Msanii Ray Kigosi aifumua serikali ya CCM na kuwaonya wasanii

Mdakuzi

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
4,294
Reaction score
6,872
Zimepita ziku chache tangu Ikulu iandae sherehe kubwa iliyoitwa ya Rais kuagana na wasanii, ambapo katika sherehe hiyo wasanii mbalimbali wa filamu na muziki walihudhuria na kuungana na viongozi kadhaa wa CCM pamoja na mgombea wao wa kiti cha Urais.
Sherehe hiyo ilikuja baada ya wasanii wa fani ya uigizaji kufungiwa milango ya Ikulu kwa kipindi kirefu, ilikuwa tangu baada tu ya maziko ya Steven Kanumba na baada ya hapo ni wanamuziki pekee ndio waliokuwa na nafasi ya kukutana na kiongozi huyo wa nchi.
Hata wakati ambao Ikulu iliandaa futari maalum kwa ajili ya wasanii, na kufuturu na wanamuziki pekee. Kisha kesho yake mkuu wa nchi akaifuta futari maalum iliyokuwa afuturu na waigizaji, tena ilifutwa dakika za mwisho wakati wasanii hao wakiwa njiani kuelekea Ikulu. Hilo linaonekana kama kumkera muigizaji Vincent Kigosi au Ray na kuamua kufunguka vilivyo kwa kuichana serikali ya CCM ambayo iliwatumia katika chaguzi zilizopita kisha kuwatupa, lakini baada ya kukaribia uchaguzi mkuu imewasogeza tena karibu kupitia sherehe hiyo.


Kupitia Instagram Ray ameandika yafutayo:

Ova
 
Heko kigosi wewe no kamanda CCM in adui namba moja kwa maisha ya mtanzania .Wakati ndio huu wakufanya mabadiliko kijana anayeishabikia CCM ni Wa kumwogopa kama ukimwi chagua UKAWA
 
Bongo movie njaa ndio inawasumbua.... Wana njaa sana alafu wanataka waishi maisha ya juu
 

Nijuavyo, Ray ni Team Ukawa/Lowassa, Bongo Movie wengine ni Jackline Wolper, Niva, Capturado, Cheni, Shija, Anti Ezekiel, Mtitu etc. Na wanamuziki ni Juma Nature na kampani yake ya Wanaume Halisi, Tundaman etc...
 
Akili migando mingi kule, wakike washazoea maisha ya kupewa vya bure na kugongwa gongwa...unadhani kuna wanachokielewa. Afadhali ya huyu kaamka
 
Labda kwa sasa, ila kipindi kile cha kutangaza nia hukumuona mwanza kwa Wassira?
Lindi mtama huko kwa Membe?
Ila ni jambo jema kumuona kazinduka kutoka kwenye njaa kali wanazoendekeza wasanii wenzie.

Nina uhakika na kile nisemacho. Huwa wana vikao vyao pale Leaders Club, siku moja JB alitaka kujiunga nao lakini alifukuzwa kama mbwa mwizi, kwa kuonekana ndumilakuwili..
 
Mwanangu nifah, huyu kijana mwenzenu ametamka hayo na sidhani kama alikuwa seriously. Vinginevyo amejitoa muanga kwa jinsi unavofaham mfumo mzima unapousemea vibaya.
 
Halafu design kama wengi wa wanaokimbiliaga CCM wanafuata fursa tu.

Ray kaongea point kabisa.
Wenye masikio na wasikie
 
Mh!!
Sawa....ila kwa wana mabadiliko kama sisi hili ni jambo jema kabisa.
Tunahitaji kuona wasanii wengine wakifunguka kama yeye.
Nahisi mnapeana moyo kwa sasa huku ile sheria ikiwa inapata moto, we gonna see soon.
 
Hongera sana Ray umeonesha kujitambua...achana na hao team njaa wasiojielewa.
 
Huyu jamaa hata aandike nini hawezi aminika ktk jamii.

Mwanaume mwenye umri wake bado anaishi ka mtoto . Maisha yake ya kuokota malaya hovyohovyo na kugwaya ku assume full responsibility kama baba mwenye familia vinamshushia hadhi na hawezi aminika. Labda awakusanye watu wa type yake.
 
leo wale mazombie yaliyoalikwa mliman city kula piza na bia kila zimbie leo eti limejifanya ni Team CCM na Team Magufuli wakiongozwa na porn star wao sepetu

Kumuita mtu "porn star" ilhali yeye hajajiweka hadharani kuwa hiyo ni shughul yake ni utovu wa nidhamu katika infinity level,,,
 

Na vile vipuri anavovaaga me huwa simpendei hapo tu,kwan akiigiza bila heren inakuaje
 
Hongera sana Ray umeonesha kujitambua...achana na hao team njaa wasiojielewa.

Nimefanya kazi na wasanii kwa kipindi kirefu kidogo.
Ninajua wazi kuwa hakuna wakati ambapo muziki na sanaa umetambulika kama ajira, biashara na fani rasmi katika sekta za kiuchumi kama katika serikali awamu ya nne. Tumetoka mbali na changamoto kubwa bado zipo zifanyiwe kazi.

Muziki na sanaa hivi sasa vinamchango mkubwa kwenye GDP.
Mnyonge mnyongeni lkn haki yake mpeni.

Wasanii wetu wakubwa wa level ya Ray wananyonywa ni kwa sababu ya kubweteka na kusubiri kila kitu kiletwe na serikali. Mtu anasubiri serikali isimamie mauzo ya kazi zake, kumtafutia soko na kufanya mikataba.. wengi hawajifunzi na kutumia njia ka kisasa za usimamizi wa kazi zao na biashara zao kama lilivyo kwa makampuni..ingekuwa biashara zingine za sekta binafsi zinaendeshwa hivyo tungeshahama mji siku nyingi.

Sheria za intellectual property zishaendelea sana siku hizi. Na kuna fursa kibao zinazotokana na technolojia ya kisasa amabayo haitumiki kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…