tatum
JF-Expert Member
- Jan 16, 2018
- 5,786
- 4,491
Msanii wa bongo movie Riyama Ally uliyechaguliwa kushiriki Tuzo za Sinema zetu pale Mlimani city na hukwenda lakini umemjibu vibaya mmoja wa wapenzi wa sinema kuwa tuzo hizo ni kama ulihongwa tu sidhani kama ni maneno mazuri sana.
Kwasababu Mkurugenzi wa Azam Media Tido Mhando alitoa maelezo kuwa walipokea filamu nyingi sana na majaji walizichuja kwa vigezo bila hata kujuana na kufikia maamuzi ya nani anastahili tuzo.
Sasa kama na wewe uliwekwa katika mizani na ukashinda basi heshimu waliokuchagua na si kukebehi Tuzo hizo utajiharibia watazamaji na majaji wameheshimu kipaji chako.