Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,294
- 6,872
Zimepita ziku chache tangu Ikulu iandae sherehe kubwa iliyoitwa ya Rais kuagana na wasanii, ambapo katika sherehe hiyo wasanii mbalimbali wa filamu na muziki walihudhuria na kuungana na viongozi kadhaa wa CCM pamoja na mgombea wao wa kiti cha Urais.
Sherehe hiyo ilikuja baada ya wasanii wa fani ya uigizaji kufungiwa milango ya Ikulu kwa kipindi kirefu, ilikuwa tangu baada tu ya maziko ya Steven Kanumba na baada ya hapo ni wanamuziki pekee ndio waliokuwa na nafasi ya kukutana na kiongozi huyo wa nchi.
Hata wakati ambao Ikulu iliandaa futari maalum kwa ajili ya wasanii, na kufuturu na wanamuziki pekee. Kisha kesho yake mkuu wa nchi akaifuta futari maalum iliyokuwa afuturu na waigizaji, tena ilifutwa dakika za mwisho wakati wasanii hao wakiwa njiani kuelekea Ikulu. Hilo linaonekana kama kumkera muigizaji Vincent Kigosi au Ray na kuamua kufunguka vilivyo kwa kuichana serikali ya CCM ambayo iliwatumia katika chaguzi zilizopita kisha kuwatupa, lakini baada ya kukaribia uchaguzi mkuu imewasogeza tena karibu kupitia sherehe hiyo.
Kupitia Instagram Ray ameandika yafutayo:
Ova

Usiku wa jana nimetafakari vitu vingi sana kuhusu nchi yangu iliyobarikiwa kila aina ya utajiri wa madini mbuga za wanyama wakiwemo aina mbalimbali za wanyama wa kuvutia na hekta kubwa za misitu ila ninaona vipofu wengi sana wasioelewa nini tulichobarikiwa ndani ya Tanzania yetu. Tumeingizwa mikenge mingi sana katika mikataba tena mibovu, bajeti kandamizi kwa watu wa hali ya chini mifumuko ya bei kila kukicha hali ngumu kwa wasanii wa Tanzania kila siku ahadi zisizotekelekeza.
Why nasema hivyo wasanii wenzangu?
Tumeumia kwa kipindi kirefu sana bila msaada wowote, hatuna hakimiliki ya kazi zetu, zinaibiwa kama njugu sokoni Kariakoo yaani tulitupwa kama takataka kwenye dampo, lakini sasa hivi kipindi cha uchaguzi ndio tunaonekana umuhimu wetu. Tuamke na kuwaambia wananchi wachague viongozi makini watakaoweza kutuvusha Watanzania kwenda hatua nyingine. Tuna watu wengi sana nyuma yetu wanaotuamini sisi wasanii kama kioo cha jamii, tusiwapoteze Watanzania kuwaambia viongozi wa chama fulani ndio wanafaa kwa vijisenti vidogo tunavyopewa. Watanzania huu ni wakati sahihi wakutulia na kuwachagua viongozi makini wanaofaa. Ni katika kukumbushana tu, Waswahili wanasema utakaokata nao kuni ndio utakao ota nao moto.
Ova