BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai ametaja sababu za kusimama mradi huo ni kutoonesha tija na kuwa na ugumu kiutekelezaji.
Amesema mpango huo si kipaumbele chao, wanachokifanya kwasasa ni kuhakikisha wana Dawa za kutosha, Wanatekeleza Matakwa ya Kikanuni na Kuimarisha Muundo wa utendaji.
Ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa mwaka ulioishia Juni 30, 2021 ilionesha usambazaji wa Dawa nchini ni 34%, na kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo hadi kufikia sasa usambazaji umefikia 50%.
=====================
Bohari ya Dawa Nchini (MSD) imesema bima ya afya kwa wote haiwezi kuwa na mafanikio kama bei ya bidhaa za afya zitakuwa na bei kubwa. Serikali katika mkutano wa nane iliwasilisha Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ambapo umepelekwa katika kamati ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kujadiliwa.
Mkurugenzi Mkuu MSD, Mavere Tukai amesema hayo leo Jumatatu, Oktoba 17, 2022 wakati akielezea mnyororo wa ugavi wa bidhaa za afya.
“Bima ya afya kwa wote haiwezi kuwa na mafanikio kama bei ya bidhaa zitakuwa na bei kubwa na jukumu la Bohari ya Dawa ni kupambana kwa njia yote kuweza kupata bei shindani, tunanunua value for money (thamani ya fedha),” amesema.
Amesema jukumu lao ni kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinapatikana kwa gharama nafuu ambayo itaweza kuhakikisha mifuko ya bima inaweza kubeba. Amesema jukumu lao la pili ni kuhakikisha uwepo bidhaa na ubora wake.
Kuhusu deni wanaloidai Serikali, amesema mwaka jana Serikali ililipa zaidi ya Sh100 bilioni kutoka katika deni wanaloidai. “Madeni yakishahakikiwa yanawekwa katika kundi ya madeni yaliyohakikiwa na Serikali inalipa kwa hiyo tunalipwa,” amesema.
Kwa upande wa usambazaji wa dawa ambao katika ripoti ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa mwaka unaoishia Juni 30, 2021 walifikia lengo la asilimia 34, amesema kwa jitihada zilizofanyika hivi sasa usambazaji umefikia asilimia 50.
“Ni vizuri uende kwa mpangilio mzuri lakini hauvunji utaratibu kuliko ukaharakisha halafu zikaja hoja kila ulichonunua hukufuata utaratibu,” amesema. Aidha, amesema mradi wa usambazaji wa dawa kwa kutumia ndege zisizo na rubani umepumzika kwa sababu tija yake haijakaa vizuri.
“Tusidanganye ulikuwa ni mpango mgumu, utekelezaji wake ni kama tunahangaika kuwa na maghala mazuri, halafu unarusha kindege, unapeleka kitu fulani mahali fulani ni mpango utaendelea kuwepo lakini kwa sasa tunaona kama si kipaumbele,” amesema.
Amesema mpango huo si kipaumbele katika vipaumbele vikubwa na kwamba kipaumbele wawe na dawa, matakwa ya kikanuni na kuimarisha muundo wao.
MWANANCHI