Heri ya chrismas na mwaka mpya!
nianze kwa kusema mimi sio shabiki wa bongo flavour napendelea sana hip hop na jazz
lakin hapa acha nitoe hii tathimin yangu kwenye bongoflavour kwa mwaka 2021 ambao tumeacha siku chache kuumaliza
kwenye muziki wetu wa bongo flavour naona jamaa marioo amefanya vema sana mwaka wote wa 2021 sana. almost ngoma zake zote alizotoa ndani ya mwaka 2021 ni kali na zimekuwa hit songs
nikiambiwa nimtaje msanii wabongo flavour aliefanya vizuri kwa mwaka 2021 basi ningesema marioo.
kwa upande wenu jf vipi?
mbali na huyo nilie mtaja, nani unaona amefanya vizurii zaidi mwaka 2021 kwenye bongo flavour?
mtu ambaye amezingua kwa mwaka huu naona ni ray vanny.. sisemi kama hajui, ila ajawa amsha amsha kwa mwaka huu.