Msanii wa Hiphop maarufu kama 'Roho 7' yu wapi siku hizi?

Unalilia kwenda kwenye kazi za kitumwa hizo rafiki yangu? Anyway bado hujayaona utabadilika baadae
SIYO KAZI YA KITUMWA NDUGU YANGU USITAFSIRI VIBAYA JESHI.SIONI UTUMWA WOWOTE KULE, POPOTE NI KAZI TUU MAANA POTE USIPOKUWA UKIONGOZWA NA MKUBWA WAKO, NI LAZIMA UJIONGOZE WEWE MWENYEWE IWE BIASHARA, SERIKALINI, KULIMA N.K LA SIVYO MAISHA YANASHINDIKANA.NAPENDA SANA JWTZ SEMA MZEE BABA KABANA SANA KULE SIKU HIZI, NAPALILIA KWELI KWELI RAFIKI YANGU BAS TUU.
 
Pole sana kwa kuwa na nia ya kwenda huko ila mi kazi zote hizo za JWTZ sijui na TISS na kwa mbaali Polisi mi huwa naziona za kitumwa sana.......ila komaa mkuu huenda ukapata nina jamaa zangu walienda huko mpaka leo wanatamani kutoka sema ndo hivyo wakitoka watakuja kula nini mtaani
 
Utatapeliwa humu ndugu yangu .
huyo unayemuomba msaada mwenyewe mwanafunzi 😀 😀 😀 😀 .
yko Udom anapambna na hali yake 😀

Hahahaa, mkuu umenichekesha sana.
-Kaveli-
 
Ni kweli kuwa Roho Saba ana undugu na YAKI?rapper mwingine pia alitamba kpnd hcho alikuwa anawakilisha Iringa km skosei
Yaki huyu jamaa alikuwa anaandika sana nyimbo enzi zake, sijui ilikuwaje akautupa mkono muziki.
 
Yaki huyu jamaa alikuwa anaandika sana nyimbo enzi zake, sijui ilikuwaje akautupa mkono muziki.
Hata sijui aisee sijui hata atakuwa wapi,,, sema life pia ni kitu kingine ambacho knawafanya watu wachange mwenendo wa maisha
 
Ni kweli kuwa Roho Saba ana undugu na YAKI?rapper mwingine pia alitamba kpnd hcho alikuwa anawakilisha Iringa km skosei
Wote walipotea baada ya producer amba kuamia dar tokea iringa.
Roho 7 alizaa na farida ambaye alikuwa msanii wa tetemesha aliyeingia kwenye game akiwa mdogo sana na wimbo wa pesa.
Yaki akaja kutoa wimbo wa we ni wangu ambao alimshirikisha farida kwenye chorus huku beat ikiwa ya crank from amba
Baadae yaki akatoa ngoma ya rafiki ikifuatiwa na tonight ambayo chorus kaimba amba mwenyewe sauti auto tune
Wasanii walikuwa wanatoka dar wanamfuata amba iringa mfano mheshimiwa temba kwenye ngoma ya maneno, na AY ngoma ya mikono juu, full shangwe hussein machozi, na kwa ajili yako.
Sema akahisi akija dar atamake zaidi kumbe ndo akapotea.
Ila now producer amba anatengeneza gospel ndiye alipika album ya ambone mwasongwe ile yenye nyimbo kama nguvu ya msamaha, kuokoka n.k
 
Umenikumbusha sana huyu jamaa, ila kwataarifa nilizonazo nikwamba aliingia jeshini
 
Acha Uongo ww, najua nataman life la mabaka baka sema umekosa opportunity ya kwenda huko pambana na hali yako wacha watu watimize wajibu wao
 
Daa angalau hata amekula shavu,nilitegeme nisikie ni teja liko chimbo limesiz kumbe jamaa anaakili hakuzolewa na umaarufu
 
Aisee,,umenikumbusha Farida a.k.a ReeKay,,sikuwa najua km alizaa na Roho Saba thanks kwa info,,,

Yaki alikuwa anajua sana sijui hata yuko wapi kwa sasa,, Kilichomkuta Amba nahisi ndo klichomkuta producer mwingine mkali toka Mwanza kwa kipindi flani alitamba sana Q The Don toka Mo recods,,huyu jamaa kuna kpnd flan alitamba sana na hata alitishia uwezo wa maproducer toka dar na kuna artist kbao walitoka dar n Arusha kuja Mwanza kufanya ngoma kina N2N, Makini,Jay Moe,Stopper ila alipoenda tu dar kufanya hits km CNN ya Ngwear jamaa hakutamba tena km ilivotegemewa
 
Roho saba alijiunga na jeshi baada ya kuhitimu masomo na sasa ni officer
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…