Msanii Roma Mkatoliki amevuka mstari mwekundu lakini anachekewa tu!

Tusikubali kuwa wafuasi wa giza la mwendazake! Kuna uwongo hapo?
Mstari mwekundu ndio unaosababisha tuibiwe hadi leo! Hivi nani hajui kuwa msoga group ndio wenye nchi sasa hivi. Hivi makamba, Ritz1, etc sio msoga group? Tusidanganye jamani wala kutishana hasa anapotokea mwenzetu kuibua mambo ya kweli! Kazi ya msanii ni kuonya na siyo kuwa praise group nyakati zote>
 
We jamaa ni mchochezi tu. Yaani watanzania woote wameusikiliza ila wewe tu ndio umeona umevuka mipaka??

Hivi kwanini mnapenda ugomvi?

Unataka Rais Samia na yeye aanze ile michezo yenu?

Kwa Taarifa yako Mh Rais Samia yuko bize kuwaletea Watanzania Maendeleo hana muda wa kupoteza kwa vitu visivyo na msingi.

Mama Piga Kazi watanzania wapenda amani na Maendeleo tuko Nyuma yako wasikuyumbishe.
 
Kwani remote ikiwa msoga,kuna tatizo gani?
 
Tafsiri ni ya kwako kwa sababu Roma hakuna mahala amemtaja JK.

Uchawa ni mzigo sana
 

Huu ni mtazamo ya kijamaa ambapo rais anaonekana ni mungu mtu. Kwa akili hizi viongozi wetu wataendelea kupora chaguzi na kukaa madarakani kwa shuruti, maana wanajua wakishapata madaraka watatokea wajinga wa aina yako wa kuwasujudia na kuwakinga wakipewa ukweli wao.
 

Nchi ikiongozwa Watu wanaojiona Duni na wasiojiamini kama wewe ndio inaingia kwenye shida.

Yeye kaona hivyo na pengine anasababu ya kuona hvyo.
Kwa hiyo wewe unayeona Roma anatumiwa na watu Fulani(anarimotiwa) ukamatwe Kwa Mtazamo wako huo?

Alafu aliyekuambia Ukiwa Rais au Mtawala hauwezi kurimotiwa ni Nani?
Kama Rais akiamua kurimotiwa wewe inakuuma nini?

Hiyo rimoti ukimpeleka Mahakamani akasema rimoti ni Kupata muongoza na ushauri Kutoka Kwa wazee WA taifa akiwemo huyo WA msoga bado atakuwa na Makosa?

Ninyi ndio mkiwa karibu na Watawala ndio mnaua na kuweka Watu ndani kisa kutokujiamini.
 
Asante sana Robert.

Moderators futeni nyuzi kama hizi zinaleta uchochezi.
 
Roma yuko Marekani, hayo ni mambo ya kawaida kabisa huko Marekani. Huko Rais anasemwa kama kawaida kwa kila namna katika CNN, Fox News n.k
 
Wee chawa kwani kasema uongo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…