wa sasa atampereka seo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…