Msanii wa bongo muvi ang'aka akidai kusingiziwa mtoto wa miaka 10

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Posts
1,817
Reaction score
4,061

Chekibud anadai mwanamke anamsingizia kuwa mtoto ni wake kwa kuwa wanafanana anadai anafanana na watu wengi na sio watoto wala ndugu

mwanamke anadai walikutana club billicanas wakafanya kwa usiku mmoja kisha akashika mimba na kuzaa
 
Hivi inakuwaje wana bishana kwa mdomo wakati DNA ipo!!? Au ndio bwana chekibud ana tafuta kiki!!?
Halafu hata usiku mmoja mtoto anaweza kupatikana sjui elimu yake ali ipatia wapi na sijui alisoma mpaka darasa la ngapi huyo jamaa.

Am out!
 
Kufanana wala si ishu, mimi nimefananishwa sana hadi nikafikiria ingekuwa sura zinazofanan ni majambazi au zinafanya matukio mabaya nahisi ningekuwa segerea hadi leo. maana kila mkoa nakutana na watu wanaonifananisha....hadi sasa rekodi yangu...
  1. Morogoro....nilifananishwa na kondakta wa daladala ya mjini..kihonda
  2. Njombe...nilifananishwa na muuza duka la mpesa
  3. Dodoma.....kuna wanafunzi wa udom walisema mm nilikuwa nawatembezea vitu hivi sasa nimewakimbia
  4. Mwanza/misungwi.....nilifananishwa na bwana mmoja mkazi wa maeneo ya karibu
  5. Misenyi......walisema nafana na afisa mmoja pale ofisi za halmashauri
  6. Karagwe....nikafanaishwa na mtumishi wa Mungu wa kanisa la TAG
  7. Kahama.....nikafananishwa na mfanyabiashara mmoja
  8. Basihaya/bunju.....nikafananishwa na jamaa mmoja afisa wa benki ya azania
  9. Majimoto/mpanda...nikafananishwa na mwanajeshi na walikuwa wakiniogopa hadi naondoka hawakuamini
  10. Sanawari/arusha.....kuna jamaa hadi sasa tunawasiliana yaani ameniganda hadi nimechoka kukana naitikia, eti tulikuwa wote kule same wakati mm hata sijawahi kuishi same
  11. Vwawa/mbozi....nilifananishwa na mwalimu wa sekondari
Nabado, kuna watu wanaendelea kunifananisha...nashukuru si kwa ubaya maana nitabeba mzigo wa watu mda wowote aiseee!!!. Swala la kufananisha watu ni baya sana
 
Hivi inakuwaje wana bishana kwa mdomo wakati DNA ipo!!? Au ndio bwana chekibud ana tafuta kiki!!?
Halafu hata usiku mmoja mtoto anaweza kupatikana sjui elimu yake ali ipatia wapi na sijui alisoma mpaka darasa la ngapi huyo jamaa.

Am out!
Ila chekbud kaongelea masuala ya DNA pia katika hii clip
Yuko tayari kufanya
 
Hapa ndipo unapopata picha kamili ya matumizi ya KINGA..!!
Siku moja atakapogundilika star mmoja kama WEMA kuwa ameathirika na UKIMWI kutakuwa na vilio na kusaga meno.
 
Duh ...utakuwa na sura common sana jamaa.
 
Mtoto huwa hakataliwi hadharani bwege huyu, imeshatokea Lea tu atakuwa asipokufaaa wewe atawafaa wengine wanaokuhusu, Mtoto mwenyewe mkubwa umerahisishiwa mambo mengi tu,
 

Chekibud anadai mwanamke anamsingizia kuwa mtoto ni wake kwa kuwa wanafanana anadai anafanana na watu wengi na sio watoto wala ndugu

mwanamke anadai walikutana club billicanas wakafanya kwa usiku mmoja kisha akashika mimba na kuzaa
Dah hizi zinaa hizi?Unamkuta mwanamke disco humjui,na unamuudhi Mungu unafyeka kavu!huyu cheki budi hana tofauti na magaidi wa ISIS
 
Mapaka mwananmke kamfananisha nae ujue kuwa kulikuwa na uhusiano. Jama ni Madaktari mliomo humu mtueleze ni sekunde ngapi Ujauzito unapatikana maana huenda wengi wanahitaji elimu hiyo. The kid is so cute so innocent!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…