MZIMU
JF-Expert Member
- Apr 29, 2011
- 4,058
- 1,373
Nimekutana na Msanii huyu mkongwe Tanga Stendi ya Basi jana tarehe 20/07/2014. Hali nilio muona nayo sikuamini macho yangu kwamba ni yeye!. Nililazimika kumfuata na kumsalimia. Nikamuuliza Tofee, kulikoni?. Tofee ndio jina lake la kwanza la Usaniii. Kwa sasa anajulikana kwa jina la Usanii Kama Kimaro Mushi, kutoka na umahiri wake wa kuigiza lafudhi ya Kichaga katika maongezi ya kisanii.
Jina lake halisi ni Salimu Athumani. Kiufupi Mzee huyo anaonekana anaishi maisha ya kubahatisha kiasi kwamba hata hela ya kula inabidi apewe na wasamaria wema.
Katika vipindi vya vituko show anaokeana katika igizo la Kitimtim akiwa na wasanii wenzake Issa Makombe a.k.a Mapembe na Na Kijeba.
Kilichoniuma mimi ni kwamba, kwa kazi za kisanii alizocheza tu! hakupaswa kuishi maisha anayoishi ya kubatisha riziki kwa watakao mthamini. Mimi nimemuona na kumsikia katika tasnia za vichekesho tangu zamani na hua naangalia kazi zake.
Sikuamini kama mtu mwenye kufanya kazi mahiri kama zile anaweza kutangatanga asijue wapi atapata hela ya kula ya siku hiyo.
Na baadhi ya kazi zake kama vile kitimtim sio za zamani sana kiasi cha kua hivyo alivyo. Hizo picha za chini sio muenekano wake wa sasa. Kwa sasa nikama anaishi ndani ya pango na Kutoka Asubuhi.
Swali ni kwamba! BASATA, BONGOMOVIE, AL-Riyamy PRODUCTIONS, MZEE MAJUTO na Wadau wengine mko wapi juu ya dhulma hii ya Wasanii wakongwe kama hawa. Mbona kuna watu wana endesha magari kwa jasho la wazee hawa!
Natoa wito kwa vyomba vya habari kumfuatilia na hata kufanya nae Mahojiano. Nadhani taswira yake katika tasnia hii ni zaidi ya alivyokua Mzee small au Bibi kidude.

Last edited by a moderator: