Uchaguzi 2020 Msanii T.I.D aitaka CHADEMA imlipe kwa kutumia neno "Ni Yeyee" kwenye kampeni zao

Uchaguzi 2020 Msanii T.I.D aitaka CHADEMA imlipe kwa kutumia neno "Ni Yeyee" kwenye kampeni zao

Huyu naona mbwimbwi limemzidia tu mpaka anaweweseka! Afanye mziki ndio kipaji alichopewa na sio kutegemeakuingiza kipato kwa slogan zake uchwara.
 
Waendelee kuwanengulia CCM wataishia kuwa na wafuasi na mashabiki na watoto wa shule
 
Kutafutiana ban hatutaki jamani ,watu tukitulia mnakuja kutuchokoza hivi kwa nini?
 
dah...ndugu zanguni chadema ni bora mkamtafuta kigogo mkamalizana nae tu,huyu jamaa ninavyomjua akili zake akianza kudeal perpendicular na huyo aliyemuibia idea yake ( Tundu lisu) aisee atamshusha sana umaarufu na kumpunguzia kura zake za urais [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Akadai haki yake Mahakamani kama hatimiliki ya neno " ni yeye".
 
Tanzania itatoka hapa ilipo baada ya watu Kama Hawa kupungua

Who Is tid
 
Akawashtaki na WaEbrania
IMG_20200805_205953.jpg
 
Aingie google aandike hiyo sentensi ndiobatajua kuwa hata yeye kaidukua kwenye kwaya.
 
Msanii Khalid Mohamed aka Top In Dar (TID) ameibuka na kutaka chama cha Demokrasia na Maendeleo kimlipe kwa kutumia neno "niyeye" katika kampeni zao. Msanii TID anadai neno "niyeye" ni ubunifu wake

Lakini hata hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 5 hadi cha 7 cha Sheria ya Hakimiliki ya mwaka 1999, Copyrights and Neighbouring Act of 1999, "maneno" na "mawazo" ya wasanii si sehemu ya vitu vunavyotakiwa kulindwa chini ya Sheria hiyo.
Sheria hiyo imeweka wazi kuwa inalinda kwa lugha ya kisheria "expressions" and not "ideas".

Ijulikane wazi kuwa wazo linaweza kufanana na la msanii mwingine lakini namna ya kulieleza na kuliwasilisha wazo husika inaweza kuwa tofauti kabisa toka msanii mmoja hadi mwingine. Kwa mfano wasanii wawili wanaweza kuwa na wazo la kuimba wimbo wa mapenzi wa mwanamke masikini kumpenda mwanaume tajiri lakini si rahisi kutumia beat na melody ya aina moja. Wanaweza pia wakajikuta wanatumia baadhi ya maneno sawa kwa mfano katika scenario hiyo neno kama " mapenzi" "nakupenda" etc yanaweza tumiwa na wote lakini kwa namna tofauti.

Hivyo kinacholindwa na sheria ni "expression" yaani ule ufundi na ubunifu wa msanii wa kulielezea jambo na siyo "maneno" anayotumia msanii wala "wazi" la msanii.

Isipokuwa tu maneno husika yawe yamesajiliwa chini ya sheria nyingine mfano kama trades mark au service mark ya bidhaa ya mhusika na anayetumia awe anatumia katika namna inayovunja haki au kuwachanganya wateja wa bidhaa hizo mbili. Jambo ambalo katika mazingira haya halipo.

Kwa vyovyote vile huwezi kusema kutumia kwa neno niyeye kwa CHADEMA achilia mbali tu kwamba halilindwi chini ya copyright laws bali tu hakuna madhara yoyote ya kiuchumi anayoyapata TID na vilevile CHADEMA hawalitumii kujiingizia pesa hivyo ni "fair use".

View attachment 1527556

Huyu dish limeshayumba,halafu Polepole naye anaishikia bango, yaani CCM safari hii wamechanganyikiwa mbaya.
 
Back
Top Bottom