Bongo supa staa ni kile waingereza huita monkey, see monkey do. Usishangae kesho akafanya mambo mengine kama usagaji baada ya kuona mastaa wa majuu wanavyofanya. Hamjaona wanavyojifanya kuigiza kiingereza au kukizungumza wakati wengi hakipandi na kama kinapanda wanakitumia mahali si pake? Ulimbukeni ni asili yao na usupastaa bongo si kingine bali ulimbukeni. Hata baadhi ya viongozi wamo kwenye kundi hili la malimbukeni. Wanapewa jezi za mpira kila waendako na hawang'aki. Huenda nao watachora tatuu siku si nyingi.