Taratibu jamani......
Mwancheni dogo naye atusue. Maadamu remix zake zinabamba, sioni shida. Hata MwanaFA walisema anatafsiri nyimbo za Fedrostar, lakini tunaona hadi leo ni mkali. Hata T.I.D kwenye Nyota Yako tunajua ilikuwaje.
Lakini mbona kucopy nyimbo hata mamtoni kupo, tumesahau mkasa wa Haiti, akina Jimmy Fox, Wyclif Jean, Lionel Richie na wenzake akina Celin Deon wameimba wimbo wao. Na ktk kundi kubwa lote ni Lionel Richie pekee aliyekuwa kwenye original version ya wimbo ule.
Mbona tunawabania madogo, au tunataka waingie vichochoroni wakafanye ujasiriamali wa roba za mbao? Let's be serious. Mi dogo namkubali.