Msanii Ruby kuwa msanii wa kwanza kuburuzwa mahakamni kwa kutumia wimbo wa msanii mwenzie kujiingizia kipato? Wasanii wanalakujifunza? COSATA je?

Msanii Ruby kuwa msanii wa kwanza kuburuzwa mahakamni kwa kutumia wimbo wa msanii mwenzie kujiingizia kipato? Wasanii wanalakujifunza? COSATA je?

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam wana jamvi.

Muziki wetu umukuwa sana kwa sasa tunaweza sema ni ukweli uliowazi kuwa biashara ya sanaa na muziki ni moja ya biashara kubwa kabisa kwa sasa nchini kwa sababu kuna watu wana tajirika kupitia muziki na wengine wana filisika kabisa kupitia muziki huu huu.

Ni ukweli usiopingika kuwa kila biashara ina miongozo yake na kanuni zake lakini kwa bahati mbaya kabisa muziki wetu na sanaa yetu inaonekana haina miongozo kabisa wala kanuni kuhusu haki za waunda sanaa na watengezaji muziki lakini jambo ambalo si kweli japo kuna madhaifu kwenye baadhi ya miongozo na kanuni lakini biashara ya muziki na sanaa ina sheria na kanuni japo zinahitaji maboresho ndio maana tuna kitu kinaitwa" COSOTA'"

Hivi karibuni kumezuka tabia kwa baadhi ya wasanii kutumia nyimbo za wasanii wenzao tena ambao bado wako hai kwenye sanaa tena wanao hit na kuziimba kwenye majukwaa yaliyo andaliwa kwa wao kujipatia kipato na huwa wanaimba wimbo mzima bila hata ruhusa ya mwenye wimbo au kuwa katika label moja....na haya yamekuwa mazoea kiasi kwamba ni kawaida kuusikia wimbo wa msanii yeyote kwenye show ambazo hata hazimuhusu tena wimbo unaimbwa na msanii mwenzie na hela yote ana weka mfukoni peke yake bila kujua ametumia haki za watu na anapaswa kulipa.

Hivi karibuni nimesoma documents sehemu ambazo zimeandaliwa kufungua case ya madai dhidi ya msanii Ruby kutumia nyimbo za baadhi ya wasanii wawili(majina kapuni) kutumbuiza na kujipatia kipato bila kuwa na ruhusa za wamiliki wa nyimbo hizo na wamiliki halali wa midundo(beats) za nyimbo husika............. na wahusika wanataka kulipwa haki yao kutokana na kipato alicho ingiza msanii Ruby alipotumia nyimbo zao kwenye baadhi ya matamasha hivi karibuni.......... na wanataka kuweka zuio mahakamani kuiomba mahakama izuie pesa anazo lipwa Ruby kwenye show zake mpaka hapo case ya msingi kuhusu madai yao itakapo tolewa maamuzi.

Ni ukweli usiopingika kuwa kama Ruby anatumia nyimbo za wasanii wenzie kutumbuiza kwenye matamasha yanayo muingizia pesa bila ruhusa ya wahusika ni bora akaacha mara moja kwakuwa hili jambo linaweza haribu kabisa ndoto zake na akabaki ana zunguka mahakamani kila kukicha....
Ruby ni msanii mzuri sana ana uwezo mkubwa sana hana sababu ya kutumia nyimbo za wasanii wenzie kama sehemu ya show yake kujiingizia kipato kwakuwa Ruby anazo nyimbo nyingi tuu zinazo pendwa na kila mtu na kila mmoja kwa hiyo ana jiingiza kwenye matatizo kwa kujitakia tuu...

Ruby na wasanii wengine lazima wajifunze kuwa biashara ya mziki kama zilivyo baishara zingine ni kama vita na hakuna kuoneana huruma kabisa hivyo walio karibu na Ruby wamwambie ajiandae kisaikolojia kwani watu sasa watatumia udhaifu alio uonesha kumpiga......
Ninani meneja wa Ruby? Hakujua msanii wake anafanya makosa na kurudia makosa?

Nilifikiri Wasanii walijifunza kilicho ikuta kampuni moja ya mawasiliano kwa kutumia wimbo wa AY na FA ......
Ni vyema sasa COSOTA wakaamka na kuanza kutoa elimu na semina kwa wasanii wasiendelee kujiingiza kwenye matatizo yasiyo ya lazima.

Kila la kheri Ruby bila shaka yatakwisha/mtayamaliza na hautorudia makosa.

Wasalaam
 
Sasa kama hutaki kutaja majina ya nyimbo alizotumia tutaelewa vipi msingi wa mada yako!!!!

Kama wewe ni mfatiliaji wa sanaa basi una sababu ya kuuliza hili swali maana hata jana tuu kafanya kosa tena kutumia wimbo wa Isha mashauzi kutumbuiza kwenye Rhumba festival....sasa sijui aliwa hajapewa taarifa kuwa aache maana kuna wengine wamajipanga kumsue?
 
Waziri juzi kasema MC anayetumia nyimbo kusherehesha harusi n.k. nao watachajiwa wamlipe aliyeimba.. yaani wakipiga tu nyimbo ya msanii watalipa..

Kasema wanalipwa mamilioni kwa kazi moja na walioimba hawapati chochote..

Kasema hili wanalipanga kwa sasa ili lije lianze..
 
Hakika.....
 
Naona kwenye sherehe za Bongo zitakuwa zinapigwa nyimbo za nje tu
 
Ivi ukiwa mwana ccm lazima uwe mpumbafu pumbafu jinga jinga

Sasa kapun ndo nin kamai siyo ungese

Unaleta maada kwa id fake afu bado fara fara muoga muoga kibwege bwege

Shwain
 
Waziri juzi kasema MC anayetumia nyimbo kusherehesha harusi n.k. nao watachajiwa wamlipe aliyeimba.. yaani wakipiga tu nyimbo ya msanii watalipa..

Kasema wanalipwa mamilioni kwa kazi moja na walioimba hawapati chochote..

Kasema hili wanalipanga kwa sasa ili lije lianze..
"naipenda jumamosi yangu" iliishia wapi mkuu
 
"naipenda jumamosi yangu" iliishia wapi mkuu

Mwandishi kasema anatoa kitabu.. itaendelea tu humu pia kama kawa.. hakutumia akili kuimaliza hii then aandike zingine na vitabu ndio angeuza vingiiiii sana.
 
Ivi ukiwa mwana ccm lazima uwe mpumbafu pumbafu jinga jinga

Sasa kapun ndo nin kamai siyo ungese

Unaleta maada kwa id fake afu bado fara fara muoga muoga kibwege bwege

Shwain

Hahahaha imebidi nicheke tuu.... mkuu pole sana
 
Back
Top Bottom