Msanii wa Vituko Show taabani kiuchumi

Msanii wa Vituko Show taabani kiuchumi

MZIMU

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
4,058
Reaction score
1,373
Nimekutana na Msanii huyu mkongwe Tanga Stendi ya Basi jana tarehe 20/07/2014. Hali nilio muona nayo sikuamini macho yangu kwamba ni yeye!. Nililazimika kumfuata na kumsalimia. Nikamuuliza Tofee, kulikoni?. Tofee ndio jina lake la kwanza la Usaniii. Kwa sasa anajulikana kwa jina la Usanii Kama Kimaro Mushi, kutoka na umahiri wake wa kuigiza lafudhi ya Kichaga katika maongezi ya kisanii.

Jina lake halisi ni Salimu Athumani. Kiufupi Mzee huyo anaonekana anaishi maisha ya kubahatisha kiasi kwamba hata hela ya kula inabidi apewe na wasamaria wema.

Katika vipindi vya vituko show anaokeana katika igizo la Kitimtim akiwa na wasanii wenzake Issa Makombe a.k.a Mapembe na Na Kijeba.

Kilichoniuma mimi ni kwamba, kwa kazi za kisanii alizocheza tu! hakupaswa kuishi maisha anayoishi ya kubatisha riziki kwa watakao mthamini. Mimi nimemuona na kumsikia katika tasnia za vichekesho tangu zamani na hua naangalia kazi zake.

Sikuamini kama mtu mwenye kufanya kazi mahiri kama zile anaweza kutangatanga asijue wapi atapata hela ya kula ya siku hiyo.

Na baadhi ya kazi zake kama vile kitimtim sio za zamani sana kiasi cha kua hivyo alivyo. Hizo picha za chini sio muenekano wake wa sasa. Kwa sasa nikama anaishi ndani ya pango na Kutoka Asubuhi.

Tofee 3.png

Tofeee 2.png

Toffee.png

Swali ni kwamba! BASATA, BONGOMOVIE, AL-Riyamy PRODUCTIONS, MZEE MAJUTO na Wadau wengine mko wapi juu ya dhulma hii ya Wasanii wakongwe kama hawa. Mbona kuna watu wana endesha magari kwa jasho la wazee hawa!

Natoa wito kwa vyomba vya habari kumfuatilia na hata kufanya nae Mahojiano. Nadhani taswira yake katika tasnia hii ni zaidi ya alivyokua Mzee small au Bibi kidude.
 
Last edited by a moderator:
Pole yake ila tusiharakie kulaumu. We ungemulize vipi anamaisha gani hapo Tanga. Mtu unaweza kuwa na afya mbovu kwasababu ya maradhi lakini ukawa na rasilimali au asset za maana. Usije na hukumu ya macho tena kukutana naye stendi. 'Its very wrong and simple conclusion of what we see in life' Maisha yetu wabongo tunajua, mwingine alishirikishwa kwasababu ya kipaji na ukute alilipwa pesa zake kama walivyokubaliana yeye akanywea zake kwa mnazi wengine wakawekeza. Sasa aliyenywea yake kwa
Mnazi utalaumu basata na kampuni aliyofanya nayo kazi? Pia zingatia huyo mzee alijitokeza kwenye
Media akiwa tayari aged, jiulize alitumiaje ujana wake? Si sekta ya usanii tu, wengi wamefanya kazi taasisi zenye mishahara mizuri lakini baada ya mkataba kuisha ukiwaona hutaamini kama aliwahi kufanya kazi. "Some of us are very poor in management of time and what we get".Huyo mzee anafahamika kwasababu alikuwa anaonekana kwenye media, wengi walikuwa na maisha mazuri kuliko huyo sasa wapo hoi ila kwasababu hawakufahamika kupitia media wanakufa kimya kimya.
 
Mkuu isome vizuri hiyo post yangu! Nimeongea kwa lugha ya ki utu uzima Mkuu. Hayo yote Mawili yapo. Lakwanza ndio limeletea hiyo hali ya pili. Nililivyo mdodosa majibu yake yanaondoa hiyo shaka yako mkuu.
 
Umesahau kumpiga picha
 
Umesahau kumpiga picha

Mkuu sikua nimejiandaa kukutana na hilo! Kwani nilipatwa na mshangao. Ila ni vyema vyombo vya habari vikamtafuta na kufanya nae documentary. Jamii inapaswa kulifahamu hili. Maana hua tunakaa sebuleni na kufurahia kazi zake kumbe mwenyewe anateseka.
 
we utakuwa na mapenzi nae binafsi tu, jenerali amejaribu kukuelekeza kwa kina lakini uelewi. Mi nakaa sebuleni nakunja na 4 kabisa coz' nimenunua sijaiba, kuchoka kimaisha ni suala la mtu binafsi usikute hata nduguze wamlimchoka we ukajiona una huruma kumbe wanaokuzunguka wanakuona una kimbelembele
 
Mhhh! Sasa hiyo wazungu wanaita speculations or Gossips. Still anahitaji kusaidiwa kwa yale mazuri aliyo yafanya!
 
Na ungemkuta ameulamba unge conclude mzee mambo yake supa. Unaweza kukuta yuko poa sema kwa kuwa umemkuta kituo cha basi na hakuvaa vizuri basi ukahukumu mzee kapinda!
 
Halafu labda alikuwa location ndo maana akavaa ovyo si unajua tena wachekeshaji wetu kibongobongo
 
Jamani someni vizuri hiyo post yangu! Mnataka mpaka watoto wajue naongelea nini! Kama issue ni Mavazi wala nisinge poteza muda wangu juu ya hili, kwani hata jina lake halisi ilikua silijui, ameniambia yeye mwenyewe. Kila nilicho andika hapa sija hadithiwa na mtu. Nimetumia lugha ya kiiungwana kuelezea scenerio nzima. Issue nzima ni kwamba mzee yupo kwenye hali tete! Na hilo sio jambo la kuficha. Hebu vyombo vya habari vimufuatilie pale Tanga ili viweze kuhojiana nae. Inasikitisha.

Mimi nadhani watu wenye akili timamu na wasio kua na akili za kushikiwa, wameshanielewa.
 
Naungana na mleta uzi juu ya kufanyika jitihada za kuenzi kipaji za Mzee Tofi, ni kweli amenza kuonekana kwenye screen akiwa tayari mtu mzima ila muda mrefu alikuwa anashiriki michezo ya jukwaani wakiwa na mzee Majuto pale Tanga.

Kuna baadhi ya michezo ilirekodiwa enzi hizo, ila ipo kwenye poor quality, ile ya VHS kabla hata ya kuibuka Bongo Muvi....ipo moja inaitwa "Mume wangu mlevi"

Inawezekana Mzee Tofi anakosa fursa kwa sababu makazi yake zaidi ni Tanga, fursa ni chache, tofauti na mwenzake Mzee Majuto ambaye mambo yanamuendea tambarare.

Naungana na wazo la mleta uzi juu ya kuenziwa kwa mzee Tofi, ana kipaji karibu hata sawa na Mzee Majuto kwa aliyewahi kuona michezo yake ya enzi hizo.

Tusisubiri akishafariki ndio tuwasikie akina Mzee Majuto wanamlilia kwenye media....."Mzee Tofi tumetoka naye mbali" blah blah blah...

Nadhani waandishi wa habari za burudani na michezo wamfuatilie, kama kuna uwezekano hata Majuto abanwe amkumbuke mwenzake....ila kama labda anasumbuliwa na tatizo la ulevi, au matumizi mabaya ya pesa...hiyo ni ishu nyingine...ila pia bado anaweza kusaidiwa/kushauriwa kwa hilo.
 
Nikiwa nae pale tanga mbele ya vijana wawili ambao inaonekana wanamfahamu nahuku wakimuonea huruma kama mimi, nilimuuliza Mzee Tofee. Vipi mzee au una unakunywa pombe kupita kiasi. Akanijibu huku wale vijana kuonekana kukubaliana nae, kwamba yeye hanywi pombe na wala havuti bangi.

Then I was speechless!
 
Hata bi Kidude kafa masikini na ustaaa wake wote ule.msanii hana faida nje ya kazi yake. Inatia huruma sana
 
Jamani someni vizuri hiyo post yangu! Mnataka mpaka watoto wajue naongelea nini! Kama issue ni Mavazi wala nisinge poteza muda wangu juu ya hili, kwani hata jina lake halisi ilikua silijui, ameniambia yeye mwenyewe. Kila nilicho andika hapa sija hadithiwa na mtu. Nimetumia lugha ya kiiungwana kuelezea scenerio nzima. Issue nzima ni kwamba mzee yupo kwenye hali tete! Na hilo sio jambo la kuficha. Hebu vyombo vya habari vimufuatilie pale Tanga ili viweze kuhojiana nae. Inasikitisha.

Mimi nadhani watu wenye akili timamu na wasio kua na akili za kushikiwa, wameshanielewa.

bab mimi nilikuwa nakuzingua!maisha ya waigizaji na wanamuziki wa bongo flava nayaelewa huhitaji kunihadithia tena sembuse huyo mzee najua atakuwa ana hali mbaya....
 
You won't get off easy because of only talent you have, if you don't work hard you are out. Things like panctuality, to be ready and excercising all the time and in your major field, you have to take outside classes ( learning new things ) all the time.
There are more than a million peoples in the World call themselves actors/actress, and only two percents of them are making a living at it. Most of those do commercials to pay the rent. The rest are doing any job even cleaning or living on help and hope.
Don't think talent is enough to get you through. You gotta have a strong technique and a good agent. Otherwise, try another field.
 
Salamander, you are right if all other factors concerning them remain constant but, with piracy, bad contracts, bad managers, irresponsible organs and bad wills of the producers with their companies, is like to tell Palestinian boys to fight the Israelis with stones while undergoing UN and NATO Weapons sanctions together with their brothers Arabs hypocrisy and cowardice to wards Israeli.

Especially for the Veterans.
 
Wasanii bongo bado hawajakaa kwenye line so inakuwa ngumu kutambua vipaji vyao dhamani yake.
 
Back
Top Bottom