Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,237
Msanii Khalid Mohamed aka Top In Dar (TID) ameibuka na kutaka chama cha Demokrasia na Maendeleo kimlipe kwa kutumia neno "Ni Yeye" katika kampeni zao. Msanii TID anadai neno "niyeye" ni ubunifu wake
Lakini hata hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 5 hadi cha 7 cha Sheria ya Hakimiliki ya mwaka 1999, Copyrights and Neighbouring Act of 1999, "maneno" na "mawazo" ya wasanii si sehemu ya vitu vunavyotakiwa kulindwa chini ya Sheria hiyo.
Sheria hiyo imeweka wazi kuwa inalinda kwa lugha ya kisheria "expressions" and not "ideas".
Ijulikane wazi kuwa wazo linaweza kufanana na la msanii mwingine lakini namna ya kulieleza na kuliwasilisha wazo husika inaweza kuwa tofauti kabisa toka msanii mmoja hadi mwingine.
Kwa mfano wasanii wawili wanaweza kuwa na wazo la kuimba wimbo wa mapenzi wa mwanamke masikini kumpenda mwanaume tajiri lakini si rahisi kutumia beat na melody ya aina moja. Wanaweza pia wakajikuta wanatumia baadhi ya maneno sawa kwa mfano katika scenario hiyo neno kama " mapenzi" "nakupenda" etc yanaweza tumiwa na wote lakini kwa namna tofauti.
Hivyo kinacholindwa na sheria ni "expression" yaani ule ufundi na ubunifu wa msanii wa kulielezea jambo na siyo "maneno" anayotumia msanii wala "wazi" la msanii.
Isipokuwa tu maneno husika yawe yamesajiliwa chini ya sheria nyingine mfano kama trades mark au service mark ya bidhaa ya mhusika na anayetumia awe anatumia katika namna inayovunja haki au kuwachanganya wateja wa bidhaa hizo mbili. Jambo ambalo katika mazingira haya halipo.
Kwa vyovyote vile huwezi kusema kutumia kwa neno niyeye kwa CHADEMA achilia mbali tu kwamba halilindwi chini ya copyright laws bali tu hakuna madhara yoyote ya kiuchumi anayoyapata TID na vilevile CHADEMA hawalitumii kujiingizia pesa hivyo ni "fair use".