Msanii wa vichekesho, Joti jitathmini katika hili

Msanii wa vichekesho, Joti jitathmini katika hili

Sio kila entertainment ni kufundisha, mengine ni entertainment for the sake of entertainment.
Hatuwezi kuwa entertained na yasiyowezekana. Bongo movie wamezidi Utoto. Wananchi tunapiga kelele Polisi waache kubambikia watu kesi, lakini Bongo movie akiact kama Polisi anakwenda kumpekua mtuhumiwa wa madawa ya kulevya anamtoa nje mwenye nyumba halafu anapekua ndani akiwa Peke yake akikosa madawa anarudisha Taarifa nje Kwa bosi aliyemwacha na mtuhumiwa. Hata kama hatuwapendi Polisi lakini hawawezi kufanya ujinga huo. Lingine unakuta Bongo movie Askari mdogo labda Koplo anakwenda kumkamata RPC wake mla rushwa, hili jeshi gani Jamani au kuna mikoa RPC ni Konstebo? Ni vema waigizaji wakaigiza kitu sahihi ili kuifumdisha Jamii.
 
Usanii bila shule ni ujinga mtupu.Joti ni std 7 yeye ni stearing,yeye ni Director yeye ni kila kitu unategemea final product gani !.
Shule ipi unayoimaanisha? Hii hii ya kumaliza form 6 na kwenda chuo kikuu? Kama ni hii, je kwa walimu wepi?
 
Nimeangalia clip yake ya maigizo inayoitwa(kazi na ngono)katika igizo hili limeanza vema lakini ktk kumaliza nadhani lina utata. Joti aliigiza kama binti mwenye elimu ya digrii anayetafuta kazi, lakini bosi akamtaka kimapenzi ili ampe kazi na aliposhindwa kugawa uroda bosi hakumpa kazi.

Joti akarudi nyumbani na kumsimulia mama yake na hatimaye yeye mama na mtoto wakaambatana kwenda ofisini. Na walipofika ofisini mama akamkamata roba bosi na kutoka naye nje halafu Joti akakalia kiti cha bosi ofisini na kuanza kutumia desk top kama mfanyakazi.

Sasa kwanini nasema amekosea, igizo lilipoanza lilikuwa linaashiria kufundisha kupinga unyanyasaji wa kingono toka kwa mabosi, rushwa ya mapenzi. Lakini limeisha kwa kuteka ofisi. Watalam mnisaidie hii ni sawa ktk kuwasilisha ujumbe?

Joti ana vipengele vyake vinne vya uigizaji , 1. Nishai 2. Kiboga 3. Anduje 4. Babu

Kati ya hzo ni script za Kiboga ndo zinaongoza Kwa kulalamikiwa , mi nashauri aachane na script za Kiboga ( kujifanya mwanamke ) ikiwemo na hii uliyoielezea ...... Hata Mimi niliona hlo tatizo
 
Kikubwa script ifike mwisho haina haja yakutaka kujua inafikaje kikubwa tuandike mwanzo mwisho alafu tuka rekodi😃😃😃
 
mleta mada una ubongo uliosinyaa sana.

Kwanza hujui kutafsiri kazi ya sanaa.
Pili nampongeza joti kwa kuleta conflict kwenye namna ya upokeaji ambapo ni kazi nzuri ya sanaa kumchanganya mpokeaji wa kazi ile.
Tatu heb fanya kazi mwenzako ashaingiza siku ww ndo kwanza unaleta malalamiko jf kwan hao youtube na media zinazoonyesha hawajachambua kwakajua kua inamafundisho au haina.
Kazi nafanya na huenda hadi nakuzidi wewe kipato.Wewe unayejuwa kuchambtwa kazi za sanaa tupe uchambuzi wako tujifunze.
 
Kazi nafanya na huenda hadi nakuzidi wewe kipato.Wewe unayejuwa kuchambtwa kazi za sanaa tupe uchambuzi wako tujifunze.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] siwezi kukupinga kwa mawazo yako[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umeshasema ni vichekesho alafu unataka iwe kama tamthilia mkuu,
Lengo kubwa comedy movies ni kuchekesha, watu wakicheka lengo limetimia haijalishi imeishaje
Tena angeongeza zaidi angetoka nje ya lengo la comedy movies,
Ukitaka zenye mafundisho angalia tamthilia
Ni sawa na kumwambia stand up comedy au mc aongee point kama hutuba za viongozi
 
Back
Top Bottom