Msanii wa kiume bongo movie apokonywa gari

Msanii wa kiume bongo movie apokonywa gari

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Muigizaji wa filamu za Kibongo,
Salim Omary ‘ Slim ’ amejikuta akiwekwa
nguvuni katika Kituo cha Polisi cha
Makangarawe , Yombo -Buza , jijini Dar
akidaiwa kugoma kurejesha gari aina ya
Land Lover Discovery walilopewa zawadi siku
ya ndoa .
Gari hilo walipewa na wakwe zake alipofunga
ndoa na binti yao aitwaye Asia Morgan ,
mwaka jana lakini ilipofika Mei mwaka huu
( takriban miezi tisa tu ndani ya ndoa ) , wawili
hao walitengana na kusababisha wakwe hao
wageuke mbogo kudai chao kwa maelezo
kwamba walitoa zawadi hiyo kwa binti yao
hivyo kwa kuwa wametengana , wanataka
chao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu, Asia alifikia
uamuzi wa kwenda kuishi nyumbani kwao
Tegeta , jijini Dar baada ya kushindwa
kuvumilia tabia ya wivu wa kupindukia
aliyokuwa nayo Slim .
“Baada ya kutengana wazazi wa msichana
huyo walimwambia Slim awakabidhi gari
moja kwa kuwa anayo mawili na kama
anataka Discovery ( Land Lover ) wamuachie
lakini wapate moja kwa ajili ya binti yao
kuendea chuo, ” kilisema chanzo.
Salim Omary ‘Slim ’ akiwa na aliyekuwa mke
wake .
Akizungumza kwa jazba, mama mzazi wa
Asia alisema , walimzawadia gari hilo kwa
kuwa wote walikuwa wanapenda tasnia ya
filamu hivyo gari hilo lingemsaidia yeye na
mume wake katika shughuli zao.
“Kinachouma ni kwamba tusingefikishana
hapa lakini tulishamuomba sana Slim
kurudisha gari hilo au ampe mwanetu gari
lingine abaki na hilo kama analipenda lakini
alikataa na mbaya zaidi ana kila kitu ,
kuanzia ufunguo na kadi ya gari kitu
ambacho hatendi haki kwa mtoto wetu, ”
alisema mzazi huyo.
kizidi kutema cheche mbele ya kinasa sauti
cha Ijumaa , mzazi huyo alisema licha ya
Slim kwenda Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania ( Bakwata ) kushtaki ili arudiane na
binti yao, haitawezekana .
“Nashindwa kuelewa kabisa jambo hili
nilijitahidi sana kulivumilia lakini nimeona
imeshindikana kabisa hivyo tuliamua kwenda
nyumbani na kumchukua kumfikisha kituoni
hapa maana sisi tulimfanya kama mtoto
wetu lakini yeye amekuwa mkaidi, ” alisema
mama huyo.
Salim Omary ‘ Slim’ akiwa katika kituo cha
polisi Makangarawe , Yombo -Buza .
Mwandishi wetu alimfuata Slim kituoni hapo
na kuzungumza naye kuhusiana na sakata
hilo ambapo alisema anachofahamu yeye ni
kwamba zawadi inapotolewa kwenye harusi
na wazazi inakuwa ni ya mke na mume lakini
anawashangaa wazazi hao kuidai ikiwa hata
mkewe hajampa talaka .
“Nashindwa kuelewa kabisa kwa sababu
wazazi wa mke wangu walitoa gari lile kama
zawadi sasa sielewi kwa nini walidai tena
wakati mke wangu sijamuacha, suala hili lipo
Bakwata .
“Isitoshe, gari hilo nimelitengeneza sana
mpaka kufikia lilivyo sasa kwani bado lipo
gereji, lakini kwa kuwa wameamua kunidai,
baada ya miezi mitatu nitakuwa nimewapa
gari lao, ” alisema Slim .
 
Attachments

  • 1411743882216.jpg
    1411743882216.jpg
    45.8 KB · Views: 1,484
Mariooo mwaka huu kwao mbaya huna uwezo w kumiliki gari unalzmisha utawapa after 3mnth,eti lilikua bovu kwani lililetwa na breakdown kitu c chako rudisha
 
Hahahah nicheke mie...eti baada ya miez mitatu atawapa why not now....mke hutak gari unataka..wanaume tumebak mimi na baba yangu tu
over

Bongo movie kwa kupenda vya bure khaa!! Hili nalo jamaa linajifanya kidume kumbe ndo wale wale marioo, we muache tu aendekeze kupenda vya bure soon mapedeshee watamtafuta
 
Mariooo mwaka huu kwao mbaya huna uwezo w kumiliki gari unalzmisha utawapa after 3mnth,eti lilikua bovu kwani lililetwa na breakdown kitu c chako rudisha

Ahahahaa eti kwani lililetwa na break down, si ndo apo, ata kama lililetwa na boko haramu cha mtu mavi slim, rudisha mali za watu, utaolewa oooh
 
Hahaahaaa hahahaaaa... Nicheke kama mazuri mie... Binamu mpaka mwaka uishe tutaona mengi mnoo

Mmh bongo movie kwa kupenda vya bure, yani maisha ya kuigiza mpaka kwenye real life, anauzia sura mwenyewe na gari la watu, khaa, wakina wema wahongwe hadi wewe unataka vya bure,mmh hatar hii wapi mapedeshee
 
Ahahahaa eti kwani lililetwa na break down, si ndo apo, ata kama lililetwa na boko haramu cha mtu mavi slim, rudisha mali za watu, utaolewa oooh

Huyo ----- tu gari c yako unaleta ujuaji,bongo movie mwisho wao 2014 yani watu walishawachoka c wakiume n kike wote life yao fekero tu
 
Huyo ----- tu gari c yako unaleta ujuaji,bongo movie mwisho wao 2014 yani watu walishawachoka c wakiume n kike wote life yao fekero tu

Eti anadai bado hajaachana na mke wake, uachane nae au usiachane nae wenye gari wanataka, na kama uliwadanganya mademu zako kuwa gari ulinunua leo mambo hadharan umeumbukaje?
 
Eti anadai bado hajaachana na mke wake, uachane nae au usiachane nae wenye gari wanataka, na kama uliwadanganya mademu zako kuwa gari ulinunua leo mambo hadharan umeumbukaje?

Karithi tabia z madam kusema kanunua audi na nyumba
 
Karithi tabia z madam kusema kanunua audi na nyumba

Leo siku yake chungu atatamani achimbe ardhi ajifukie, watu wanapenda maisha ya kwenye maigizo, yan mpaka polisi anapelekwa mmh, halafu akitoka apo anamrudia huyo mke wake mbona nitamuona mngese maana mpaka apo familia imekudharau sana
 
Waswahili sisi tunajuana kma hajampa talaka ni wake bdo ila gari c yake ni ya wakwe
 
Loh...

Angalau huyu kalengesha kuhongwa na wakwe...

Maana wengine wanaliwa viboga

Aibu kwa bongo mavi
 
Back
Top Bottom