Kufanana wala si ishu, mimi nimefananishwa sana hadi nikafikiria ingekuwa sura zinazofanan ni majambazi au zinafanya matukio mabaya nahisi ningekuwa segerea hadi leo. maana kila mkoa nakutana na watu wanaonifananisha....hadi sasa rekodi yangu...
- Morogoro....nilifananishwa na kondakta wa daladala ya mjini..kihonda
- Njombe...nilifananishwa na muuza duka la mpesa
- Dodoma.....kuna wanafunzi wa udom walisema mm nilikuwa nawatembezea vitu hivi sasa nimewakimbia
- Mwanza/misungwi.....nilifananishwa na bwana mmoja mkazi wa maeneo ya karibu
- Misenyi......walisema nafana na afisa mmoja pale ofisi za halmashauri
- Karagwe....nikafanaishwa na mtumishi wa Mungu wa kanisa la TAG
- Kahama.....nikafananishwa na mfanyabiashara mmoja
- Basihaya/bunju.....nikafananishwa na jamaa mmoja afisa wa benki ya azania
- Majimoto/mpanda...nikafananishwa na mwanajeshi na walikuwa wakiniogopa hadi naondoka hawakuamini
- Sanawari/arusha.....kuna jamaa hadi sasa tunawasiliana yaani ameniganda hadi nimechoka kukana naitikia, eti tulikuwa wote kule same wakati mm hata sijawahi kuishi same
- Vwawa/mbozi....nilifananishwa na mwalimu wa sekondari
Nabado, kuna watu wanaendelea kunifananisha...nashukuru si kwa ubaya maana nitabeba mzigo wa watu mda wowote aiseee!!!. Swala la kufananisha watu ni baya sana