Msanii siyo kioo cha jamii bali ni mwalimu wa jamii.

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Waungwana habari!
Nimekuwa nikisikia mara nyingi watu wakisema msanii ni kioo cha jamii. Wamekuwa wakisema hivyo kwa maana kwamba watu humtazama msanii na maisha yake na wao huishi vivyo hivyo. Wanaopigia chapuo hoja hii wanaamini kwamba tabia, maadili na matendo ya msanii ni muhimu kwa jamii na ndiyo kioo chenyewe, wanaamini jamii inajitazama kwenye maisha ya msanii na kujirekebisha.

Mimi binafsi napingana vikali na nadharia hii kwani haina uhalisia katika maisha ya leo ya mtanzania. Msanii siyo kioo cha jamii bali ni mwalimu wa jamii. Mwalimu ni mtu anayetoa elimu kwa jamii katika jambo analolielewa vyema. Msanii wa Tanzania siyo kioo cha jamii kwa sababu maisha anayoishi hayana uhalisia na matendo yake yamejaa drama na ya kuigiza. Jamii ya kitanzania haijifunzi tena kwenye maisha na mienendo ya msanii bali inajifunza zaidi kwenye kazi zake za sanaa (fasihi). Fasihi ndiyo kioo cha jamii, kwa maana kwamba jamii inajifunza kwa kile anachoimba msanii zaidi.

Kwa mfano msanii kama Bahati Bukuku aliyeimba wimbo wa "umewazidi wote", anajaribu kuwaasa wanandoa kuheshimiana, kupendana na kuvumiliana halafu yeye binafsi hana ndoa na ndoa yake ilimshinda anakuwaje kioo cha jamii zaidi ya ile kazi yake?. Katika mfano huu Bahati Bukuku hawezi kuwa kioo cha jamii katika swala la ndoa, lakini wimbo wake " umewazidi wote" ndiyo kioo cha jamii kwani jamii na wana ndoa watajipima kupitia alichokiimba na kujirekebisha. Yeye msanii Bahati Bukuku atabakia kama mwalimu wa jamii kupitia kazi zake ambao ndiyo kioo.

Chukulia mfano mwingine wa msanii kama Diamond Platnumz ambaye amekuwa nguli wa kuimba nyimbo za mapenzi akihimiza wapenzi kuwa waaminifu na kutokusalitiana, kupitia nyimbo zake kama "nataka kulewa", " nitarejea", "utanipenda", " marry you", na nyinginezo anahimiza wapenzi kupendana na kuvumiliana, anapinga usaliti katika mapenzi. Lakini maisha halisi ya kimapenzi ya Diamond Platnumz yamejaa kusalitiana na kukosekana kwa mapenzi ya dhati. Kama tukisema msanii ni kioo je jamii inajifunza nini kwenye maisha haya ya Diamond Platnumz? Kama jamii itajiangalia kwenye kioo hili na kujipima mwisho wa siku itajikuta inapotoka kabisa.
Lakini jamii itajifunza zaidi kwenye nyimbo za Diamond Platnumz na kujipima kupitia yale anayoyaimba kuhusu mahusiano na si kupitia maisha yake binafsi.
Nahitimisha kwa kusema kuwa msanii siyo kioo cha jamii bali ni mwalimu wa jamii anayefundisha kupitia kazi zake za sanaa. Lakini kazi zake za kisanaa ndiyo kioo cha jamii, jamii inatakiwa ijitazame na kujipima kwenye nyimbo na maigizo ya wasanii.

Nakaribisha mjadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio lazma iwe maisha yake Binafsi ndio kioo cha jamii!
Ile kazi yake unapoisikiliza ndio ujione au uione jamii unayoishi!

Mfano;
Tumesoma vitabu mbali mbali vya Ngugi wa thiong'o unaiona jamii kupitia ile kazi yake ya sanaa Sio unaiona jamii kupitia maisha yake binafsi!
The same to lucky dube sikiliza kama Its not easy! slave, etc

Nadhani lengo kuu kusema msanii ni kioo cha jamii ilikua ni jamii ijione kupitia kazi ya msanii Sio mambo yake binafsi!
 
Msanii ni kioo cha jamii,Sio anachofanya msanii jamii ijifunze,hiyo sio maana ya kioo...

Kioo means jamii inajitazama kwa wasanii,,means wanayofanya wasanii ndio mambo yaliyo kweny jamii yetu..ni jambo lipi kafanya msanii halaf mtaan likawa halijawah kufanywa before?

Hivyo wasanii wana represent jamii ilivyo..ukiona msanii katoboa pua,,bas jua jamii nayo ndio michezo yake..huu ndio ukwel..

Msanii ni kioo cha jamii.

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 
Mh siyo kweli maisha ya msanii wa kitanzania hayana uhalisia ni maisha ya kisanii. Hata hivyo kioo kinampa mtu nafasi ya kuona wapi amekosea ili ajirekebishe, kwa mtu kuona tu maisha ya msanii atajuaje kuwa amekosea?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio lazma iwe maisha yake Binafsi ndio kioo cha jamii!
Ile kazi yake unapoisikiliza ndio ujione au uione jamii unayoishi!

Mfano;
Tumesoma vitabu mbali mbali vya Ngugi wa thiong'o unaiona jamii kupitia ile kazi yake ya sanaa Sio unaiona jamii kupitia maisha yake binafsi!
The same to lucky dube sikiliza kama Its not easy! slave, etc

Nadhani lengo kuu kusema msanii ni kioo cha jamii ilikua ni jamii ijione kupitia kazi ya msanii Sio mambo yake binafsi!
Kwa maana hiyo ni sawa ni kisema kioo cha jamii siyo msanii bali kazi yake ya kisanaa (fasihi) ndiyo kioo cha jamii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mh siyo kweli maisha ya msanii wa kitanzania hayana uhalisia ni maisha ya kisanii. Hata hivyo kioo kinampa mtu nafasi ya kuona wapi amekosea ili ajirekebishe, kwa mtu kuona tu maisha ya msanii atajuaje kuwa amekosea?

Sent using Jamii Forums mobile app
Wasanii wanafanya mambo yaliyopo kweny jamii yao...Amin nakwambia hakuna kitu msanii anafanya ambacho jamii haijawah fanya.

Yani Ukitaka kujua maisha ya waTz basi angalia wasanii..ndio jinsi tulivyo

Unapo jitazama kweny kioo unamuona msaanii au unajiona wewe?

Sent from my SM-G920P using Tapatalk
 
Dhana ya Msanii ni Kioo cha Jamii inatafsiriwa ndivyo sivyo! Kwamba, eti msanii anatakiwa kuwa na maadili mema kwa sababu watu wanajifunza kutoka kwake... inawezekana ni sahihi lakini hiyo sio maana halisi ya kuwa kioo cha jamii!

Wengi wetu tunakifahamu kioo! Ukisimama mbele ya kioo, hapo hapo kitakupa taswira yako halisi! Kama ulijiremba na ukadhani umerembeka, ukishaenda mbele ya kioo kitakuambia kinyume chake... kitakuonesha taswira yako!

Msanii ni Kioo cha Jamii kwa sababu anatoa reflection ya jamii husika!! Hata kama hujafika mahali kama US, lakini ukiangalia African American Artists and White Artists, wala hautapata taabu kufahamu taswira ya watu weusi na watu weupe wa Marekani!

Leo hii tukiwachukua Diamond Platnumz kisha ukampeleka Greenland na kumwacha huko awe huru, then kupitia matendo ya Diamond Platnumz (kioo cha jamii ya KItanzania), itawasaidia sana The Greenlanders kufahamu Watanzania ni watu wa aina gani!!!!

Na mambo YOTE, I repeat, YOTE yanayofanywa na wasanii hata kama ni ya hovyo kiasi gani; wao wanaya-copy kutoka kwenye jamii zao!! Ni mambo ambayo yamekuwa yakifanyika, si ajabu hata kabla ya mama zao hawajazaliwa... ni vile tu hayakupata reflector!

Sasa kwavile msanii ana halaiki kubwa nyuma yake, ndipo anapata fursa ya kuonesha kilichopo kwenye jamii husika kupitia matendo yake ambayo, hata kama tutajifanya kulaani namna gani, kimsingi ndicho tunachokifanya huko mitaani, na kukipenda!

Tena basi si unaona mfano wako mleta mada! Kwamba, pamoja na Diamond kuimba nyimbo nyingi zinazohamasisha upendo, yeye mwenyewe akiwa ni cheater kweli kweli!!

Hivi kuna mjadala suala la Watanzania kutokuwa waaminifu kwenye mapenzi?! Kuna mtu anaweza kubisha suala la Watanzania kupenda ngono?!

Msanii ni Kioo cha Jamii kwa sababu, mtu asiyeifahamu Tanzania anaweza kuwa na picha halisi ya Watanzania linapokuja suala la mapenzi, na anaweza kupata picha hiyo kupitia kwa akina Diamond ambao ndio kioo cha jamii ya Kitanzania... kioo kinachotoa taswira rasmi ya Watanzania!!!
 
Mkuu hapa ndiyo nachanganyikiwa kabisa, je tukisema msanii ni kioo cha jamii kwa sababu anayoyafanya ndiyo yaliyopo kwenye jamii huoni kama tunakuwa hatumaanishi kioo tena bali tunamaanisha "mfano" au pengine "sample" ya jamii husika?

Hebu chukulia mfano huu
Mtu anakwenda mbele ya kioo kujitazama kupitia kioo anajiona jinsi alivyo hivyo anapata nafasi ya kuona amekosea wapi na kujirekebisha. Pia mtu anapokwenda mbele ya kioo anaweza kuamua kujitazama sehemu moja tu ya mwili mfano sikio pekee.
Turudi kwenye maana yako sasa, kama msanii ni kioo cha jamii husika tunatarajia anayekwenda mbele ya kioo na kujitazama ni jamii husika na siyo kwama eti watu kutoka jamii nyingine waitazame jamii ya Tanzania kupitia msanii.

Pia kama msanii atakuwa kioo cha jamii kwa maana yako sioni kama kioo hicho kikimpa nafasi ya anayejitazama "jamii" kujikagua na kujirekebisha kupitia msanii.

Ndiyo maana nikasema msanii atakuwa mwalimu wa jamii lakini siyo kioo. Kazi zake "muziki, maigizo nk" ndiyo kioo cha jamii. Kazi hizi za msanii ndiyo zinazoreflect yaliyopo kwenye jamii na jamii inajiangalia kupitia kazi hizi na kujirekebisha.

Itakuwa mfano kivipi?! Kioo kinaonesha taswira ya kitu halisi bila chenga chenga!

Hivi sasa hapo ulipo ukijangalia kioo, utakachokiona ni taswira yako halisi!!! Na kama msanii ni kioo cha jamii, basi nae kama kioo atakuwa anaonesha taswira halisi ya jamii husika!!

Wewe Mwanajamii ambae unaweza kudhani jamii yako ina maadili kweli kweli labda kwavile haujichanganyi; basi jaribu kuifahamu jamii yako kupitia kioo cha jamiii ambacho ni wasanii!!!! Na hii si kwa wanajamii husika tu!!

Ili mradi Msanii ndie kioo cha jamii husika, basi kupitia wasanii unaweza kupata taswira ya jamii hata isiyo ya kwako!! Ndo maana nikakupa mfano wa African Americans na Wazungu ndani ya US!! Kwa kuangalia wasanii kutoka kwenye haya makundi mawili ya Wamarekani, unaweza pia kupata taswira ya jamii za Wazungu na African Americans hata kama hujawahi kufika America kwa sababu wasanii hawa watakuwa reflection ya jamii zao!
 
Back
Top Bottom