Msanii wa Kimataifa Alikiba kwenye headlines tena baada ya kupata dili nono hili tofauti na Sony!!

Msanii wa Kimataifa Alikiba kwenye headlines tena baada ya kupata dili nono hili tofauti na Sony!!

Eti dili za matangazo!!...kwa hiyo sasa mtakua mnasikliza na kutazama matangazo ya kiba sio mziki tena??...matangazo si hata mzee majuto anafanya??..wapi nyimbo na video kali??..au ndio hizo yooooo!! Yoooo!..hopeless!!

Kwa comment yako hii, kizaz chako kipo mtatani kwa uelewa, kama babu yao ndiyo una mawazo haya, basi sijui hao offsprings watakuaje
 
Msanii wa Kimataifa "Alikiba" anayetamba na kibao cha #Aje aendelea ku-make headlines Africa na dunian kote hasa baada ya kupata dili nono, Baada ya Kuwa offical brand ambassodor wa kampni kubwa la uuzaji wa Vifaa vya muziki Africa "AGK" lenye makao yake makuu South Africa, leo hi tena kapata dili nono la kuwaAmbassador wa Shirika kubwa la"Oliver jam Food foundation" lenye makao makuu uingereza linalojihusisha na afya, ubora wa chakula kwa watoto duniani, shirika hili lina partnership na WHO.

Ikumbukwe pia bado dili 4 ambazo msanii Alikiba ataisaini week ijayo kama sehemu ya mafanikio yake, ambapo madili haya nono yanamuweka Alikiba katika nafasi ya juu kama brand ya kimataifa. Kwahiyo hakuna shaka kwa sasa Alikiba ni msanii anyeongoza kwa kupata dili nono kwa wasanii wa Africa Mashariki.
Hongera sana Alikiba kwa kupata kusaini na Sony ambayo itakufanya "utoboe kimataifa" kama unavyosema mkataba wako au kama wewe na mashabiki zako wanavyoamini ( lolote linaweza kutokea tuache kutabiri ) Lakini kuna tatizo la watu kuelewa kwa makusudi au kwa kutokujua kipi ndio kipi na nini ndio nini, sasa kama mkuu hapa anatuambia eti " KAWA BALOZI WA DUKA KUUUUBWA LA UUZAJI WA VIFAA VYA MUZIKI AFRIKA LA AGK, acha kupotosha ukweli kama kufanikiwa atafanikiwa tu na si kwa kuongeza chumvi kwa watu kama sisi tulio na upeo mkubwa wa mambo na si wavivu wa kusoma na kutafuta habari. KUNA SHABIKI YAKE WA SOUTH NDIO ALIMPA OFA YA KUCHAGUA KIFAA CHOCHOTE CHA MUZIKI BURE BILA KULIPIA NA SI KWAMBA KAWA BALOZI WA HIYO KAMPUNI soma hii. PICHA 10: Alikiba yupo Johannesburg South Africa... hivi ni vitu unatakiwa kujua - MillardAyo.Com Lakini pia hiyo ya kuwa balozi wa oliver jam food foundation, NI KWELI KAWA BALOZI LAKINI NI " WAKUJITOLEA" KAMA ILIVYOKUWA KWA UBALOZI WA TEMBO NA SI VINGINEVYO SEMA LABDA ATAKUWA ANAPATA POSHO NA TIKETI ZA MAHALI ATAKAPOKUWA ANAHITAJIKA TU.
 
Mkuu kubishana si fan yangu bali kujifunza,

Imetokea sehemu nyingi tu hata huko Ulaya tunajua wazi Rooney analipwa kiasi gani pale Utd, Hali kadhalika tunajua ataondoka lini pale kulingana na ukomo wa mkataba wake.

Ninachojua mikataba inayokuwa ya kificho ni ya kifisadi au midogo isiyoendana na hadhi ya mtu au vitu vinavyopatana kwenye mkataba huo. Hii ndiomaana huwa na kificho ili kuficha maovu au kulinda hadhi ya waingia mkataba huo kwa maslahi ya wao wenyewe..!!!

Daimond tunajua kwenye wimbo wa Utanipenda alilipwa na Dr Mwaka Tsh 50Ml (kwaajili ya tangazo lake). Vilevile inajulikana hata kwenye mtaba wake na Voda alilipwa kiasi cha Tsh 600ml kama sikosei (I stand to be corrected) Sijafuatilia kwenye Tomato kujua alilipwa bei gani. Ila nadhani ukitaka kujua utajua tu labda aamue kukuficha kulingana na maelezo ya hapo juu.

Halafu nikuambie kitu mkuu,

Acha kushabikia vitu kiasi cha kutoweza kukosoa au kurekebisha popote, usiwe mtu wa kumeza tu, jaribu kufukunyua na kuchimba kile unachokipenda na kukithamini. Ni kwakufanya hivyo utakuwa unakilinda na kukiendeleza kwa wakati mmoja bila wewe mwenyewe kutambua.

Badilika mkuu.

BACK TANGANYIKA
cha kuongezea Davido kasign dili la $1mil Sony na iliwekwa wazi siku hiyo hiyo, sijajua kwa nn kwa kiba imefichwa.
 
cha kuongezea Davido kasign dili la $1mil Sony na iliwekwa wazi siku hiyo hiyo, sijajua kwa nn kwa kiba imefichwa.
We jamaa uko nyuma sana na habari za muziki na burudani kwa ujumla,mi nakushauri hebu kuwa shabiki tu hautopungukiwa na kitu. Sasa unadhani kila mkataba unaenda na mihela we wa wapi .......... Ina maana hata seven ( meneja wa kiba) alipokuwa anaelezea nini atakachonufaika nacho kiba ujakisikia ........... Ingekuwa inahusu mihela yule dada si ndio lingekuwa neno lake la kwanza........
 
Kama mtu anafanya vizuri lazima apongezwe. Tunahitaji naye awekeze na atoe ajira kwa wenzake na afanye investments.

Asisahau watoto saba alionao siyo mzaha awawekee msimamo wa maisha yao. Ni wakati mzuri kwake sasa kuwa na familia na kuachana na tabia ya kuwatongoza kina Gigy insta.

Kila la heri katika njia ya mafanikio lakini kumbuka hayo.
 
Kikubwa tuone output ya hayo madeal, sasa ni wakati wakuacha kuishi kwenye nyumba za mashuga mamy wake! Anunue nyumba akae kwake ili asiwe na stress za maisha ndo mashabiki watapata mziki mzuri, na mziki mzuri ndo mashabiki wanachokitaka
 
We jamaa uko nyuma sana na habari za muziki na burudani kwa ujumla,mi nakushauri hebu kuwa shabiki tu hautopungukiwa na kitu. Sasa unadhani kila mkataba unaenda na mihela we wa wapi .......... Ina maana hata seven ( meneja wa kiba) alipokuwa anaelezea nini atakachonufaika nacho kiba ujakisikia ........... Ingekuwa inahusu mihela yule dada si ndio lingekuwa neno lake la kwanza........
Povu la nini sasa? wewe uliyekuwa mbele ndo umeongea nini sasa hapo? kwa hiyo alichokuambia seven ndio umeona ndio conclusion? nimejaribu kueleza mikataba mingi sana ya local artisties haiwekwi wazi, mara nyingi inawanufahisha managements. jiongeze basi, sio kila atachokwambia seven ndio kimemaliza, kwa hiyo umeamini ally K kasign mkataba wa kusimamiwa kurecord na koshoot tu? ndio maelezo ya seven hayo uliyoyabeba wewe,kama kuna jambo lingine aliloongea seven kuhusu huo mkataba, leta wewe, zaidi ya blah, blah, za project nyingine.. lazima kuna manufaa ambayo anayapata hayako wazi, Ally kiba sio cheap kiasi hicho. next time jiongeze... kumbuka kuwa Ally kiba aliwahi kuwa na conflicts na Sony,... sio lazima nikuelezee maana wewe source zako ni story za meneja.
 
Hongera zake
Ila isiwe hawa sony ndio wale wakina rosemuhando na keko ( wa uganda ) na nakaya sumari waliwasainisha halafu wakapotea kimya ghafla
 
Kuna mtu anaitwa David Bisbal. Huyu jamaa Yuko chini ya Sony kwa more than a decade. Ashapewa shavu na watu Kama Miley Cyrus, Rihanna na wengineo, lakini Mimi bila kuishi nchini kwao nisingemfahamu. Kwahiyo kuwa chini ya lebo yoyote kubwa sio mwisho wa kila Kwenye game. Juhudi binafsi inahitajika bila kusahau bahati ya mtu.
 
Povu la nini sasa? wewe uliyekuwa mbele ndo umeongea nini sasa hapo? kwa hiyo alichokuambia seven ndio umeona ndio conclusion? nimejaribu kueleza mikataba mingi sana ya local artisties haiwekwi wazi, mara nyingi inawanufahisha managements. jiongeze basi, sio kila atachokwambia seven ndio kimemaliza, kwa hiyo umeamini ally K kasign mkataba wa kusimamiwa kurecord na koshoot tu? ndio maelezo ya seven hayo uliyoyabeba wewe,kama kuna jambo lingine aliloongea seven kuhusu huo mkataba, leta wewe, zaidi ya blah, blah, za project nyingine.. lazima kuna manufaa ambayo anayapata hayako wazi, Ally kiba sio cheap kiasi hicho. next time jiongeze... kumbuka kuwa Ally kiba aliwahi kuwa na conflicts na Sony,... sio lazima nikuelezee maana wewe source zako ni story za meneja.
We kweli Funza, sasa nisimuamini Meneja wake, ila unanilazimisha nikuamini wewe ambaye si meneja wake halafu unajiona uko sawa............... Halafu angalia jinsi ulinzokuwa funza eti "mikataba mingi ya local artisties haiwekwi wazi" LAKINI KICHWA CHA HABARI YAKO UNATUAMBIA HUYU NI "MSANII WA KIMATAIFA" huku ndani unasema yeye ni local artist, sasa kwa "UNDUMILAKUWILI" = (unafiki) huu unanitaka nikuamini wewe na si meneja wake, ziko sawa kichwani wewe .......... Manufaa anayapata kweli na keshayaeleza MENEJA WAKE usilete blah blah hapa,labda uniambie wewe ndio SEVEN MWENYEWE.
 
Hongera sana Alikiba kwa kupata kusaini na Sony ambayo itakufanya "utoboe kimataifa" kama unavyosema mkataba wako au kama wewe na mashabiki zako wanavyoamini ( lolote linaweza kutokea tuache kutabiri ) Lakini kuna tatizo la watu kuelewa kwa makusudi au kwa kutokujua kipi ndio kipi na nini ndio nini, sasa kama mkuu hapa anatuambia eti " KAWA BALOZI WA DUKA KUUUUBWA LA UUZAJI WA VIFAA VYA MUZIKI AFRIKA LA AGK, acha kupotosha ukweli kama kufanikiwa atafanikiwa tu na si kwa kuongeza chumvi kwa watu kama sisi tulio na upeo mkubwa wa mambo na si wavivu wa kusoma na kutafuta habari. KUNA SHABIKI YAKE WA SOUTH NDIO ALIMPA OFA YA KUCHAGUA KIFAA CHOCHOTE CHA MUZIKI BURE BILA KULIPIA NA SI KWAMBA KAWA BALOZI WA HIYO KAMPUNI soma hii. PICHA 10: Alikiba yupo Johannesburg South Africa... hivi ni vitu unatakiwa kujua - MillardAyo.Com Lakini pia hiyo ya kuwa balozi wa oliver jam food foundation, NI KWELI KAWA BALOZI LAKINI NI " WAKUJITOLEA" KAMA ILIVYOKUWA KWA UBALOZI WA TEMBO NA SI VINGINEVYO SEMA LABDA ATAKUWA ANAPATA POSHO NA TIKETI ZA MAHALI ATAKAPOKUWA ANAHITAJIKA TU.
watakuloga oh!
mtu ana deal za kimataifa af we unaleta taarifa zako hizi
ahaahahahhahahaha
 
Back
Top Bottom