Wanajamii mnisamehe tu lakini sina budi kuuliza hata jukwaani yamkini nitasaidiwa. Msanii huyu aitwaye jina la usanii Mainda siku nyingi sijamuona akishiriki katika filamu yuko wapi jamani? Siyo siri mimi ni mshabiki wake napenda uigizaji wake. Nimekosa nimtafutie wapi lakini katika jukwaa naamini wapo wenye taarifa zake nisaidieni hata kama kuna uwezekano wa kupata contacts zake nitashukuru ili nafsi yangu ipate kuridhika. Sina nia ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi bali ni kutaka kujua tu wapi siku hizi shughuli zake za uingizaji anafanyia ili niwe naangalia huwa nafurahishwa sana actions zake.
Wanajamii naomba msaada wenu.
Wanajamii naomba msaada wenu.