Msanii wa Vituko Show taabani kiuchumi

Msanii wa Vituko Show taabani kiuchumi

Tujiulize kwanza kwanini wengine hawalalamiki maisha yakienda kombo kwanini iwe wasanii tu na ni kwanini nimsaidie mtu ambaye naye alikuwa na maisha yake mbona naye hakusaidia wenzake.Kila mtu na aubebe msalaba wake,tusitake sifa hapa za kujifanya eti tuna huruma sana,kama una huruma basi tuwasidie watoto yatima wasio na mbele wala nyuma. Mzee Cleopa msuya alisema umefika wakati sasa kila mtu abebe msalaba wake na huo ndio ukweli wenyewe.Hakuna mtu asiyejua maisha ya wasanii na hao wa muziki wa kizazi kipya wanavyofuja maisha ,halafu baadae utasikia oh tuwasaidie oh wamelitangaza taifa na tunasahau kuwa kila mtu anachangia ujenzi wa taifa kwa nafasi aliyonayo.
 
Tujiulize kwanza kwanini wengine hawalalamiki maisha yakienda kombo kwanini iwe wasanii tu na ni kwanini nimsaidie mtu ambaye naye alikuwa na maisha yake mbona naye hakusaidia wenzake.Kila mtu na aubebe msalaba wake,tusitake sifa hapa za kujifanya eti tuna huruma sana,kama una huruma basi tuwasidie watoto yatima wasio na mbele wala nyuma. Mzee Cleopa msuya alisema umefika wakati sasa kila mtu abebe msalaba wake na huo ndio ukweli wenyewe.Hakuna mtu asiyejua maisha ya wasanii na hao wa muziki wa kizazi kipya wanavyofuja maisha ,halafu baadae utasikia oh tuwasaidie oh wamelitangaza taifa na tunasahau kuwa kila mtu anachangia ujenzi wa taifa kwa nafasi aliyonayo.

Maisha hua hayako hivyo! Sio wote walioko Magerezani wanahatia, binadamu tumeumbwa tofauti, usimhukumu mtu kabla ya kumpa nafasi ya kumsaidia. Wapo wengine wanauwezo wa kuweka wakili na wakapindisha sheria, wapo wengine hawana uwezo wa kujitetea kabisa na kubaki kulia. Inahitaji watu wenye akili timamu sana kuwasaidia wanadamu wenzao walioko kwenye matatizo bila kuwakejeli kwamba wamejitakia wenyewe. Nobody is perfect, and everybody deserves a second chance. Sio wasanii wote wapo kwenye hali walizonazo eti kwasababu wanafuja maisha yao. Kuna kundi kubwa la watu wanaishi kwa ujanja ujanja tu kwa kwatumia jasho la wenzao. Wasanii ni watu ambao tunaona kazi zao katika majumba yetu kila siku! Haiwezikani ikawa idadi kubwa ya wasanii hawa wewe wanafuja maisha yao na idadi ndogo sana ndio ifanikiwe. Sihitaji kurudia katika posti zilizo pita kuhusu hali hii, rudia na usome post zote utapata majibu katika ninacho kwambia. It is easy to blame then to help. Hapa tunacho fanya sisi ni kuionyesha jamii kua, kuna tatizo. Watu wanahaki kujua mambo haya!

Ni vizuri kila mtu akapewa nafasi ya kuhukumiwa peke yake na sio Hukumu za jumla kama zinazotolewa na baadhi ya watu tunapokua tunajadili matatizo ya jamii.

Anyway, hua tunatofautiana uelewa. Lets be objective and rather not subjective.
 
Naungana na mleta uzi juu ya kufanyika jitihada za kuenzi kipaji za Mzee Tofi, ni kweli amenza kuonekana kwenye screen akiwa tayari mtu mzima ila muda mrefu alikuwa anashiriki michezo ya jukwaani wakiwa na mzee Majuto pale Tanga.

Kuna baadhi ya michezo ilirekodiwa enzi hizo, ila ipo kwenye poor quality, ile ya VHS kabla hata ya kuibuka Bongo Muvi....ipo moja inaitwa "Mume wangu mlevi"

Inawezekana Mzee Tofi anakosa fursa kwa sababu makazi yake zaidi ni Tanga, fursa ni chache, tofauti na mwenzake Mzee Majuto ambaye mambo yanamuendea tambarare.

Naungana na wazo la mleta uzi juu ya kuenziwa kwa mzee Tofi, ana kipaji karibu hata sawa na Mzee Majuto kwa aliyewahi kuona michezo yake ya enzi hizo.

Tusisubiri akishafariki ndio tuwasikie akina Mzee Majuto wanamlilia kwenye media....."Mzee Tofi tumetoka naye mbali" blah blah blah...

Nadhani waandishi wa habari za burudani na michezo wamfuatilie, kama kuna uwezekano hata Majuto abanwe amkumbuke mwenzake....ila kama labda anasumbuliwa na tatizo la ulevi, au matumizi mabaya ya pesa...hiyo ni ishu nyingine...ila pia bado anaweza kusaidiwa/kushauriwa kwa hilo.

true true true true.
 
Hebu toa hiyo miwani unatumia simu nini?Swali pia sijalielewa.

Hahaha! Mkuu imebidi ni cheke! nilikusudia hawajakaa vizuri kivipi? Na hili neno ''dhamani'' sijalielewa mkuu.
 
true true true true.

Pia tatizo nadhani wengi wetu tunadhani mzee Tofi kaibuka tu from no where, la hasha....nimeshaona baadhi ya michezo yake, wakiwa na Mzee Majuto enzi hizo (sema kama nilivyosema picha zipo kwenye poor quality)..ni miaka ya mwisho ya themanini na mwanzo ya tisini, so hata recording zake hazikuwa proper.

Sijui kama mtaamini Mzee Tofi alikuwa anavunja mpaka mapigo ya breakdance ya MJ....Wakazi wa Tanga wanaweza kumuelezea vizuri zaidi.
 
Jamaa alikua mahiri zaidi au sambamba na Mzee Majuto. Nipo angalia kazi zake hujawa sana na huzuni, vile ambavyo yuko leo.
 
Sikua najua kuwa huyu bingwa pia anaruka brakedance.
 
Back
Top Bottom