MSD yaidai Serikali TSh 434.2 bilioni kwa huduma za bidhaa za afya vituoni

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya Ukimwi, imeishauri Serikali kukamilisha mchakato wa kuandaa sheria itakayosimamia huduma ya uvunaji, utunzaji na upandikizaji wa chembechembe na viungo vya binadamu ili kuweka msingi madhubuti wa utoaji wa huduma hiyo kwa wananchi.

Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo, Jumatatu Juni 2, 2025 Mwenyekiti wa kamati hiyo, Elibariki Kingu, amesema ni muhimu kwa Serikali kuweka mfumo wa kisheria utakaowezesha huduma hiyo kutolewa kwa ufanisi, usalama na kwa kuzingatia haki za binadamu.

Aidha, kuhusu magonjwa yasiyoambukiza, kamati hiyo imeshauri Serikali kuongeza juhudi za kupambana nayo kwa kufanya tafiti za kina kubaini ukubwa wa tatizo, kutoa elimu kwa umma juu ya vyanzo na njia za kujikinga, huku ikisisitiza umuhimu wa lishe bora, mazoezi ya mwili na ushirikishwaji wa sekta mbalimbali katika mapambano hayo.

Kwani MSD siyo serikali? MSD waseme wanadai vituo vya kutolea huduma kiasi hicho siyo serikali. Kwa serikali ni nini? Au ni dude gani hilo?
 
Watu watavunwa hata kama uwezekano wa kupona upo, siyo afrika hii.
 
Back
Top Bottom