mfianchi
Platinum Member
- Jul 1, 2009
- 11,904
- 8,371
Tujiulize kwanza kwanini wengine hawalalamiki maisha yakienda kombo kwanini iwe wasanii tu na ni kwanini nimsaidie mtu ambaye naye alikuwa na maisha yake mbona naye hakusaidia wenzake.Kila mtu na aubebe msalaba wake,tusitake sifa hapa za kujifanya eti tuna huruma sana,kama una huruma basi tuwasidie watoto yatima wasio na mbele wala nyuma. Mzee Cleopa msuya alisema umefika wakati sasa kila mtu abebe msalaba wake na huo ndio ukweli wenyewe.Hakuna mtu asiyejua maisha ya wasanii na hao wa muziki wa kizazi kipya wanavyofuja maisha ,halafu baadae utasikia oh tuwasaidie oh wamelitangaza taifa na tunasahau kuwa kila mtu anachangia ujenzi wa taifa kwa nafasi aliyonayo.